TANESCO na Msigwa mtuambie kwanini umeme wa Tanzania kwenda Kaskazini una transmission losses kubwa kuliko wa Ethiopia kuja kwetu, mbali zaidi!

Watakovo kueleza watatumi mfano wa choo kikiwa juu mlimani si rahisi kujaa haraka
Kimsingi,huu mkataba wa kununua umemem unaweza ukawa na lojiki, japo sidhani. Jambo la msingi ni Tanzania na Samia kutoingia kichwa kichwa bila kuwa makini kuona long term implications ni nini,kama wanavyofanya siku zote. Wauweke wazi huo mkataba tuuchambue. Mkataba wa umeme Samia na Mbarawa ndio wanapitisha, unategemea nini hapo, kupigwa tu!
 
Yah. Nenda sima post ya Tibaijuka ... Ameeleza sawa na hivyo usemavyo.
Tibaijuka wamemweleza eti ni kwa ajili ya energy security. Sasa lini tena tumebadilisha objective ya kununua umemem toka Ethiopia kwa nia ya kukwepa transmission losses na kwenda kwenye supply security?

Katika vitu hivi, kila kimoja kina approach yake. Huwezi kubadili lengo moja kuwa jingine kwa mradi uleule. Ukisema ni supply security unaweza kukuta umeme wa Ethiopia ni wa mwisho kwenye list - hasa Egypt anapotishia kuwapiga kwa sababu ya hilo bwawa!
 
Tatizo kubwa la wanasiasa wa Tanzania ni kufikiri kwamba Watanzania wote hawana uwezo wa kufikiri, na hivyo huridhika kutoa maelezo mepesi ya kisiasa hata kwenye mambo ya kisayansi.

Mfano ni hili la kupeleka umeme mikoa ya Kaskazini, ambapo Tanesco wanasema gharama za transmission ni kubwa - wao wanaziita hasara, na ni afadhali kununua umeme kutola Ethiopia!

Sasa mtu mwenye akili atajiuliza, kwani huo umeme wa kununua kutoka Ethiopia kuja Tanzania unapitishwa kwenye medium gani ambayo haina transmission losses mnazosema huku kwetu ni gharama sana? Na kumbuka kwamba source ya umeme toka Ethiopia iko mbali zaidi ya source yeyote ya umeme ndani ya Tanzania kwenda mikoa ya kaskazini. Kama transmission losses zinaendana na umbali, basi gharama ya transmission losses ya kuleta umeme toka Ethiopia yapaswa kuwa kubwa zaidi (angalia ramani hapo chini)

View attachment 3265426

Kumbuka kwamba, ili Ethiopia watuuzie umeme wao, lazima wana factor-in transmission losses zao za kutoa umeme Ethiopia kuja Tanzania. Sasa ikiwa sisi Tanzania kulipia transmission losses za Ethiopia ni nafuu kuliko kubeba transmission losses za line zetu wenyewe, ni kitu gani ambacho Ethiopia wanafanya kwenye hiyo transmission line yao kuja Tanzania ambacho sisi kimetushinda kufanya? Tilia maanani kwamba umeme wa Ethiopia na Tanzania wote unatokana na maji, hivyo gharama za uzalishaji ni karibu sawa.

Na mikataba ya kununua umeme ni ya muda mrefu siku zote. Kama issue ni transmission lines, kwa nini tujifunge kwenye mkataba wa muda mrefu (lock in effect) badala ya kuwa na mkakati wa kuboresha transmission lines kwa faida za muda mrefu?

Najua Tanesco mmetoa tamko kuuunga mkono kauli ya Raisi Samia mkijua wazi maelezo yenu hayajitoshelezi. Mmejitoa akili ili msijbu kuendana na kauli za wanasiasa, na si mara ya kwanza mnafanya hivi.

