MGOGOHALISI
JF-Expert Member
- Apr 16, 2011
- 3,294
- 4,920
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza.
Licha ya waziri wa nishati kuelekeza kuwa wananchi waunganishiwe umeme kwa 27,000 tanesco Dodoma bado wamekaidi agizo hili. Wameamua kuwaunganisha wateja wenye nguzo karibu na nyumba zao huku wengine wakiambiwa walipie gharama za kuwasogezea nguzo karibu. Mbaya zaidi hata nguzo walizotawanya mitaani hawataki kuzisimika kitendo kitakachofanya kila mtu kuwa karibu na nguzo, wameziacha chini zinaliwa na mchwa.
Wananchi wa Dodoma wanamuomba waziri wa nishati atembelee mitaa kama Makulu, Chidachi karibu shule ya St Marys, Iringa road na kwingineko. Nguzo zimebwagwa chini ni miezi mitatu sasa na hakuna kinachoendelea.
Yote hii ni kutaka kupata sababu ya kuwatoza wahitaji wa umeme zaidi ya kiwango alichoagiza waziri.