godson njamakuya
Senior Member
- Mar 6, 2021
- 170
- 196
Ni siku ya tatu sasa umeme unakatika bila sisi wateja kujulishwa kama kuna matengenezo yoyote yanaendelea.Nashauri kama kuna marekebisho yoyote yanayofanyika ni vyema tukataarifiwa kwenye vyombo kwamba eneo flani litakosa umeme kwa muda flani ili kupisha maboresho katika miundombinu ya umeme.
Hii itatufanya kuchukua tahadhari kwa kuzima main switch ili kuepuka madhara yanayoweza kutokea pindi umeme unaporudi. Lakini Shirika husika limekaa kimya, kipindi cha nyuma kulikuwa na yule dada jina limenitoka yeye alikuwa Afisa Uhusiano TANESCO kukiwa na marekebisho flani eneo flani lazima atangaze kwenye TV sasa hivi kitu, mnashtukia tu mko gizani haijulikani umeme utarudi muda gani,hii ni hatari kwa usalama wa vifaa vyetu vinavyotumia umeme.