Acheni kuendesha hii nchi kinyume cha maumbile. Serikali iseme ukweli kuhusu lililo nyuma ya pazia kutaka kununua umeme toka Ethiopia. Acheni maelezo ya kisiasa kwenye mambo ya kisayansi.
Kingine walitakiwa watuambie miundo mbingu ya umeme toka huko Ethiopia kuja kwetu ni wa voltage kiasi gani ? Labda uwe kuanzia 765kV au 1000kV kwenda mbele. Ambao kwa Sasa rate voltage hizo sisi hatuna haja nazo.

Lakini ukienda Arusha tu huko tayari miundo mbinu ya 400kV ipo.

Sasa sijajua wenyewe wanatumia akili gani, wengine ukiwauliza wanadai ni Grid Stability, yaani wanastabilize Grid ?
 
Kuna mtu nimesikia anasema .. umeme wa ethiopia (grid husika ya kuchukua umeme had mikoa yetu ya tz) tiar upo (ipo) karibu TZ ndani ya kenya ...

So Ikiwa grid ya taifa letu inayofika kaskazini ilihitaji kuongezewa nguvu (as matumiz ya ukanda husika ni makubwa na hayafanani na nguv ya grid husika mpaka sasa) bas ni bora tutumie grid ya Ethiopia as inaweza tugharim gharama kubwa zaid ku upgrade ile ya kwetu .. inayoenda kaskazini.....

Kwa maelezo zaid ni kua tungeweza ku uograde. Lakini ukizingatia kua kuna hasara ya kusafirisha umeme pia bas ni bora tu tuikwepe kwa kununua ule wa ethiopia ambapo wao binafsi nda watawajibika na huku kupotea kwa umeme hapo katikati ktk kuusagirisha.

Hoja ya pili ni diversification. ... (Hatupaswi kutegemea chanzo kimoja)
Hawa jamaa maelezo yao hayajitoshelezi, walitakiwa watoe maelezo ya ndani zaidi. Hili suala linahitaji mjadala wa wazi baina ya wataalamu.

Kingine, kwani Grid yetu inayofika Kaskazi ni voltage kiasi gani na hiyo inayotoka Ethiopia ni voltage kiasi ?

Sasa chanzo kimoja, ndio watu Wana hoji, vipi kwa mikoa mingine ?
 
Kingine walitakiwa watuambie miundo mbingu ya umeme toka huko Ethiopia kuja kwetu ni wa voltage kiasi gani ? Labda uwe kuanzia 765kV au 1000kV kwenda mbele. Ambao kwa Sasa rate voltage hizo sisi hatuna haja nazo.

Lakini ukienda Arusha tu huko tayari miundo mbinu ya 400kV ipo.

Sasa sijajua wenyewe wanatumia akili gani, wengine ukiwauliza wanadai ni Grid Stability, yaani wanastabilize Grid ?
Point nzuri. Kama wanasema transmission infrastructure ipo tayari, ni lini tathmini imefanyika kuangalia uwezo wa hiyo grid toka Ethiopia? Je wameangalia reliability yake? Wameangalia scalability yake kwa kuwa haikujengwa with transmission to Tanzania in mind? Wameangalia technological compatibility (HVDC au HVAC) na kama imetumia aluminum au copper conductors kwa hiyo ina losses za chini ukilinganisha na za kwetu? Wameangalia nini itakuwa impact kwenye grid resistance and inductive reactance watakapounganisha na Tanzania? Je itaunganishwa na na grid iliyopo ya upande wa Tanzania, na kama ndio, wameangalia connectivity? Na isipounganishwa na grid ya Tanzania, siku umeme wa Ethiopia ukifeli then hiyo mikoa ya kaskazini itakuwaje?

Ndio maana nikasema, Samia na Msigwa wasichukulie haya mambo kisiasa katika kutafuta kura za kaskazini na kuwaburuza TANESCO
 
Hapa wanatakiwa hii lugha yao ili iweleweke vizuri watumie data za wazi na nina Imani hawawezi kufanya hivyo sababu namba hazidanganyi.
 
