TANESCO inarudi mikononi mwa mafisadi?

TANESCO inarudi mikononi mwa mafisadi?

technically

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2016
Posts
12,706
Reaction score
52,355
Mafisadi walianza muda mrefu Sana kuila tanesco record zinaonyesha TANESCO ilianza kuliwa toka mwaka 1994.

Magufuli alipoingia akajaribu kuwaondoa mafisadi wote kuliteka shirika la TANESCO ingawa alikuwa anatumia nguvu ila kiasi alifanikiwa ingawa watu Kama Tundu Lissu walimshauri kwamba atengeneze Sheria zitakazodumu muda wote kwenye rasilimali za Nchi.

Kwa kujua atatawala milele aligoma na kujisemea atawashugulikia apendavyo na kweli aliwashughulikia .

Sasa hayupo yamerudi ndani ya shirika labda angemsikiliza Tundu Lissu juu ya kufuata mfumo wa Bolivia leo tungekuwa salama.

Walianza kuwatumia watu wanaotumbuliwa kuongea bungeni, Mnakumbuka kauli ya Nape kwamba serikali awaachie sector binafsi kuwekeza kwenye umeme? Jamaa alitaka Rufiji ijengwe na sector binafsi na wawauzie umeme tanesco.

Yaani turudie Yale Yale ya Symbion, Dowans, Richmond na IPTL!!

Leo January na Zito wakitumiwa na magege ya wezi na mafisadi wanataka kuuza hisa za tanesco shirika la umma ili umeme wa Nchi ulioshika usalama wa taifa uwe chini ya mafisadi ?

Waipangie Tanesco Bei ya umeme Kama wanavyotaka?

Vyanzo vyote vya umeme vilivyojengwa kuanzia utawala wa nyerere Leo viwe chini ya majamaa tu wengi wao Wala hata hawaishi nchini!!

Yaani hatujifunzi tu kutokana na makosa, sasahivi umeme umeanza kukatika katika hovyo tu na biashara za vijana mnajua zinategemea umeme!

Kuna maeneo unaamhiwa umeme unakatika mara 5 kwa siku Sasa najiuliza Yale majamaa yakiingia Tena tunapona ? Wakati yanaingia na mikakati ya kuagiza makotena ya Generator?

Vijana waliojiajiri na masaloon waliomaliza vyuo wanaishije!! Tuiombee TANESCO na Nchi.
 
95B606AA-972B-4A41-9181-D660E7DA26EE.jpeg
 
Kuna combination chachu sana kwenye hii wizara, kuanzia waziri mwenyewe, bodi aliyoiunda, Zitto, na uhusiano wao na mwenye mamlaka ya nchi, historia zao huko tulipotoka hazileti matumaini kabisa kwenye suala la kumkomboa mtanzania wa hali ya chini, tupo kwenye circle ya wapigaji tunaishi kwa matumaini tu.
 
On the other side of the coin private sector imeonyesha efficiency ya hali ya juu. Jiulize tungekuwaje kama TTCL ingeendelea na ile monopoly. By mwaka 1993 kabla Tigo hawaja connect mteja wa kwanza, TTTCL ilikuwa na landline subscrbers kama 105,000 tu.

Leo hii hawa mobile operators wana connect zaidi ya Watanzania 26 Milioni. Ngoja tuwape benefit of doubts
 
Kuna combination chachu sana kwenye hii wizara, kuanzia waziri mwenyewe, bodi aliyoiunda, Zitto, na uhusiano wao na mwenye mamlaka ya nchi, historia zao huko tulipotoka hazileti matumaini kabisa kwenye suala la kumkomboa mtanzania wa hali ya chini, tupo kwenye circle ya wapigaji tunaishi kwa matumaini tu.
Shida yako wewe hasa ni nini?
 
Sikuwahi kumwamini makamba katika nafasi kubwa

Ni mtu anayeweza kutumika na wengine na hawezi kujisimamia mwenyewe.

Nape enzi ya kikwete alitaka kuonyesha anaweza badae akapewa ukatibu mwenezi nae akaanza kupoteza dira.

Zito ni.mti wa diri na nikiunganishi kwa watawala anaowaweza kuwatumia na kisha yakiharibika hujifanya yeye hayumo.

Makamba aache tanesco wajiendeshe kama shirika huru.

Tuliyaona kwenye treni walivyo ichakaza na kufa baadhi ya njia.

Kwenye umeme walitupandishia bei, eti watu wanachukua ubia wa kuuza umeme bila kuzalisha, tulipata shida bei zikapanza na umeme ulikatika hata kwa nusu week leo tena wanarudi?

Makamba na zito acheni utani.

Hao wawekezaji kama wanataka wapeni maeneo wajenge vyanzo vyao kisha washindane au wauzie tanesco.
 
Kila kitu mnawaza hasi tuu sasa ni vyema mbakie hivyo hivyo na akili zenu hasa,tuwasaidiaje sasa? Acheni tufanye Kazi.
Historia ndiyo inayotufanye tuwaze, kama wangekuwa na good records tusingewaza haya...
 
Awamu ya sita ni janga kubwa sana. Halafu yule mpuuzi tumbo tumbo wa bao la mkono anataka Hangaya atawale hadi 2035.
 
Ufisadi haujawai kuisha TANESCO hata awamu ya mwendazake ulikuwepo tena wa kutisha...kila awamu inakuja na MAFISADI wake ila kinachofanyika ni kuwabrain wash WADANGANYIKA kwamba tulikuwa tunaibiwa sana.
Basi ufisadi wa Tanesco kipindi cha Magu ulikuwa wa kijanja sana maana ela walipiga na bado mishe mishe za kutumia umeme mitaani ziliendelea,lakini huu ufisadi wa kina january wa umeme kukatika katika hovyo aisee ni wa kishamba mno alafu sisi tunawaona maboya tu kwa sasa maana huku mtaani kila mtu sasa hivi kajanjaruka kifupi utawala wa Magu miaka 6 umewafungua watu wengi sana.

Ndio maana hata maza kuwa Rais na anashindwa kupita huko vijijini ni mashauzi yake binafsi ila sio kwamba Urais unamzuia yani sawa mtaani mna maza flani kafanikiwa kimaisha ila kutembelea majirani hapendi sio kama yuko busy ila hana hiyo hulka ila siku akipata jambo full kujiliza liza kwa majirani.
 
Ni vizuri kushauri kama hivi, lakini ni vyema kuwa na future plan ya kuja kuyaondoa haya hata kama wewe ni raia wa kawaida, huu ndio uzalendo.
Raia wa kawaida io nafasi napata wap na Lin? Ni ndoto
 
Back
Top Bottom