Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Tatizo kubwa la wanasiasa wa Tanzania ni kufikiri kwamba Watanzania wote hawana uwezo wa kufikiri, na hivyo huridhika kutoa maelezo mepesi ya kisiasa hata kwenye mambo ya kisayansi.
Mfano ni hili la kupeleka umeme mikoa ya Kaskazini, ambapo Tanesco wanasema gharama za transmission ni kubwa - wao wanaziita hasara, na ni afadhali kununua umeme kutola Ethiopia!
Sasa mtu mwenye akili atajiuliza, kwani huo umeme wa kununua kutoka Ethiopia kuja Tanzania unapitishwa kwenye medium gani ambayo haina transmission losses mnazosema huku kwetu ni gharama sana? Na kumbuka kwamba source ya umeme toka Ethiopia iko mbali zaidi ya source yeyote ya umeme ndani ya Tanzania kwenda mikoa ya kaskazini. Kama transmission losses zinaendana na umbali, basi gharama ya transmission losses ya kuleta umeme toka Ethiopia yapaswa kuwa kubwa zaidi (angalia ramani hapo chini)
Kumbuka kwamba, ili Ethiopia watuuzie umeme wao, lazima wana factor-in transmission losses zao za kutoa umeme Ethiopia kuja Tanzania. Sasa ikiwa sisi Tanzania kulipia transmission losses za Ethiopia ni nafuu kuliko kubeba transmission losses za line zetu wenyewe, ni kitu gani ambacho Ethiopia wanafanya kwenye hiyo transmission line yao kuja Tanzania ambacho sisi kimetushinda kufanya? Tilia maanani kwamba umeme wa Ethiopia na Tanzania wote unatokana na maji, hivyo gharama za uzalishaji ni karibu sawa.
Na mikataba ya kununua umeme ni ya muda mrefu siku zote. Kama issue ni transmission lines, kwa nini tujifunge kwenye mkataba wa muda mrefu (lock in effect) badala ya kuwa na mkakati wa kuboresha transmission lines kwa faida za muda mrefu?
Najua Tanesco mmetoa tamko kuuunga mkono kauli ya Raisi Samia mkijua wazi maelezo yenu hayajitoshelezi. Mmejitoa akili ili msijbu kuendana na kauli za wanasiasa, na si mara ya kwanza mnafanya hivi.
Acheni kuendesha hii nchi kinyume cha maumbile. Serikali iseme ukweli kuhusu lililo nyuma ya pazia kutaka kununua umeme toka Ethiopia. Acheni maelezo ya kisiasa kwenye mambo ya kisayansi.