Point nzuri. Kama wanasema transmission infrastructure ipo tayari, ni lini tathmini imefanyika kuangalia uwezo wa hiyo grid toka Ethiopia? Je wameangalia reliability yake? Wameangalia scalability yake kwa kuwa haikujengwa with transmission to Tanzania in mind? Wameangalia technological compatibility (HVDC au HVAC) na kama imetumia aluminum au copper conductors kwa hiyo ina losses za chini ukilinganisha na za kwetu? Wameangalia nini itakuwa impact kwenye grid resistance and inductive reactance watakapounganisha na Tanzania? Je itaunganishwa na na grid iliyopo ya upande wa Tanzania, na kama ndio, wameangalia connectivity? Na isipounganishwa na grid ya Tanzania, siku umeme wa Ethiopia ukifeli then hiyo mikoa ya kaskazini itakuwaje?

Ndio maana nikasema, Samia na Msigwa wasichukulie haya mambo kisiasa katika kutafuta kura za kaskazini na kuwaburuza TANESCO
Fact
 
Kwa wale wanaojenga na wamefikia hatua ya wiring wanafahamu bei za vifaa vya umeme kama ukiamua kuelekezwa na fundi vitu vya kununua bila kumhusisha fundi kwenye manunuzi.
Niliishawahi kununua vifaa kwa maelekezo ya fundi, nikagundua kuwa wholesalers wana bei mbili, bei ya mchekea ni vifaa duni wakati kuna bei mbaya ndio vinapaswa kuwa bora .... Lakini sio mara zote.
Tanesco watakuwa wamefanya manunuzi ya vifaa duni vinavyopoteza umeme na kuongeza gharama ambayo wanaitafsiri kuwa hasara kwa makusudi ili waje na utetezi wa program ya East Africa Power Pool.... Huu ni wizi wa kitaasisi unaohusisha nchi za nje. Hizi ni hujuma za wazi kabisa tena zinafanywa bila kuwa na soni.
 
Hata mimi nimeshindwa kushangaa nime pigwa na butwaa. Kutoka Grand renaissance dam ilipo sehemu inaitwa Guba mpaka Arusha Tanzania ni 2,292 Km. Inaweza ikapungua kidogo au ikaongezeka kidogo. Hivyo transmission loss inategemea kuwa kubwa. Mwalimu wangu wa umeme nikiwa Tanga Technical school form one alinifundisha kuwa ' The longer the wire, the bigger the resistance'. Kutoka Mwalimu Nyerere Dam mpaka Arusha city ni kama 800 Km ya weza kuwa zaidi kidogo au pungufu. Kwa mujibu wa Mwalimu wangu wa Electrical Engineering ni wazi kuwa umeme toka Ethiopia unapotea mwingi toka kwao mpaka Arusha /Moshi kuliko wa Nyerere Dam mpaka Arusha / Moshi. Labda wenzetu wanatumia 'Hardened copper'. Na Tanesco wanatumia Bronze wala siyo normal Copper.
 
Tanesco wanamzunguka mama ili wamharibie duuh !
 
Nimeona mahali wanasema eti ni kwa usalama wa nishati (energy security) kuchukua umeme vyanzo mbalimbali.

Sasa najiuliza, energy security kwa Tanzania ni kwa mikoa ya Kaskazini tu? Hapo ndipo akili ya Tanesco imeishia katika suala la energy security?

Halafu sasa, wao wameshasema ni kwa ajili ya transmission losses kubwa. Sasa wanabanwa wanaanza kusema ni kwa ajili ya energy security!
Na wakumbuke walisema tanzania itakuwa na umeme wakutosha na mwingine watauza nchi nyingine jirani,hizi kauli bhana,hakika njia ya muongo huwa ni fupi.
 
Tatizo kubwa la wanasiasa wa Tanzania ni kufikiri kwamba Watanzania wote hawana uwezo wa kufikiri, na hivyo huridhika kutoa maelezo mepesi ya kisiasa hata kwenye mambo ya kisayansi.

