Tanesco Morogoro kila mara ni kuomba radhi tu?

Tanesco Morogoro kila mara ni kuomba radhi tu?

KITEKSORO

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2012
Posts
346
Reaction score
425
SHIKRIKA LA UMEME TANZANIA TANESCO MKOA WA MOROGORO.

TAARIFA YA KUOMBA RADHI KUKOSEKANA KWA HUDUMA YA UMEME BAADHI YA MAENEO YA MKOA WA MOROGORO.

Shirika la umeme Tanesco linaomba radhi wateja wetu wanaotumia laini ya Tungia,Mzinga,Kilosa,Mikese kwa kukosa huduma ya Umeme usiku wa kuamkia leo kutokana na changamoto zilizojitokza:

Siku :Jumanne.
Tarehe 31/08/2021.

Sababu :hitilafu iliyosababisha kosekana kwa huduma ya Umeme Usiku wa kuamkia leo kutokana na changamoto iliyojitokeza wakati wa kuunga trasfoma kubwa la Msamvu.

Maeneo yanayokosa umeme ni Tungi,Mikese,Mzinga,Mkambarani,Mgeta,Mlali,Tandali,Maguruwe,Area 5&6,Kola A&B,Wilaya yote ya Kilosa yote Kilosa ,Wilaya ya Morogoro vijijini.

Juhudi zilizofanyika team imeanza kurejesha huduma ya iii meme baadhi ya Maeneo mengi ya Mji kupitia transfoma hilo na sasa Tunaendelea na kuunga laini zilizokosa umeme usiku wa kuamkia leo .

Tunaomba radhi sana kwa usumbufbcu utakao kuwasa umejitokeza.

Tahadhari usishike wala kukanyaga nyaya zilizolala chini yoa taarifa Emergency Tanesco Morogoro kipitia namba 06770630010684>89272 tutakufikia .


imetolewa na :
Ofisi ya Uhusiano huduma kwa wateja Tanesco Morogoro.

31/08/2021.
 
Hawa tanesco wa moro wamekua pasua kichwa. Wanakata umeme wanavyojiskia tofauti na kipindi cha jiwe.
 
Hawa Tanesco ng'ombe kabisa.. unakataje umeme kwa masaa 48? Sijawahi kuona shirika la kibabaishaji kama Tanesco yaani. Hawana tofauti na policcm yaani

Na ili umaskini wa nchi hii upungue, ni vema hili shirika liuzwe tu.. hamna namna. Maana hata wasipouza umeme bado mishahara wanapata..

Tanesco! Tanesco! Tanesco! Nimewaita mara ngapi? Hayaa..
Utalalamika sana kwa sababu hata mchawi wako humjui ni nani.Haya ya Tanesco ni matokeo ya mchawi fulani ambae hata humjui!

Unatakiwa uhangaike na mchawi na wala siyo kuhangaika na Tanesco ambao ni matokeo.Unahitaji PhD ili kujua vitu vidogo kama hivi?!
 
Leo ni wiki ya tatu umeme haukai kwa masaa matatu huku nilipo, mpaka mida huu ni masaa 24 tangu ukatike, na ni wiki ya tatu hatujawai kukaa na umeme zaidi ya masaa ma4! Hawajui, laiti wangejua jinsi wanavyoua mitaji ya watu wasingekaa nasi mtaani, yaani baada ya pomoka watu wa hovyo wanaofuata ni hao wapuuzi
 
Leo ni wiki ya tatu umeme haukai kwa masaa matatu huku nilipo, mpaka mida huu ni masaa 24 tangu ukatike, na ni wiki ya tatu hatujawai kukaa na umeme zaidi ya masaa ma4! Hawajui, laiti wangejua jinsi wanavyoua mitaji ya watu wasingekaa nasi mtaani, yaani baada ya pomoka watu wa hovyo wanaofuata ni hao wapuuzi
ndugu mteja,
tunaomba kupata taarifa zako kwa ajili ya ufuatiliaji zaidi ikiwemo;
jina kamili
namba ya simu
eneo lako
wilaya
mkoa
namba ya mita
 
Back
Top Bottom