Preciousvision
JF-Expert Member
- May 14, 2026
- 888
- 1,205
Ni ukweli ulio wazi sasa hivi wakuu wa taasisi za serikali ikiwemo TANESCO wanamdharau huyu Rais ndiyo maana wanamhujumu, wanamchonganisha kwa wananchi aonekane ameshindwa kuongoza.
TANESCO mlitukatia umeme tangia asubuhi saa 3, mmerudisha sa 12 jioni, ajabu mmeukata tena, ni nini mmeshindwa kurekebisha tangia asubuhi? Km ni hivyo mna haja gani ya kuendelea kuwa ofisini? Tunaomba serikali kupitia aidha mkurugenzi mkuu wa TANESCO au waziri wa nishati aondoe hawa viongozi wa TANESCO mkoa wa Arusha na wilaya ya Arumeru.
Umeme ni maisha ya watu, wao wana mishahara na marupurupu wanacheza na maisha yetu hawajali. Uzembe huu wa viongozi unafanyika hasa kipindi hiki cha Samia km Rais, kwanza hawakutoa hata taarifa kabla kuwa kuna katizo la umeme. Nchi sahivi ni km haina uongozi, ukienda LATRA wananchi wananyanyaswa na wamiliki wa vyombo vya usafiri, wamejiongezea nauli wanavyotaka hakuna wa kuwadhibiti, nchi imeoza tukimbilie wapi?