Mfano ni hili la kupeleka umeme mikoa ya Kaskazini, ambapo Tanesco wanasema gharama za transmission ni kubwa - wao wanaziita hasara, na ni afadhali kununua umeme kutola Ethiopia!

Sasa mtu mwenye akili atajiuliza, kwani huo umeme wa kununua kutoka Ethiopia kuja Tanzania unapitishwa kwenye medium gani ambayo haina transmission losses mnazosema huku kwetu ni gharama sana? Na kumbuka kwamba source ya umeme toka Ethiopia iko mbali zaidi ya source yeyote ya umeme ndani ya Tanzania kwenda mikoa ya kaskazini. Kama transmission losses zinaendana na umbali, basi gharama ya transmission losses ya kuleta umeme toka Ethiopia yapaswa kuwa kubwa zaidi (angalia ramani hapo chini)

View attachment 3265426

Kumbuka kwamba, ili Ethiopia watuuzie umeme wao, lazima wana factor-in transmission losses zao za kutoa umeme Ethiopia kuja Tanzania. Sasa ikiwa sisi Tanzania kulipia transmission losses za Ethiopia ni nafuu kuliko kubeba transmission losses za line zetu wenyewe, ni kitu gani ambacho Ethiopia wanafanya kwenye hiyo transmission line yao kuja Tanzania ambacho sisi kimetushinda kufanya? Tilia maanani kwamba umeme wa Ethiopia na Tanzania wote unatokana na maji, hivyo gharama za uzalishaji ni karibu sawa.

Na mikataba ya kununua umeme ni ya muda mrefu siku zote. Kama issue ni transmission lines, kwa nini tujifunge kwenye mkataba wa muda mrefu (lock in effect) badala ya kuwa na mkakati wa kuboresha transmission lines kwa faida za muda mrefu?

Najua Tanesco mmetoa tamko kuuunga mkono kauli ya Raisi Samia mkijua wazi maelezo yenu hayajitoshelezi. Mmejitoa akili ili msijbu kuendana na kauli za wanasiasa, na si mara ya kwanza mnafanya hivi.

Acheni kuendesha hii nchi kinyume cha maumbile. Serikali iseme ukweli kuhusu lililo nyuma ya pazia kutaka kununua umeme toka Ethiopia. Acheni maelezo ya kisiasa kwenye mambo ya kisayansi.
Halafu huo umeme wa Wahabeshi tunaulipia kwa dollar kama petroli
 
kwamba tunanunua umeme kutoka Ethiopia kupitia Kenya
Halafu sisi Tz tunawauzia Kenya
kwmba umeme wa Ethiopia unazalishwa kwa gharama nafuu na no mwingi kuliko sisi ao megawatts 6000 sisi megawatts 2000
🤔🤔🤔🤔
Yaani mimi sijaelewa kabisa
 
Hawa watu katika kukuelewesha huwa wanakuchanganya ili uelewe! Watasema hatujasaini mkataba wa bandari ya Bagamoyo, ila tumewapa waarabu bandari, kwa hiyo msihofu hakuna mkataba mbovu umesainiwa!
 
Uzuri wa mainjinia wa Tz linapokuja swala la upigaj huwezi warudisha nyuma 😂😂
 
Kuna mkanganyiko. Ufafanuzi wa kitaalamu unahitajika!

IMG-20250310-WA0006.jpg
IMG-20250310-WA0008.jpg
IMG-20250310-WA0007.jpg
IMG-20250309-WA0077.jpg
IMG-20250310-WA0009.jpg
 
Kutoka kutaka kuuza mpaka kununua umeme Ethiopia lol!

Kama tunashindwa kuutoa umeme bwawa la mwalimu nyerere kwenda kigoma na Arusha ndio tutaweza kuutoa bwawa la mwalimu nyerere kwenda DRC au tulitaka kuuza online?
 
Back
Top Bottom