TANESCO haitakiwi itetewe Wala kuhurumiwa, ijitetee na isimamiwe

Chendembe

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2019
Posts
459
Reaction score
500
Mambo ni mengi mno kuihusu TANESCO hali inayoweza kuchafua hali ya nchi.

Ni ngumu kueleweka na jamii unaposimama kulitetea au kuliongelea shirika kubwa kuliko yote hapa nchini.

Kwa muundo wa uendeshaji wa shirika hili na mashirika mengine ya umma, Ni serikali pekee kupitia wizara husika ndio inaweza kuwajibisha watendaji wa Shirika hili.

Hakuna chombo mahususi chenye Mamlaka ya kukagua uendeshaji na uwajibikaji wake kwa jamii zaidi ya Wizara husika na serikali.

Wizara inapokuwa sehemu ya shirika, na au kuwa msemaji wa TANESCO, jamii inakosa matumaini juu ya adha ya dharau, rushwa, upendeleo na huduma zisizoridhishwa za shirika hili.

Jamii inataraji Wizara kusimama na jamii katika kuboresha huduma na si vinginevyo.

Pamoja na kwamba idara ya elimu ukaguzi nayo sikuizi imemezwa na siasa na wanasiasa wamepora majukumu yake

NASHAURI kuwa na kitu Kama hiki kwa Wizara ya Nishati na wizara zingine zinazosimamia mashiri ya umma nchini.

Nawasilisha
 
TANESCO dawa yao ni kuwa na mashirika mengi ya ugavi wa umeme Ili wapate ushindani kama upande wa mawasiliano TTCL walivyofanyiwa!!
 
Tanesco hii ya Tanzania au ya nchi gani? Because Tanesco ya Bongo haiteteki hata wangemwajiri Adv. Kibatala & Rudy Guiliani!
 
Kusema kweli Tanesco Wana dharau Sana Kwa wateja wao na majibu ya kebehi, utafikiri hio huduma hatulipiii. Mimi ninaeongea hii ni karibu mwezi mzima hatuna umeme, walisema transformer Lina tatizo wakaja wakalitoa, Sasa hivi ukifuatilia wanakwambia eti hawana gari la kubebea transformer kulirudisha mahali walipolitoa. Inasikitisha hata ukiwasikiliza majibu Yao, hao ni Tanesco mlandizi
 
TANESCO dawa yao ni kuwa na mashirika mengi ya ugavi wa umeme Ili wapate ushindani kama upande wa mawasiliano TTCL walivyofanyiwa!!
Miundombinu ya simu ni wireless networks. Miundombinu ya umeme ni wired networks. Kuwepo kwa makampuni mengi ya umeme ni vurugu kubwa kwa mandhari ya miji yetu. Kila kampuni litaleta nguzo na nyaya zake, na litapitisha popote pale ili mradi limfikie mteja. Huo utakuwa mji?
 
Mambo ni mengi mno kuihusu TANESCO hali inayoweza kuchafua hali ya nchi.

Ni ngumu kueleweka na jamii unaposimama kulitetea au kuliongelea shirika kubwa kuliko yote hapa nchini.

Kwa muundo wa uendeshaji wa shirika hili na mashirika mengine ya umma, Ni serikali pekee kupitia wizara husika ndio inaweza kuwajibisha watendaji wa Shirika hili.

Hakuna chombo mahususi chenye Mamlaka ya kukagua uendeshaji na uwajibikaji wake kwa jamii zaidi ya Wizara husika na serikali.

Wizara inapokuwa sehemu ya shirika, na au kuwa msemaji wa TANESCO, jamii inakosa matumaini juu ya adha ya dharau, rushwa, upendeleo na huduma zisizoridhishwa za shirika hili.

Jamii inataraji Wizara kusimama na jamii katika kuboresha huduma na si vinginevyo.

Pamoja na kwamba idara ya elimu ukaguzi nayo sikuizi imemezwa na siasa na wanasiasa wamepora majukumu yake

NASHAURI kuwa na kitu Kama hiki kwa Wizara ya Nishati na wizara zingine zinazosimamia mashiri ya umma nchini.

Nawasilisha

jiwe aliweza kuendesha miaka mitano nchi bila umeme kukatika!!Leo tumerudi kule kuleeee[emoji3]
Na kuna wasomi wanajifanya wanaakili sasa hata umeme wa uhakika n ndoto
 
Hakika Kuna baadhi ya watumishi ni shida, wanapenda kuandaa mazingira ya rushwa.
Mbaya zaidi Ni pale upatwapo na tatizo kuihusu TANESCO Hakuna kwa kukimbilia kupata msaada. Jaribu kwenda Wizarani ushangazwe na msaada utakaopewa.

Kusema kweli Tanesco Wana dharau Sana Kwa wateja wao na majibu ya kebehi, utafikiri hio huduma hatulipiii. Mimi ninaeongea hii ni karibu mwezi mzima hatuna umeme, walisema transformer Lina tatizo wakaja wakalitoa, Sasa hivi ukifuatilia wanakwambia eti hawana gari la kubebea transformer kulirudisha mahali walipolitoa. Inasikitisha hata ukiwasikiliza majibu Yao, hao ni Tanesco mlandizi
 
Miundombinu ya simu ni wireless networks. Miundombinu ya umeme ni wired networks. Kuwepo kwa makampuni mengi ya umeme ni vurugu kubwa kwa mandhari ya miji yetu. Kila kampuni litaleta nguzo na nyaya zake, na litapitisha popote pale ili mradi limfikie mteja. Huo utakuwa mji?
Watu wanashindwa kufikiria hilo. Watakuja na underground cables sasa sijui utasambazaje na miji yetu hii ambayo haijapangwa
 
Back
Top Bottom