Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu wateja wake kuwa changamoto iliyojitokeza leo asubuhi katika njia za manunuzi ya umeme (LUKU) imefanyiwa kazi. Kwa sasa wateja wetu wanaweza kufanya manunuzi ya umeme kupitia njia zote za mawakala, mitandao ya simu na njia za kibenki.
Shirika linawashukuru wateja wake kwa uvumilivu katika kipindi chote ambacho changamoto hii ilijitokeza.