Jamani, Tanesco, nalia na nyie! Mtatutoa roho nyie. Yaani mtu unanunua umeme wa shilingi elfu 20, unapewa umeme wa shilingi elfu 10? Hivi nyie mna matatizo gani?
Iko hivi, juzi umeme kwangu uliisha usiku, nikasema ninunue umeme wa elfu 5, ukagoma. Nikajua labda pesa haitoshi, nikiongeza elfu 20, nikanunua wa elfu 5, bado ukagoma.
Ninawapigia simu, hampokei. Are you guys serious? Yaani mtu unalala usiku kucha bila umeme, bila sababu ya msingi. Nimeamka asubuhi, bado nikajaribu kununua, mkagoma.
Nawapigia, mnaniambia nadaiwa miezi mitatu kodi ya pango. What is kodi ya pango? Kila nilipokuwa nikinunua umeme, mnakata pesa halafu mnakuja kuniambia nadaiwa elfu 6 ya kodi ya pango?
Haya, tuseme nadaiwa. Kwanini mimi ninalala usiku kucha bila umeme? Na uzembe ni wa kwenu? Nani aliwaambia mmalize miezi mitatu mfululizo bila kukata hiyo kodi? Na hiyo kodi ya pango mnayoisema ni ipi wakati kila nikinunua umeme mnakata?
Basi haya, mkakataa kunipa umeme mkasema mpaka ninunue umeme kuanzia elfu 6 na miatano ili mkate pesa yenu. Nimenunua umeme wa elfu 20, mmenipa umeme wa elfu 11, kwanini? Hivi nyie? Oooh, mpaka nashindwa kuandika kwa sababu ya hasira nilizonazo.
Jamani wana JamiiForums, naomba muangalie hizo picha hapo, mnisaidie na nyie, mnakutana nayo haya au?Baada ya kunikata hiyo pesa, nawapigia, wananiambia ni makato, like seriously???? Yaani nimekatwa elfu 9 yote halafu Serikali inajivunia kukata makato yote haya huku sisi nyoyo zinawaka moto.
Hizo screenshots