Wewe unamuamini waziri mkuu?Raisi ,waziri mkuu na waziri wa nishati Kwa nyakati tofauti walituahidi kuwa ujenzi wa bwawa la imeme ukikamilika tutakuwa na imeme wa kutosha., hivyo, bei itapungua. Sasa tumuamini nani Kati ya Maharage au muheshimiwa Raisi?
Kazi kweli kweliLicha ya gaharama za uzalishaji wa umeme kutarajiwa kushuka baada ya kukamilika kwa Bwawa la kuzalisha umeme la Julius Nyerere (JNHPP) Juni 2024, imebainika kuwa uzalishaji huo hautapunguza bei ya umeme kwa wateja.
Bwawa hilo linatarajia megawati 2,115 za umeme zitakazoingizwa katika Gridi ya Taifa.
Hayo yameelezwa leo Julai 27 na Mkurugenzi wa Tanesco, Maharage Chande katika kikao kazi kati ya Tanesco na msajili wa hazina na wahariri wa vyombo vya habari lengo kuelezea mafanikio na kazi za shirika hilo.
Amesema kwa mwaka 2020/2021 gharama ya uzalishaji wa umeme ulikuwa Sh1.5 trilioni ikilinganishwa na ongezeko la Sh 1.6 trilioni kwa mwaka 2021/2022.
"Mradi wa Mwalimu Nyerere ukikamilika gharama za umeme zitashuka lakini hatutashusha bei kwasababu tutashindwa kwenda," amesema.
Chande alitoa mchanganuo wa matumizi ya umeme kwamba mpaka sasa shirika hilo linawateja milioni 4.4, ambao miongoni mwao wateja wa viwandani ni 4,000 na majumbani zaidi ya milioni tatu.
Kiwango hicho kinawafanya wananchi kutumia asilimia 50 ya megawati 1400 zinazozalishwa na Tanesco kila siku na viwanda nako ni asilimia 50.
Kuhusu upotevu wa umeme, Makamu Mkurugenzi wa uzalishaji umeme Tanesco, Pakaya Mtamakaya amesema mwaka 2020/2021 upotevu ulikuwa wa asilimia tisa lakini kufikia 2021/2022 upotevu ukipungua kufikia asilimia 8.
Amesema sababu ya upotevu wa umeme ni umeme wenye kilovoti ndogo kusafirishwa umbali mrefu na sasa wanaendelea na mkakati wa kupunguza upotecy wa umeme.
Kuhusu bwawa la Nyerere
Ifikapo Juni, 2024 mradi huo utaanza kuzalisha.
Chanzo: Mwananchi
Pia soma: Habari njema: Bei ya umeme kushuka kutoka Sh.600/= hadi Sh. 35/= kwa unit moja bwawa la Nyerere likikamilika
Mjinga sana wewe jamaa, Dkt Magufuli alitupenda sana watanzania, alifanya kazi kwa uzalendo. Bei ya umeme inatakiwa kupungua.Uwo ndio ukweli, sio siasa za mwenda zake
Exactly, lengo ni kutufanya tusiwe competitive, mkishusha bei ya umeme inamaana wawekezaji wa viwanda watakuja soko la viwanda vya ulaya na china litakufa, vita ni kubwa sana tena sana ila tunaamini ukombozi waja very soon chini ya Dkt Samia, atawafukuza wanafiki wote.Au ni masheti ya mikono ya IMF. Ghana wana masharti ya mikono toka IMF kwamba waongeze bei ya umeme. Kwa kuwa hayo masharti nafuu ya mkopo hatuyajui ndo maana inakuwa ngumu sana kujua kwa nini tanesco wanasema hivyo. Mpaka sasa sababu zao ni nyepesi sana.
Naunga mkono hojaMASHETANI WAKUBWA
Mods unganisha huu Uzi hapaLicha ya gaharama za uzalishaji wa umeme kutarajiwa kushuka baada ya kukamilika kwa Bwawa la kuzalisha umeme la Julius Nyerere (JNHPP) Juni 2024, imebainika kuwa uzalishaji huo hautapunguza bei ya umeme kwa wateja.
Bwawa hilo linatarajia megawati 2,115 za umeme zitakazoingizwa katika Gridi ya Taifa.
Hayo yameelezwa leo Julai 27 na Mkurugenzi wa Tanesco, Maharage Chande katika kikao kazi kati ya Tanesco na msajili wa hazina na wahariri wa vyombo vya habari lengo kuelezea mafanikio na kazi za shirika hilo.
Amesema kwa mwaka 2020/2021 gharama ya uzalishaji wa umeme ulikuwa Sh1.5 trilioni ikilinganishwa na ongezeko la Sh 1.6 trilioni kwa mwaka 2021/2022.
"Mradi wa Mwalimu Nyerere ukikamilika gharama za umeme zitashuka lakini hatutashusha bei kwasababu tutashindwa kwenda," amesema.
Chande alitoa mchanganuo wa matumizi ya umeme kwamba mpaka sasa shirika hilo linawateja milioni 4.4, ambao miongoni mwao wateja wa viwandani ni 4,000 na majumbani zaidi ya milioni tatu.
Kiwango hicho kinawafanya wananchi kutumia asilimia 50 ya megawati 1400 zinazozalishwa na Tanesco kila siku na viwanda nako ni asilimia 50.
Kuhusu upotevu wa umeme, Makamu Mkurugenzi wa uzalishaji umeme Tanesco, Pakaya Mtamakaya amesema mwaka 2020/2021 upotevu ulikuwa wa asilimia tisa lakini kufikia 2021/2022 upotevu ukipungua kufikia asilimia 8.
Amesema sababu ya upotevu wa umeme ni umeme wenye kilovoti ndogo kusafirishwa umbali mrefu na sasa wanaendelea na mkakati wa kupunguza upotecy wa umeme.
Kuhusu bwawa la Nyerere
Ifikapo Juni, 2024 mradi huo utaanza kuzalisha.
Chanzo: Mwananchi
Pia soma: Habari njema: Bei ya umeme kushuka kutoka Sh.600/= hadi Sh. 35/= kwa unit moja bwawa la Nyerere likikamilika
Walijihami kujenga imani ila ni debe tupuTumepigwa NDOIGE...Wakati wanajenga walituambia bei ya kununua umeme itapungua ila sasa Maharage kashasema hawapunguzi.
Haya DPW wanakuja wanatuambia Mapato yataongezeka na ajira zitaongezeka sana ,wakishaanza kupiga mzigo tu ndiyo biashara ishakwisha hata mapato yakipungua na waliokuwa na ajira kuondolewa kwasababu ya uwepo wa mashine za kisasa hakuna wa kumuuliza....Kuna la Kujifunza hapa.