Tanesco na baadhi ya viongozi wenye dhamana Serikalini wanapata faida gani kukata umeme?

Cashman

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2018
Posts
3,017
Reaction score
5,294
Nikishangaa sana, suala la umeme kukatika hovyo hovyo tena siku nzima,kwa hapa shinyanga mjini,limekithiri sana tangu waziri wa nishati aondolewe na kuwekwa Makamba.

Hata wakati wa JK haikuwahi kuwa hivi.Kwa sasa hali imezidi sana kwani hata siku kama ya leo ambapo wananchi wengi wanafuatilia matangazo ya maadhimisho ya sherehe za mapinduzi Zanzibar,Umeme umekatika.

Ninasikitika sana kwa hili kwani ninaona huenda kuna fursa ya upigaji uliohalalishwa kupitia kitu wanachoita service.

Ninatamani kujua huko kwenye service huwa wanabadili nguzo tu au kuna vipuri huwekwa?Kwa nini kwa miaka mitano hakukuwa na huu mchezo wa kukata umeme kila siku kwa mgao?

Kama kuna vipuri vinawekwa ni nani anayeviagiza nje?Au kuna watu wana stock ya majenereta wanataka kuuza?

Je, kama ni suala la mabwawa ya kuendesha mitambo ya kuzalisha umeme,Maji yamepungua,vipi gas yetu ambayo mara tu ilipianza kuzalishwa,gharama ya service charge ikaondolewa?

Kwa suala hili,nimeanza kukumbuka kiburi cha mameneja wa Tanesco miaka ya nyumba.Ufalme wao umerejea.
 
Itakuwa wameelekeza nguvu kazi kwenye ule mradi mkubwa wa JNHPP kule Mto Rufiji. Tuweni na subira jamani. Hamwoni hali inaelekea kuwa shwari?

Tunaahidi kushughulikia tatizo husika mara moja. Isitoshe mitambo na vipuri vipya vilikuwa vinafanyiwa upembuzi yakinifu na usanifu, mchakato ukikamilika, soon vitaingizwa na kuanza kutumika. Umeme nchini, tatizo husika litakuwa historia!

Great News ni kwamba tunashirikiana na wanasayansi wakubwa wa China, Ulaya na Marekani ili kufinyanga mionzi sawa na ile ya jua, itayokuwa na uwezo wa kuzalisha umeme wa kutosha kutumiwa na kila raia wa Tanzania aliyeko sasa na ajaye, kwa zaidi ya miaka 500 ijayo!

Kwani zile trilioni 14,000 (dola bilioni 6,000) za akiba yetu ya nchi hamkuzisikia?
 
Kama ninyi wenyewe hamwezi kujitetea, nani atadiriki kuja kuwateteeni? Fanyeni ^key-two!^ Hata japo kwa kujipaka matope tupu mwili mzima na kuvalia mifuko ya rambo ili kufanya maandamano ya amani kuanzia Mjini Kati hadi Magogoni!

Let your voice be heard!

Arusha huku kwetu ni siku ya tatu leo wanakata asubuhi mpaka usiku, hawana huruma na hatuna mtu wa kututetea, masikini tunazidi kudidimia.
 
Faida ni Ili wafanyabiashara wa majenerata na solar wauze.
Umeme ukiwa wa uhakika zinadoda madukani
 
Nikishangaa sana,suala la umeme kukatika hovyo hovyo tena siku nzima,kwa hapa shinyanga mjini,limekithiri sana tangu waziri wa nishati aondolewe na kuwekwa Makamba.

Hata wakati wa JK haikuwahi kuwa hivi.Kwa sasa hali imezidi sana kwani hata siku kama ya leo ambapo wananchi wengi wanafuatilia matangazo ya maadhimisho ya sherehe za mapinduzi Zanzibar,Umeme umekatika.

Ninasikitika sana kwa hili kwani ninaona huenda kuna fursa ya upigaji uliohalalishwa kupitia kitu wanachoita service.

Ninatamani kujua huko kwenye service huwa wanabadili nguzo tu au kuna vipuri huwekwa?Kwa nini kwa miaka mitano hakukuwa na huu mchezo wa kukata umeme kila siku kwa mgao?

Kama kuna vipuri vinawekwa ni nani anayeviagiza nje?Au kuna watu wana stock ya majenereta wanataka kuuza?

Je kama ni suala la mabwawa ya kuendesha mitambo ya kuzalisha umeme,Maji yamepungua,vipi gas yetu ambayo mara tu ilipianza kuzalishwa,gharama ya service charge ikaondolewa?

Kwa suala hili,nimeanza kukumbuka kiburi cha mameneja wa Tanesco miaka ya nyumba.Ufalme wao umerejea.
Kipi cha JK inaonekana ulikua bado ujakua
 
Ni afadhali kidogo kwani Prof Muhongo aliwadhibiti kiasi fulani Tanesco.Na ukweli hali ilianza kuwa nzuri kuanzia kwa Muhonngo.
Iliendelea kuwa stable hadi pale tu alipoingia January.Asee hali ni tete sana.
Kipi cha JK inaonekana ulikua bado ujakua
 
Itakuwa wameelekeza nguvu kazi kwenye ule mradi mkubwa wa JNHPP kule Mto Rufiji. Tuweni na subira jamani. Hamwoni hali inaelekea kuwa shwari?

Tunaahidi kushughulikia tatizo husika mara moja. Isitoshe mitambo na vipuri vipya vilikuwa vinafanyiwa upembuzi yakinifu na usanifu, mchakato ukikamilika, soon vitaingizwa na kuanza kutumika. Umeme nchini, tatizo husika litakuwa historia!

Great News ni kwamba tunashirikiana na wanasayansi wakubwa wa China, Ulaya na Marekani ili kufinyanga mionzi sawa na ile ya jua, itayokuwa na uwezo wa kuzalisha umeme wa kutosha kutumiwa na kila raia wa Tanzania aliyeko sasa na ajaye, kwa zaidi ya miaka 500 ijayo!

Kwani zile trilioni 14,000 (dola bilioni 6,000) za akiba yetu ya nchi hamkuzisikia?
Mkuu haya maneno ni matamu kwa kuyasikia lakini hatua ya utekelezaji ndo huwa zinatuacha hoi hadi tunaanza jiuliza, ni haya haya yalitufurahisha mwanzo? Au kuna vitu halisia mwanzoni hatukuambiwa. Refer gas ya Ntwara na mengine mengi
 
Nunua Generator,Kuna mtu kaingiza hayauziki.....Hela ya generator moja kuwapa maboss wakata umeme wa TANESCO Ili auze 10 ni jambo rahisi sana
 
Back
Top Bottom