KERO TANESCO mtaunguza nyumba Kigamboni mnakata umeme mara 8 kwa siku

KERO TANESCO mtaunguza nyumba Kigamboni mnakata umeme mara 8 kwa siku

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Revolution

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2008
Posts
960
Reaction score
927
Pamoja na kero ya kukatika kwa umeme inayoendelea katika Jiji la Dar es Salaam, Tanesco wanaweza kukata umeme na kuurejesha mara 8 au 10 kwa siku katika Manispaa ya Kigamboni.

Hii ni hatari sana! Kwanini msiukate tu kisha kama kuna hitilafu ama mgao mkaurejesha baada ya kutatua tatizo? Mtakuja kuunguza nyumba au vitu na kuwapa wananchi hasara.

Hivi hali ya kukatika kwa umeme imekuwa worse baada ya kuanza kazi kwa bwawa la kufua umeme la JK Nyerere!!??

Mbona kipindi cha nyuma hapo kwenye miaka mitatu au minne iliyopita hakukuwa na shida ya umeme licha ya kutokuwa na Bwawa kwa wakati huo!!?
 
Back
Top Bottom