KERO TANESCO mnakata umeme kuanzia Kimara mpaka Mbezi kwa zaidi ya masaa 12 kila siku bila ya kutoa taarifa yoyote ile ya kueleweka

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Mkono Mmoja

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2019
Posts
3,359
Reaction score
6,568
Kwa takribani wiki mbili wakazi wa Kimara mpaka mbezi wanaishi pasi na umeme kila siku kwa zaidi ya masaa 12 bila ya taarifa yotote.

TANESCO kila inapofika saa 4 asubuhi wanakata umeme na hurudi saa 5 Usiku. Kama kuna mgao waelezeni wananchi wafahamu kuliko huu ujinga mnaoufanya.

Taarifa iwafikie TANESCO na tunataka majibu ya haraka juu ya hili jambo.

Pia soma: KERO - Tanesco Mkoa wa Kinondoni Kusini- Kimara/Kibamba
 
Roving Journalist wasialiana na hawa jamaa watueleze huduma za umeme zinarejea lini.

Wafanyabiashara wa samaki na nyama wanaozesha mali zao daily kutokana na kukatiwa umeme bila ya taarifa
 
Nchi hii ishawashinda, mwaka wa 60+ toka uhuru mpaka leo, umeme tabu, maji changamoto, afya tabu, elimu ya hovyo, barabara changamoto, ajira ndio tatizo linakuja kwa kasi, gharama za maisha zinapanda kila uchwao, pesa yetu inashuka thamani.

Hawana cha maana wanachofanya zaidi ya porojo, mara deni la taifa stahamilivu, mara uchumi wa kati, tumepata gesi umaskini bai bai, sijui madini gani, wao wanajiwahi mapema, gesi, bandari, madini, mbuga za wanyama, hazina manufaa na mtanzania zinawafaidisha wao tu.

Ikishindikana arudi tu mkoloni mzungu tujue moja.
 
aisee ni hatari fikiria wafanyabiashara wanakaa zaidi ya masaa 12 bila ya umeme na hakuna taarifa yoyote wanayoitoa. Wanakata wapojiskia tu na wanaurudisha wanapotaka wao.
 
Tanzania kweli imeendelea watu wa kimara na mbezi ya uswahilini siku hizi wanatumia umeme asee

Hongera Mama Samia
 
Kuna ndugu yangu kaniambia washakata tena.

CCM nchi imewashinda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…