TANESCO inarudi mikononi mwa mafisadi?

Huku Jpili hakukuwa na umeme na Leo tena hakuna umeme.
Hi wizara haihitaji waziri muuza sura inahitaji mtu wa kazi.
Hizo tozo badala ya kubooresha mnaharibu?
Tumerudi enzi za Kikwete.
Kweli hata huku nilipo hakuna umeme,yaani waziri yupo bize kupanga watu wa kumsifia Twitter
 
I hope, naamini 100%, Usalama wa Taifa utatusaidia na majizi haya. Zitto, January, i never ever trusted them. Zitto kama Speaker ya January kwa sasa. Ni kuwa makini sana na hawa watu, hii idea ya kubinafsisha Tanesco inatoka wapi? Hii ni hatari kuu katika nchi yetu, hatari ya juu kabisa kabisa. Mama Samia naamini atakaa macho sana kuliko kawaida kuhusu hawa watu. Mungu wetu tusaidie, kila siku tunakuita Munguuuu, Munguuuu wetuuuu, Munguuuu wetuuu, tusaidie tusaidie. Mpe Mama Samia macho makali kabisa ya kuona mbaliiii na wakati wote


Mungu wa Abraham, Jacob and Isaac tusaidie, tusaidie
 
Sukuma Gang ndembendembe,kifo Cha Mende,mlalo,chaaaaaaaaaaaaaaaaaaali.

Kateni umeme mpendavyooooooo.
 
Private sector ilifeli kwenye ATCL Ikafeli kwenye TRC,lakini wacha tuone
Hata kwenye TANESCO walifeli umeisahau NETGROUP SOLUTION kuwa waliwahi kubinafishiwa TANESCO na Mkapa? Uakawashinda wakairudisha Kama ATC na TRC.
Kwa ufupi walisha jaribu wakashindwa.
 
Sukuma Gang ndembendembe,kifo Cha Mende,mlalo,chaaaaaaaaaaaaaaaaaaali.

Kateni umeme mpendavyooooooo.
Wasukuma wamefanya Nini hapa? Siku hizi kutetea maslahi ya nchi unaitwa sukuma gang sawa mtuite tu Ila kwenye ufisadi tutadili na nyie Msoga gang
 
Çcm ni ukoo wa panya, hakuna asiyekuwa mpigaji kuanzia ikulu mpaka shinani
 
Genge lenye nguvu kubwa kuliko serikali? Nguvu ya genge hili inatokana na nini? Viongozi wa genge hili ni akina nani?
Genge hili linafukarisha na kuyumbisha nchi kivipi?
 

Kwani lini Tanesco aliwahi kuwa huru na ufisadi?
 
Tutajie ufisadi uliofanyika kipindi Cha Magufuli,sio kusema tu toa ushahidi.

Kwani kipindi paymaster mtoto wa dada sicho kile kile chenye 1.5tr/- za Assad, viwanja vya chato, madege yasiyonunuliwa kwa utaratibu, waziri wa nishati mtoto wa nyumbani nk?

Hadi hapo usidhani nimesahau ya madaraja ya kigongo busisi na wale maofisa Tanroads wa milele waliokuwa hawastaafu.

Utakuwa umetenda haki pia usiposahau kuna na madudu mengine yasiyo kifani huku:



Lini tumewahi kuwa nafuu sie?
 
Ufisadi haujawai kuisha TANESCO hata awamu ya mwendazake ulikuwepo tena wa kutisha. Kila awamu inakuja na MAFISADI wake ila kinachofanyika ni kuwabrain wash WADANGANYIKA kwamba tulikuwa tunaibiwa sana.
Wakati mwingine acha ujinga wako
 
Unaulizwa hili unajibu lile!!!!!!! Wewe unajua 1.5 T wewe, kazi kubwabwaja tu
 
Umeandika pasipo kuweka ushahidi wowote wa maana (tangible proof) nadhani hii ni kusoma na kuiacha kama ilivyo. Imekaa kizandiki na kinafiki, ni siasa zile zile za kushambulia mtu badala ya kuja na hoja zenye kueleweka.
 
Ameanza kwenye bodi kuweka maharage, majaa, gachuma na yale majina walituumiza huko nyuma ili kuja kumalizia kuhamisha mali za umma kua zao binafsi.
 
Ndio tena mara millioni ili kulipiza kisasi cha kupoteza miaka sita iliyopita kutokana na kuhangaika na kesi za uhujumu uchumi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…