TANESCO, Songas zamaliza Mkataba wa Uzalishaji Umeme. Serikali yagoma kuendelea na mkataba kulinda maslahi ya nchi

Sikubaliani na wewe kuhusu elimu ya sheria za kimikataba ya kimataifa. Nadhani kinachomiss ni uzalendo ila elimu ipo ya kutosha. Wakipewa rushwa wanaachia vifungu visivyo na masilahi kwa taifa viingie kwenye mikataba. Kusoma na kuelewa ni kitu kimoja na kulinda masilahi ya taifa ni kitu kingine
 
na investment waliyofanya ni hasara kwa nani ? mbona wame invest pakubwa na muda ni mdogo miaka 20 tu? hapa naona kabia tunapelekwa mahakamani tena
 
Issue ni terms za mkataba ambao una capacity charges ambazo lazima ulipe whether umeingiza umeme kwenye grid au hujaingiza.

Ili kujibu hoja yako ya mapungufu ya umeme yanayojitokeza mara kwa mara, la msingi kufanyika ni Serikali kununua mitambo hiyo ili kuja kuitumia italapohitajika. Lakini ku extend mkataba HAPANA.

Kama wameshtaki kwenye hizo Mahakama zao kama watashinda ni bora walipwe watokomee tu kwa sababu malipo ni mara moja tu
 
Ulipaswa useme songas walikua wanaingiza megawatt ngapi kwenye grid ya taifa ili tuone hilo gap kama haliwezi kufidiwa na bwawa
 
Kwani mkataba umevunjwa au umefika ukomo wake?
Mkataba umefika kikomo lakini sio kikomo, mnapoambiwa mnasaini mikataba ya milele alafu mnabisha ndio muone sasa

Mkataba wa songas umeisha, Ila wameenda mahakamani kushtaki na wanadai fidia zaidi ya trillion 3. Maana kwenye mkataba mlosema ukiisha kutakua na automatic renewal. Yaleyale ya DP world, ni miaka 30 lakini ikiisha ni lazima kuwaongezea. Hiyo ndio mikataba mnasaini
 
Why not, hatuna umeme wa kutosha bado, sehemu kubwa ya nchi hakuna umeme wa kutosha, sehemu kubwa Tanzania huwezi kufungua kiwanda cha maana sababu hakuna umeme wa kutosha, labda kama unaongelea umeme wa kuwashia vibatali
Si kweli. Songas walikua wanazalisha megawst 190 tu. Kwa sasa umeme unaozalishwa ni megawatt zaidi ya 3000, huku mahitaji yakiwa chini ya megawatt 2000. Hivyo bado tuna ziada ya umeme. Na hapo bado bwawa halijazalisha kwa 100%. Kuhusu uoungufu wa umeme hilo liondoe
Umeme utakwama kwa mengine(miundombinu ya usafirishaji)
 
Asante shujaa wetu kwa kuanzisha ujenzi wa bwawa la Nyerere. Bila wewe kuanzisha huo mradi tungeendelea kupigwa mpaka tukomae. Sasa tunao ujasiri wa kusitisha mikataba isiyo na maslahi mapana kwa taifa. Rip JPM!
JPM aliyafanya haya akitimiza ilani ya CCM, mahaba yetu yanampa heshima kubwa huku tukisahau yeye alitimiza ilani ya Chama chake baada ya kukabidhiwa na kuagizwa aitimize.
 
na investment waliyofanya ni hasara kwa nani ? mbona wame invest pakubwa na muda ni mdogo miaka 20 tu? hapa naona kabia tunapelekwa mahakamani tena
Kupelekwa mara ngapi? Tayari huko wanadai fidia ya zaidi ya trillion 3. Mliwaahidi mkataba ukiisha mtawaongezea
 
Kama huo mkataba ni mbovu ni nani ali authorize kusainiwa kwake ?
Na ni nani amefanya assessment ya kina na kuona kwamba Taifa lipo secured interns ya uhakika wa nishati ya umeme kama hao Songas wataondoka huduma zao katika grid ya Taifa ?
Hivi kuna taahira anayeweza kusema hii nchi iko salama na kujitosheleza kwa upande wa nishati ya umeme ?
Hivi hii sera ya viwanda huwa wanamwimbia nani ?
Hivi ni mpuuzi gani anaweza kuja kufunga heavy manufacturing facility au data center Hapa nchi Kwa scarcity ya nishati hii ya umeme na price rates za juu kiasi hiki ?

Kweli ukitaka kuangamiza taifa , haribu akili za watu wake , hii ni symptom ya upungufu wa akili , nchi kama Rwanda kila siku wanawaza kuongeza vyanzo vya kuzalisha nishati ya umeme na kufanya diversification katika power grid Yao ,Yani kuwana vyanzo mbalimbali vya ufuaji wa umeme ,sisi Taifa la watu wenye mitindio wa ubongo tunawaza kutegemea hydro power ambayo hata bado haitimizi demand ya sasa let alone matumizi ya nishati yanayoongezeka kila siku ,
Rwandan wana jenga kinu cha nuclear ,hawa nguruwe wa hili taifa wanawaza kupunguza miradi ya umeme , mbwa kabisa

