TANESCO: Pamoja na mvua kunyesha bado maji hayatoshi kuzalisha umeme wa uhakika

TANESCO: Pamoja na mvua kunyesha bado maji hayatoshi kuzalisha umeme wa uhakika

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
66,537
Reaction score
75,687
SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limesema pamoja na mvua zinazoendelea kunyesha lakini bado hazijasaidia kutoa kiwango cha juu cha maji kinachoweza kupata umeme wa uhakika.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Msemaji wa Shirika hilo Elihuruma Ngowi, wamekagua mabwawa mbalimbali ya kufua umeme kwa njia ya maji ikiwemo kituo cha Hale, ambacho kinazalisha megawati 21 na kwamba kwa sasa kutokana na mtiririko wa maji kuwa wa wastani kinazalisha megawati 10.5.

Alisema kituo kingine ni New Pangani Folls ambacho kinauwezo wa kuzalisha megawati 68, na kwamba uwezo wake umepungua kutokana na mtiririko mdogo wa maji na kwa sasa kinazalisha megawati 10 asubuhi na 40 jioni.

“Pia tulifika kwenye kituo cha Kidatu ambacho kinauwezo wa kuzalisha megawati 204, lakini kutokana na mtiririko wa maji kuwa wa wastani mitambo iliyoko hapo inafua umeme wa megawati 194,” alisema na kuongeza:

“Bwawa lingine ambalo tumejionea ni Mtera lililoko mkoa wa Dodoma ambalo linauwezo wa kuzalisha megawati 80, lakini kutokana na mtiririko wa maji kuwa wa wastani umeme unaozalishwa kwa sasa ni megawati 75, hali inayosababisha kuwe na upungufu wa megawati tisa,” alisema Ngowi.

My Take.
Umeme wa Maji sio rafiki.
 
Hii inashangaza kidogo,

Tanesco.png

Tuambiwa mabwawa hayana maji ya kutosha na mara zote ni sababu hizo hizo, ila sasa ni majira ya mvua kubwa sehemu kubwa tu ya nchi lakini ni mwendo wa mgao usio na kichwa wala miguu, na kama siku zote wana sababu zisizo eleweka na za kisiasa.

Kuna haja sasa ya kutaifisha shirika hili na serikali ibaki na udhibiti wa bei pekee.
TANESCO
 
Prof.Assad alisema maji mengi ya mvua yanaenda baharini utazani bahari ina shida ya maji kuliko sisi
 
Back
Top Bottom