ELIMU KUTOKA TANESCO
TOA TAARIFA SAHIHI NA KAMILI ILI KUPATIWA HUDUMA BORA NA KWA WAKATI
Mpendwa mteja wetu unapotoa taarifa kupitia njia zetu mbadala za Mitandao ya Kijamii
Whatsapp, Facebook,
Twitter Instagram Jamii forum,
Barua pepe nk unashauriwa kutoa taarifa kamili zitakazowawezesha wataalamu wetu na viongozi kukupatia Huduma bora na za haraka. Tunakuomba uzingatia yafuatayo[emoji116][emoji116]
1.
Jina la mtoa taarifa
Hii inatusaidia kumtambua mtoa taarifa kwenye mifumo yetu. Hakikisha unapewa namba ya Taarifa maarufu kama (TB namba) Ili mafundi wakiagizwa kuja kukuhudumia isije kutokea (wakagongana). Kama usipotoa taarifa ukapewa namba ya taarifa, mafundi wawili au watatu wanaweza kuja kwako kwa wakati mmoja.
2.
Eneo,
Wilaya,
kijiji Mtaa Hii inatusaidia kujua kazi fulani inafanyiwa kazi na ofisi ipi na kujua kama tatizo la eneo husika limeshatolewa taarifa na wateja wengine.
Mnaweza kuwa eneo moja lakini mnahudumiwa na transfoma au njia ya kusambaza umeme (feeder) tofauti
2.
Alama au mtu au kitu maarufu kilichopo eneo lako
Taja, Mfano nyuma ya ofisi ya Mbunge, karibu na Msikiti/Kanisa la eneo X, Ofisi za Serikali, Ofisi za watu binafsi , watu mashuhuri mfano kulia mwa Nyumba ya Msanii X iliyopo eneo la Madale nk.
3.
Namba ya simu
Namba ya simu ya mteja aliiyetoa taarifa au inayopatikana. Namba hii inatusaidia kumfikia mteja aliyetoa taarifa kwa wakati, na pia kumpigia mteja aliyetoa taarifa kujua kama alihudumiwa au bado.
4.
Jinsi ya kufika eneo husika
Toa maelezo ya ziada ya jinsi ya kufika nyumbani kwako ili hata wataalamu wetu wakifika na simu zako hazipatikani iwe rahisi kukupata au kuulizia kwa majirani zako.
5.
Elezea kwa ufasafa unachohitaji, unacholalamika, au unachoomba
Ni muhimu sana kutaja nini unakitolea taarifa ili wataalamu wa TANESCO wajue na kujiandaa kabla ya kufika kwako.
6.
Muda wa kutokea kwa tatizo
Kama ni hitilafu au tatizo linalohitaji ufumbuzi wetu tafadhali onesha tatizo limetokea tangu lini au hutokea muda gani.
6.
Namba ya mita
Kama ni tatizo la mita au taarifa zinazohusu manunuzi ya umeme uwe na namba ya mita na ni changamoto gani unaipata mfano: __Nikiingiza umeme mita namba xxx inaandika connect au error 77, FF1, Sleep, au nikinunua umeme wa shilingi kadhaa napata ujumbe fulani mfano
Insuffient balance nk_
7.
Namba ya taarifa
Kama mteja ulishatoa taarifa TANESCO kwa kupiga simu, au kufika TANESCO, anashauriwa kuonesha namba ya taarifa uliyopatiwa wakati wa kutoa taarifa na Ofisi Husika mfano
NMR042021TB-0008
Zingatia
Huduma bora inaanza na utoaji wa taarifa kamili na fasaha
TANESCO Tunayaangaza Maisha Yako