TANESCO mmekubali kutumika kudai kodi ya majengo (TRA) kinyume na mkataba wenu? Kwa hili tutawashitaki; Serikali hamna huruma

Unaweza kutolea maelezo haya maneno "applicable on electricity supply " kwenye kipengele namba 10 ulichokinukuu?
Kwahiyo shida ni kiingereza au ni ‘ufahamu’…, maana inaeleza tu kwamba inapotokea mabadiliko ya sheria ndogo ndogo ihusuyo huduma ya umeme inabidi uwe tayari kukubaliana na manadiliko hayo
 
Yote yangekuwa sawa kama kinachokusanywa angalau kingetumika vizuri maendeleo yakaonekana. Mbona mtaani hali ngumu hivi? 😳

Shida ya nchi hii siyo ukusanyaji wa kodi Bali ni matumizi mabaya ya kodi .... Ulishawahi kujiuliza kwanini magari ya serikali huwa hayazimwi kwenye mikutano hata kama ni SAA mbili yanaunguruma tu,
Sasa unataka vigogo wakitoka huko mkutanoni wakute magari yamepata moto waungue? Inachukua dakika kadhaa mpaka kiyoyozi kiweze kupoza hewa ndani ya gari! 😬😬😬
 
Kwahiyo shida ni kiingereza au ni ‘ufahamu’…, maana inaeleza tu kwamba inapotokea mabadiliko ya sheria ndogo ndogo ihusuyo huduma ya umeme inabidi uwe tayari kukubaliana na manadiliko hayo
Suala sio lugha, hicho kifungu kinaongelea mambo yanayohusu usambazaji wa huduma ya umeme.

Mleta hoja kando ya mambo mengine analalamika TANESCO kufanya kazi ya TRA.

Sawasawa na wewe uende hospital kutibiwa kwenye malipo uambiwe lipia na Kodi ya ujenzi wa barabara.
 
Bora umemwelewesha! Maana hajui kwamba umeme huwezi kupata kama hela yao ya kodi ya jengo usipoweka! Sasa madeni yote yakipishwa kwenye luku haoni kwamba wanatunyima huduma ya msingi ambayo ni umeme na maji
 
Sasa unataka vigogo wakitoka huko mkutanoni wakute magari yamepata moto waungue? Inachukua dakika kadhaa mpaka kiyoyozi kiweze kupoza hewa ndani ya gari! 😬😬😬

Nimesikitishwa na kitendo Cha kiongozi wa bunge kutokatwa tozo hata kidogo kwenye muamala wa 20k. Hata makato ya kampuni ya simu hakuna kabisa.
 
Nimesikitishwa na kitendo Cha kiongozi wa bunge kutokatwa tozo hata kidogo kwenye muamala wa 20k. Hata makato ya kampuni ya simu hakuna kabisa.
Ndugu yangu. Kuna watu wanaishi kama malaika katika nchi hii...........

Mwanasheria wangu angekuwepo ningeendelea zaidi ila kwa sasa ngoja niishie hapo!

Natumaini mko salama huko Kizimkazi!
 
Kwakuwa taasisi zote 2 zipo chini ya serikali, basi serikali ina uhuru wa kuvi-synchronise ili visaidiane in-tandum katika kutekeleza majukumu na kufikia malengo ya serikali..
 
Kwakuwa taasisi zote 2 zipo chini ya serikali, basi serikali ina uhuru wa kuvi-synchronise ili visaidiane in-tandum katika kutekeleza majukumu na kufikia malengo ya serikali..

Narudia Tena, umeelewa maana ya hicho kipengele ulichokitaja?

Kwahiyo TRA wanaweza kutolewa Kisha jukumu la kukusanya mapato/ Kodi likagawanywa Kwa taasisi zingine?
 
Narudia Tena, umeelewa maana ya hicho kipengele ulichokitaja?

Kwahiyo TRA wanaweza kutolewa Kisha jukumu la kukusanya mapato/ Kodi likagawanywa Kwa taasisi zingine?
Ndio, na Nimekueleza nilichoelewa. TRA anapewa nguvu ya kutumia taasisi zingine kama Bank, Tanesco, Makampuni binafsi (VAT) nk. Na nguvu hii amepewa kisheria, hivyo jibu ni ndio, taasisi zingine zinaweza kukusanya kodi na kuiwasilisha TRA.
 
Ntapoteza muda mwingi sana. You are right sir
 
Wanao lipa kodi Tanzania niwachache hatuna mfumo mzuri wa kodi kumbe jamii inatakiwa ibuni mfumo mzuri,(rafiki), wa kodi yaani wewe na mimi, mfano mimi ninaanga kwenye mfumo wa kukuza ama kuimalisha ujasiriamali, entrepreneurial ecosystem
 
Hii nchi ijinga mwingi sana! Hii kodi sijawah kuilewa, tunaibiwa kindez sana yan
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…