TANESCO hiki mnachofanya tuite wizi, ukwapuaji, unyang'anyi, au uhujumu uchumi

BANDOKITITA

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2022
Posts
1,484
Reaction score
2,852
TANESCO kwa nini mbona mnakwapua pesa za wanyonge bila huruma. Mwanzo wananchi walipiga kelele kuwa mmepandisha kodi ya jengo kutoka 15,000/= hadi 2,000/=lakini mlikuja kukanusha huku ukweli mkiujua.

Sasa hivi kuna uhuni unaofanywa wakati wa kununua umeme kuliko hapo awali. Sasa hivi karibu kila mtu anaenunua umeme lazima akutane na kipengele cha DEBT COLLECTED. Hapa Kuna makato yasiyoeleweka. Hata km mteja hadaiwi lazima hicho kipengele kikuhusu tena hapa wanakata pesa nyingi sana kuanzia elfu 3,000/= na kuendelea.

Bila kujitokeza na kutoa ufafanuzi juu ya makato haya, tutaendelea kuamini kuwa hili shirika ni chanzo cha kuwafanya wananchi masikini wa kutupwa kutokana na dhuluma.
 
FB_IMG_1721559534987.jpg
 
Nasikia za chinivini wanataka kuweka elfu tatu
 
TANESCO kwa nini mbona mnakwapua pesa za wanyonge bila huruma. Mwanzo wananchi walipiga kelele kuwa mmepandisha kodi ya jengo kutoka 15,000/= hadi 2,000/=lakini mlikuja kukanusha huku ukweli mkiujua.

Sasa hivi kuna uhuni unaofanywa wakati wa kununua umeme kuliko hapo awali. Sasa hivi karibu kila mtu anaenunua umeme lazima akutane na kipengele cha DEBT COLLECTED. Hapa Kuna makato yasiyoeleweka. Hata km mteja hadaiwi lazima hicho kipengele kikuhusu tena hapa wanakata pesa nyingi sana kuanzia elfu 3,000/= na kuendelea.

Bila kujitokeza na kutoa ufafanuzi juu ya makato haya, tutaendelea kuamini kuwa hili shirika ni chanzo cha kuwafanya wananchi masikini wa kutupwa kutokana na dhuluma.
Mimi juzi nilishindwa kununua umeme kwenye simu, nikaenda Tanesco nakutq ninadeni la tsh 21,000/= Bila kujua limetoka wapi wakati kila mwezi nanunua umeme na ninakatwa kila mwezi. Kweli Tanesco wamekua wezi hasa
 
Pengine ni njia mojawapo ya serikali kujipatia kipato ili kugharimia mishahara ya watumishi wake. Si unaona siku hizi ulipaji wa mishahara unavyofanyika bila tarehe maalumu kama ilivyokuwa imezoeleka huko nyuma. Kibubu hakina salio maana kila pembe ya nchi wenye mamlaka yao na mafisadi yanatafuna nchi.
 
Mimi juzi nilishindwa kununua umeme kwenye simu, nikaenda Tanesco nakutq ninadeni la tsh 21,000/= Bila kujua limetoka wapi wakati kila mwezi nanunua umeme na ninakatwa kila mwezi. Kweli Tanesco wamekua wezi hasa
Hili shirika ni sumu kwa maendeleo ya watanzania
 
Ungeanza na matusi ya nguoni ili wakutafute.lakini ukiandika hivyo. IgP atakwambia DRAMA
 
Umeuliza swali zuri sana. Kwanini hawana huruma?

Ni kwasababu hauna cha kuwafanya. Au nasema uongo ewe Mtanzania muoga?
 
Back
Top Bottom