TANESCO ndilo shirika linalochukiwa zaidi Tanzania kwa mwaka 2023, hadi wahubiri wawaomba waumini kuwasamehe

TANESCO ndilo shirika linalochukiwa zaidi Tanzania kwa mwaka 2023, hadi wahubiri wawaomba waumini kuwasamehe

Resilience

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2023
Posts
1,096
Reaction score
4,948
Tatizo la umeme lilianza January Makamba aliitisha kongamano kubwa la matajiri na viongozi mbalimbali kwa fedha nyingi za serikali.

Tatizo la TANESCO lilipanuka pale ambapo wanasiasa akiwemo Naibu WAZIRI Mkuu Biteko alipoanza kufanya siasa na kuacha kusema kweli kuhusu undani wa tatizo

Tatizo lilizidi kukuwa pale Mwenyenzi Mungu alipoleta mvua ambayo ilifuta kauli za ulaghai za wanasiasa kwamba mgawo unatokana na ukame.

Changamoto ilizidi kupanuka pale watendaji wa TANESCO walipokosa wakuwakemea au kuwawajibisha.

Kwa ujumla wamewakwaza wengi hasa ikizingatiwa ni shirika linalolipwa fedha za maslahi makubwa nchini.

Viongozi wa dini wameliona tatizo laTANESCO na kutuomba tuwasamehe ili Mwenyenzi Mungu afungue njia tupate watu sahihi kwenye sekta hii. Tumelitangaza shirika linalochukiwa ila pia tuamue sasa kusamehe may be 2024 Mwenyenzi Mungu atamwonyesha Mh. Rais safu mpya itakayosaidia kuondoa hizi fedhea.
 
Hatuna tatizo la umeme nchini, bali hakuna utashi wa kisiasa karika kuamua kuleta suluhisho. Tatizo lililopo limepikwa kwa makusudi ili kuwanufaisha baadhi ya viongozi na wafanyabiashara wakubwa.

Tatizo kubwa kwa sasa hatuna vyombo makini vya habari ama wanahabari wenye kuweza kufanya habari za kiuchunguzi na kuibua na kuweka hadharani madudu haya. Zipo tetesi nyingi lakini hakuna mfukunyuzi mwenye kuweza kuweka ama kuvujisha habari.

Angetokea mzalendo mmoja wa kuvujisha siri kama yule wa kwenye IGA tungaliweza kufahamu mambo mengi.
 
Viongozi wa dini wameliona tatizo laTANESCO
,
20230929_221501.jpg

itakayosaidia kuondoa hizi fedhea.
20230403_222344.jpg
 
Mungu utuhurumie sisi wananchi wako tunaoteseka , viongozi wa serikali wao hawajui kero ya kukosa umeme kwa sababu wana uwezo wa majenereta , Sola nk.
Sisi wengine tumekosa umeme Sikukuu hii muhimu sana kwetu.
Mwenyezi Mungu wewe ndiye unayejua dhamira zilizopo mioyoni mwa watawala wetu hawa, wewe ndiye unayejua Kama ni viongozi wa haki au wa dhuluma.
NAKUOMBA UWAADHIBU WAO NA FAMILIA ZAO ILI NAO WAFADHAIKE. MUNGU WA DAUDI ULIWAINUA WAFALME NA WATAWALA TANGU ENZI ZA KALE NA ULIWASHUSHA NA KUWAADHIBU WALE WALIOKUWA WAMEJAWA KIBURI, UKATILI NA UBINAFSI.

NA IWE HIVYO EEEH MWENYEZI MUNGU
 
Back
Top Bottom