Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Mwanachama wa JamiiForums.com aliyejitambulisha kuwa ni Mkazi wa Bariadi katika Kata ya Muamatondo amedai kunachangamoto kubwa ya kukatikakatika kwa umeme hasa katika Kijiji cha Mwasinasi.
Hoja ya Mdau ipo hapa ~ Kata ya Muamatondo wilaya ya Bariadi suala la umeme kukatika limekuwa kero sana
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Simiyu limeelezea kuhusu suala hilo kwa kusema limeona hoja ya Mdau.
Afisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja Tanesco Mkoa, Adeline Lyakurwa anaelezea:
"Hiyo taarifa tumeiona, lakini kwanza mfumo wetu wa TANESCO kuna namba za mawasiliano ambazo Mwananchi anaweza kuripoti tatizo au changamoto kisha tukaishughulikia.
"Kuhusu suala hilo, siku za nyuma kulikuwa na changamoto, Transfoma ilikuwa na shida na ilisababisha kuwe na changamoto ya umeme lakini katika suala hilo hakuna mteja ambaye ameripoti.
"Wateja wengi wamekuwa wakilalamika kwenye Vyombo vya Habari bila kufikisha taarifa rasmi kwenye eneo husika.
"Tatizo la Transfoma lilishughulikiwa lakini tumetuma mafundi kwenda eneo la tukio kuona kuna changamoto gani, kwani mara nyingi mteja akiripoti tatizo linashughulikiwa na anapata majibu ndani ya Saa 24.
"Pamoja na hivyo asili ya Mkoa wa Simiyu umeme unsafiri umbali mrefu sana, unatokea Bunda, Magu, Shinyanga na ndio maana Serikali ikaone itengemeze kituo cha kupoza umeme, Mkandarasi yupo 'site'.
"Tumeshazungumza na Wadau wa Simiyu na wanajua changamoto ambayo tunaipitia.
"Niwaombe Wananchi wanapokuwa na changamoto wanaweza kupiga simu kwenye namba 0734013113, 0748550000 ambayo pia inapatikana kwa njia ya WhatsApp, kwa maombi ya umeme pakua NIKONEKT App au piga *152*00#.”
Pia soma ~ Adeline Lyakurwa: Ndege alinasa kwenye nyaya za umeme, mafundi wamerekebisha, umeme umerejea Bariadi (Simiyu)