TANESCO Kigoma ifumuliwe

TANESCO Kigoma ifumuliwe

Prakatatumba abaabaabaa

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2022
Posts
1,842
Reaction score
6,087
Inakuwaje zinapita siku 3 hakuna umeme? Tena hapa Kigoma Manispaa, bora ingekua Kibondo huko.

Unalala unaamka siku moja, mbili tatu hakuna hata huo umeme, kesho tunaamka siku ya nne bila umeme lakini maeneo mengine upo.

Hawatoi taarifa kwanini wamekata, ukienda ofsini kwao hupewi majibu ya uhakika, na bado wamekaa ofisini tu bila wasiwasi.

Umeme ni huduma ya lazima huwezi kuzima umeme siku 4 bila kutoa taarifa yoyote.
 
Back
Top Bottom