TANESCO Morogoro kila siku umeme kukatika, kwanini?

KITEKSORO

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2012
Posts
346
Reaction score
425
Kama tujuavyo, bila nishati ya umeme shughuli nyingi zinakwama. Umeme kukatika siku nzima ni hasara kubwa sana kwa Taifa.

Leo Morogoro hakuna umeme tangu asubuhi hadi sasa. Namna hii uchumi wa mkoa na wa watu binafsi unaathirika sana.

Inawezekana umeme haukatwi makusudi ila kama kuna hitilafu zifanyiwe kazi haraka kama dharura ili umeme urejee.

Inakera sana kwa kweli. Najaribu kujiuliza wahusika wa Tanesco mida hii wanashughulikia hii hali au nao wamekaa tu wanakunywa serengeti lite za moto?
 
Kila mahali kuna taarifa za kukatika kwa umeme, nadhani mgao sasa ni rasmi wahusika wamegoma kulisema hili
 
Mheshimiwa amesema siku hizi wanafanya "scheduled maintainances" ambazo hazikufanyika enzi za mwendazake kwa watu kuhofia kutumbuliwa. Kwahiyo kaa kwa kutulia. 😀
 
Tumia lugha ya ukali acha kuwachekea hawa mbwa!!!
Morogoro mkoa wenye huduma duni kila Idara Morogoro..
Sijui watu tumerogwa, huduma Maji duni sana, Umeme nao hivyo hivyo...ah
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…