pharao
JF-Expert Member
- Jan 17, 2017
- 397
- 690
Mimi ni mkazi wa Mbagala, Mbande, na kwa kweli hali ya umeme katika maeneo haya ni ya kutisha. Maeneo yote yanayozunguka Chamanzi, Mbande, na Kisewe yanakumbwa na matatizo makubwa yanayohusiana na huduma ya umeme kutoka Tanesco.
Katika kipindi cha wiki mbili zilizopita, taa sita ndani ya nyumba ninayoishi zimeungua pamoja na kompyuta mbili (Desktop) kutokana na kukatika kwa umeme na kurudishwa kiholela. Kila jioni, kuanzia saa moja hadi saa sita au saba usiku, umeme unakatika na kurudi mara kwa mara, kiasi kwamba ndani ya dakika moja umeme unaweza kukatika na kurudi hata mara 10 au 20! Hii ina maana kuwa ndani ya masaa sita au saba, umeme unaweza kukatika na kurudi zaidi ya mara 5000! Hali hii ni hatari sana, hasa kama uko mbali na nyumba yako, ambapo unapofika nyumbani unaweza kukuta vifaa vingi vimeharibika.
Katika wiki moja, tunapata umeme mchana kwa siku mbili tu, huku siku zingine zote Wakisema kwamba wanafanya matengenezo. Lakini wanapourudisha jioni, umeme unakuwa unstable na unaanza kukatika na kurudi mara kwa mara, hali inayosababisha vifaa vyetu kuharibika.
Ni ukweli kuwa watu wengine hatupendi kulalamika hovyo, lakini hali hii si ya kawaida na inachosha na kuchukiza Mno. Kama kuna marekebisho ya mitambo yanayohitajika, tunaomba tuambiwe mapema. Hata mkisema mkate umeme kwa miezi sita mfululizo ili mfanye marekebisho hayo, tutakubaliana na hali hiyo kwa kuwa ni bora kuliko kupokea umeme ambao hauna uhakika na unasababisha hasara.
Kupata umeme katika maeneo haya imekuwa kama kupokea zawadi, kwani kila siku kuna matengenezo, na wakirudisha umeme, ni hali ya shot!
Waziri wa Nishati tunaomba Ufuatilie Suala Hili ijulikane shida ni nini, kama Bili tunalipa kwa wakati! Mbagala ni moja ya maeneo yenye population Kubwa zaidi Hapa DSM.
TANESCO