TANESCO: Bwawa la Mwalimu Nyerere (JNHPP) kuhusishwa na athari za mafuriko ya Kibiti na Rufiji ni kupotosha Umma

Na sisi hapa JF tunapenda kuufahamisha umma kwamba, uongozi wa CCM unajaribu kutumia kila njia kuonyesha hili tatizo halijasababishwa na Bwawa la Nyerere, pamoja na kuwapa TANESCO maagizo waseme hivi.

Tunaukumbusha umma kwamba wanasiasa sasa ndio wamekuwa mainjinia wa kutoa ufafanuzi, na mainjinia wako kimya. Wenye akili wote wanajua kwamba tatizo ni kwamba Bwawa la Nyerere lilijazwa maji kupita kiasi na bila mpangilio, na walipogundua hili wakaamua kufungulia maji mengi kulinusuru bwawa na kuepuka mafuriko makubwa hata zaidi ambayo yangeleta maafa makubwa sana ikiwa Bwawa lingepata madhara. Hii ingekuwa habari ya ulimwengu na aibu kubwa kwa Tanzania, kashfa mbaya kwa uongozi wa Tanzania. Lakini hawataki kukiri hili na kusema ukweli. Mbaya zaidi, wanawalaumu wananchi ambao wamewasababishia haya matatizo.

Tunajua kuwa TANESCO inabidi wakubali maelekezo toka juu kuhusu kutoa maelezo juu ya mafuriko ya Rufiji kwa sababu tu ya kulinda ugali wao na ule wa chama tawala. Tunawaelewa, lakini wanapaswa pia kuelewa wanashiriki dhambi ya wanasiasa. Tunatumaini dhamiri zao zitawishitaki.

Tungenda Tanesco wajibu ndio au hapana kwa maswali haya mawili;

  1. Je, ni kweli kwamba maji yalipofunguliwa Bwawa la Nyerere yalifunguliwa katika flow rate ambayo ilijulikana ingepeleka maji mengi downstream ambayo yangesababisha mafuriko?
  2. Je, ni kweli kwamba katika kipindi cha mwaka mzima cha masika na kiangazi, ikiwa maji yangeruhusiwa kupita kwa kiwango cha wastani unaokubalika, mafuriko yasingetokea kwa sababu ya dry and wet season flow rates balancing effect lakini hilo halikufanyika kwa kutaka Bwawa la Nyerere lijae haraka?
TANESCO tayari hatuwaheshimu, sasa msitake kutupa sababu nyingine ya kutowaheshimu.

Ushauri wetu kwenu ni kwamba, badala ya kutumia ubongo wa wanasiasa ku-manage maji ya bwawa la Nyerere, tumieni computer programe kama inavyotakiwa - flow in rate-retention-flow out rate. Mngefanya hivi, angalau mngewapa tahadhari wananchi miezi minne hata mitano kabla ya mafuriko, kama kweli tatizo lilikuwa ni natural weather issue. Lakini mkaamua kuwa watu wenye macho mnaokubali kuongozwa na vipofu.
 
Rufiji mafuriko yapo toka enzi....nakumbuka wimbo wa mbaraka mwinshehe
 
Shida ya wabongo tukisikia mashirika ya Umoja wa Mataifa (UNESCO na WWF n.k ) tunahisi sijui wao ni miungu. Hayo mashirika yanaongozwa na watu kama wewe tu hayo majina yasifanye muwe mnanyenyekea kila wanachosema na kuhisi wao ni Mungu.

Kwa taarifa yao tu hayo mashirika huwa yana skendo nyingi na taarifa zao zimekuwa zikigubikwa na utata rejea ile report ya DOING BUSINESS ambayo watanzania tulikuwa tunafanya reference kwa kila kitu lakini baadaye ikaja kugundulika waandaaji walikuwa wanapokea rushwa na kuzipendelea baadhi ya nchi.

Kwa hiyo tusipende sana kuamini wanacho kisema wao bila kujiridhisha huo ni utumwa wa fikira.
Asante
 
Walivyosema wanafungulia maji kutoka kwenye bwawa, ili maanisha nini? Mafuriko ni ya maji yaliyopunguzwa kutoka kwenye bwawa, wanabisha nini?
 
Hilo lipo wazi, Bwawa limemeza maji kwa kadri ya uwezo wake, yaliyozidi lazima yapite..
 
T14 Armata
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…