TANESCO: Sasa usambazaji wa umeme nchini kufanywa na sekta binafsi. Tayari Wawekezaji wameonesha nia ya kuwekeza TZS 3.3T kwa sharti la Ubia

Pole,

Lakini kila kitu ni hatua kwa hatua ipo siku tutafika tu ndg yangu
 
Uhuni mtupu.

Yaani miundombinu ijengwe kwa jasho na damu la mikopo halafu waje wezi kudandia treni na kujizolea faida.

Acheni uhuni basi kwa mali za nchi.
Wewe ndio muhuni ila haya mambo ni faida kwa Taifa
 
PPP kama PIPI tu
 
Itajwe transfer moja tu iliyofanyika kwa ufanisi ndipo tuendelee na PPP ya Kafulila kwa TANESCO.
Isiwe ni nyimbo nzuri za kikasuku tukielekezwa kwenye kipigo.
 
PPP nimeanza kuwakubali
 

ADANI analetwa kinyemela
 




Wahindi hawa wameshahonga sana. Yaani kwa ufupi shirika la Tanesco ni kama linauzwa kitu ambacho ni ujinga maana hatuna kamati au team yeyote ya maana ya kuangalia bei za umeme! Hasa kuwa na watu waaminifu. Wenzetu wakiweka kampuni za hivi wanakuwa na idara maalumu ya kuangalia bei tatizo letu kila mtu mla rushwa maslahi ya taifa yako nyuma ya matumbo ni bora Tanesco yetu kuliko kuingia hii mingenge maana hatupo tayari
 
Huyu Kafulila anataka kuturudisha tulikotoka na ni hatari kwa usalama wa nchi yetu. Anataka kubinafisha Tanesco yetu kwa jina la PPP. Kazi ya usambazaji umeme ni ya serikali kupitia taasisi yake ya Tanzania Electricity Supply Company kwa kifupi TANESCO.

Akidekezwa atabinafisha pia na uasambazaji wa maji nchini kwa njia hiyo hiyo ya PPP. Ni hatari, tutaweza kunyweshwa hata sumu .
Gharama za umeme zitapanda sana na hatutakuwa na namna ya kudhthibiti. Tumeshuhudia PPP inavyofanya kazi pale daraja la Nyerere la Kigamboni wananchi wanavyolazimika kulipa kiasi kikubwa cha pesa kupita daraja hilo despite hiyo PPP ni kati ya NSSF na serikali. Jee ingalikuwa ni kati ya kampuni binafsi ya Mchina na serikali si ingalikuwa balaa zaidi.

TANESCO yetu ilikuwa inaendelea vizuri sana. Tumemaliza ujenzi wa mitambo ya uhakika ya uzalishaji umeme pale bwawa la NHPP kwa fedha zetu wenyewe kiasi cha trillion 7. Tulitarajia sasa tutajenga na kuboresha njia za usambazaji wa huo umeme kwa njia hiyo hiyo ya kutumia pesa zetu wenyewe hata kama ni kwa kukopa. Gharama hii ya ujenzi na uboreshaji wa njia za usambazaji ilitarajiwa kuwa ndogo sana ikilinganishwa na hiyo ya ujenzi wa NHPP, si zaidi ya trillion 2. Iweje sasa tuingize watu binafsi kwenye usambazaji wa umeme wetu ambao tulingojea bei yake kwa unit iteremke kuwa sawa na ile ya ughaibuni na uchina ili viwanda vyetu viweze kushindana kwenye soko la dunia na watanzania watumie umeme badala ya kuni kupikia vyakula vyao?

Kafulila afungwe spana kwenye jambo hili. Hizo PPP zake azipeleke kwenye kilimo cha umwagiliaji au kwenye mifugo na nyuki. Asicheze na vitu nyeti vya usalama na usitawi wa taifa letu na wananchi wake kama umeme, maji na njia za usafirishaji kama barabara, reli na bandari.
 
Muhimu viongozi wetu kwa kuweka wawekezaji Bei za umeme punguza walau iwe sh. 100 kwa unit ili tupikie umeme.
 
Muhimu viongozi wetu kwa kuweka wawekezaji Bei za umeme punguza walau iwe sh. 100 kwa unit ili tupikie umeme.
Tanesco inaendeshwa kwa ruzuku. Je mtu binafsi atafidiaje hizo gharama.
 
Wafanye km mitandao ya simu, leo kila mtu ni rahisi kumiliki na kutumia simu na mtandao wowote anao uhitaji. Tanesco imetutesa sana, inabidi watu binafsi wapewe mwanya wa kuuza umeme, ili watu wapate huduma ya umeme kila kona ya nchi. Umeme siyo anasa tena, umeme ni huduma ya muhimu sana ktk maisha ya binadamu.
 
Watu binafsi wanaweza peleka umeme kijijini kwa tsh 27000?
 


 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