TANESCO hivi ni sahihi taa 6 za watt 3 kula umeme unit 1 kwa usiku mmoja?

mr pipa

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2021
Posts
4,335
Reaction score
9,286
Zaman usiku mmoja ilikuwa inakula point 35

Naona kadri siku zinavyokwenda matumizi yanapanda. Hakuna tv wala pasi wala sabufa ni nyumba tu ambayo nimeijenga kwaajili ya dharura na hakai mtu, na nimfuatiliaji

Naombeni maarifa kidogo kwenye hili jambo

TANESCO
 
Kinachokula umeme hasa ni vifaa duni vya umeme.
Hasa ile Earth rod isiyo na copper kwa 100.
Ipime kwa sumaku, ikinasa tu hapo ni fake.
Mafundi hununua Earth rod za elfu 10 mpaka 15 ili wabane pesa.
 
Zaman usiku mmoja ilikuwa inakula point 35

Naona kadri siku zinavyokwenda matumizi yanapanda. Hakuna tv wala pasi wala sabufa ni nyumba tu ambayo nimeijenga kwaajili ya dharura na hakai mtu, na nimfuatiliaji

Naombeni maarifa kidogo kwenye hili jambo

TANESCO
Habari mr pipa, asante kwa kuwasiliana na TANESCO Huduma kwa Wateja na pole kwa changamoto hiyo.

Tunapenda kukufahamisha kuwa kwa kawaida, taa 6 zenye uwezo wa watt 3 pekee haziwezi kutumia uniti 1 ya umeme kwa usiku mmoja katika matumizi ya kawaida. Hata hivyo, matumizi ya umeme yanaweza kuongezeka kutokana na sababu mbalimbali, ikiwemo muda mrefu wa kuwasha taa, hitilafu katika mfumo wa ndani wa umeme (wiring), kuvuja kwa umeme (leakage), au uwepo wa kifaa kingine kinachotumia umeme bila kutambuliwa.

Iwapo una uhakika kuwa hakuna kifaa kingine kinachotumia umeme, tunakushauri ukague mfumo wa umeme wa ndani kupitia fundi umeme mwenye sifa ili kubaini kama kuna hitilafu inayosababisha matumizi makubwa ya umeme.

Asante kwa ushirikiano wako. ^GK
 
Safi sana, mko makini. Nyinyi siyo watanzania ehe?
 
Ivi switch ya kwenye socket au yaa taa ikiwa on wakati hakuna kifaa Cha umeme connected umeme unatumika?
 
Glory acha zako, hii imekuwapo sana na hili jibu tulilitegemea kabisa. Hakunaga jingine?
 
wiring haina shida, mbona mchana haili umem hiyo wiring
Unapimaje matumizi ya umeme ya mchana na ya usiku? Kama kuna leakage mahali hata usipowasha taa umeme unaenda labda uwe unazima circuit breaker kabisa.

Wiring yako either vifaa duni au fundi duni au vyote acha kukaza fuvu.

Au kwa vile haikaliwi na mtu basi usiku kuna misukule ya mtu inalala humo ndiyo inatumia hiyo unit 1/siku.

TANESCO haiwezi kuhusika kwa namna yoyote hapo.
 
we jamaa wewe mungu anakuona
 
Habari mr pipa, asante kwa kuwasiliana na TANESCO Huduma kwa Wateja na pole kwa changamoto hiyo.

Tunapenda kukufahamisha kuwa kwa kawaida, taa 6 zenye uwezo wa watt 3 pekee haziwezi kutumia uniti 1 ya umeme kwa usiku mmoja katika matumizi ya kawaida. Hata hivyo, matumizi ya umeme yanaweza kuongezeka kutokana na sababu mbalimbali, ikiwemo muda mrefu wa kuwasha taa, hitilafu katika mfumo wa ndani wa umeme (wiring), kuvuja kwa umeme (leakage), au uwepo wa kifaa kingine kinachotumia umeme bila kutambuliwa.

Iwapo una uhakika kuwa hakuna kifaa kingine kinachotumia umeme, tunakushauri ukague mfumo wa umeme wa ndani kupitia fundi umeme mwenye sifa ili kubaini kama kuna hitilafu inayosababisha matumizi makubwa ya umeme.

Asante kwa ushirikiano wako. ^GK
ndugu mheshimiwa TANESCO dah aya sina neno ngoja nimlete fundi kwanza
 
Ivi switch ya kwenye socket au yaa taa ikiwa on wakati hakuna kifaa Cha umeme connected umeme unatumika?
Habari bless on,
asante kwa kuwasiliana na TANESCO huduma kwa wateja, tunapenda kukufahamisha kuwa Soketi ikiwa imewashwa bila kifaa chochote kuunganishwa, umeme hautumiki.^HN
 
Upo wapi boss? Ukipress button ya kwenye circuit breaker ina trip? Kama haitrip jua kabisa kama kuna uvujaji wa umeme unit zitalika tu maana protective switch gears hazina ushirikiano maana ingekua short circuit mcb ingetrip
 
Back
Top Bottom