Nchi kama China wanajenga kinu cha kufua umeme kwa kutumia coal kila wiki ,na hapo wana nuclear power plants za kutosha ,mega hydro power plants idadi isiyohesabika , wana wind power farms na solar power farms projects kubwa kuliko zote duniani ,na bado wanaongeza kila siku , taifa masikini la mbumbumbu kama hili bado linaamini umeme ni luxury ,wakati umeme ni nyenzo muhimu katika jamii na uchumi wa nchi kama zilivyo reli , barabara ,bandari nk
Imagine Mgodi wa Geita tu pale GGM mpaka mwaka huu walikuwa hawajaingia kwenye grid ya taifa na walikuwa wanazalisha umeme kwa kutumia heavy fuel Kwa generators , sasa ukiangalia cost effectiveness hapo haipo ,that's means hao wawekezaji wetu walikuwa wanafanya kazi kwenye mazingira magumu ,kwani cost ya investment kwenye kufua umeme kwa mafuta ni kubwa mara dufu kuliko kama wangekuwa wamefungwa kwenye grid ya taifa , sasa hapo unakuwa unaua hata hamu ya wawekezaji kujitanua na kuanzisha miradi mingine nchini au kuja nchini kuwekeza na hivyo kuzalisha ajira na mapato kwa nchi .
Policy makers WA hii Nchi ni mataahira
 
Ulichoandika ndio sahihi, lakini likija suala la mama samia mnajitoa ufahamu inakua sio ilani wala chama chake Bali ni yeye tu anaupiga mwingi
Mama Samia anafanya mengi sana na ya msingi, tatizo letu tunamtazama kwanza akiwa ndani ya akili zetu ni mwanamke wa kizenji.

Mipango ya Mungu tofauti sana na ya kwetu wanadamu, alitaka ukifika mwaka 2024 Novemba nchi iongozwe na Rais wa jinsia yake.

Kuna miradi mingi mipya inafumuka kama uyoga huko mikoani, hatuwezi kuijadili kwani hatuifahamu.
 
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limetangaza rasmi kumalizika kwa mkataba wa ununuzi wa umeme kati yake na kampuni ya kuzalisha umeme kwa njia ya gesi asilia ya Songas. Mkataba huo wa miaka 20 ulifikia mwisho tarehe 31 Oktoba 2024.

Katika taarifa iliyotolewa na TANESCO kupitia Kurugenzi yake ya Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma, Makao Makuu, Dodoma, Novemba 1, 2024, shirika hilo limewahakikishia wateja wake kuwa hali ya upatikanaji wa umeme nchini itaendelea kuwa nzuri licha ya kumalizika kwa mkataba huo.

"Shirika linapenda kuwahakikishia wateja wake kuwa hali ya upatikanaji wa umeme nchini ni nzuri kwa kuzingatia vyanzo mbalimbali vya uzalishaji wa umeme," imesema taarifa hiyo.

TANESCO imefafanua kuwa kwa sasa ina uwezo wa kuzalisha umeme kwa kutumia mitambo inayotumia maji, ambayo ina nguvu zaidi ya kutosheleza mahitaji ya umeme hapa nchini. "Uwezo wa uzalishaji wa umeme kwa kutumia mitambo ya maji ni mkubwa kuliko mahitaji ya umeme hapa nchini," imeeleza taarifa hiyo.

Shirika hilo limeongeza kuwa maendeleo ya Mradi wa Bwawa la Kufua Umeme la Julius Nyerere, ambao tayari umeongeza megawati 940 kwenye Gridi ya Taifa, yamechangia katika kuhakikisha usambazaji wa umeme nchini unakuwa thabiti na wa uhakika.

"Maamuzi ya Serikali kutokuendelea na mkataba huu ni kwa ajili ya kulinda maslahi mapana ya nchi," imeeleza TANESCO katika taarifa hiyo. "Hivyo, Serikali kupitia Wizara ya Nishati na TANESCO itaendelea kusimamia sekta ndogo ya umeme ili kuhakikisha kunakuwa na huduma bora, endelevu na ya uhakika ya umeme."

Kwa mafanikio ya maendeleo ya Mradi wa Bwawa la Umeme wa Julius Nyerere, Tanzania sasa iko katika nafasi nzuri zaidi ya kukidhi mahitaji yake ya nishati kwa kujitegemea katika nishati.

Uamuzi huu umeelezwa kuakisi dhamira ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha upatikanaji wa umeme wa kuaminika, wa bei nafuu, na endelevu kwa Watanzania wote.

Chini ya uongozi wake, serikali imeweka kipaumbele kwenye miradi mikubwa ya nishati, ikiiwezesha TANESCO kuongoza katika kuhakikisha upatikanaji wa umeme imara kote nchini.

Hatua hii ya kimkakati inalenga kulinda maslahi ya taifa, kuunda nafasi za ajira, na kukuza uchumi.

Chanzo ni jambo Tv
 
Tuna coal kule njombe tuna abundant reserve ya makaa ya mawe ya quality nzuri kule songea na Songwe , yet tumeshindwa kujenga hata mega project moja ya kufua umeme kwa uhakika toka moja ya hizo sites ili kupata umeme wa uhakika .
Majitu yanawaza upumbavu tu wa kujinufaisha kwa mikataba ya wizi na ushenzi mwingine usioeleweka .
Mabadiliko ya tabia ya nchi tu yenyewe ni clear indicator kwamba Hydro Electrical power si reliable ndani ya miaka michache ijayo kwani ukame unazidi kuongezeka , na bila maji huwezi tembeza hizo turbines kuzalisha power .
Sasa hivi kuna vyanzo kibao vya kama hizi small Modular reactors (SMR) ,ambapo ni ndogo ,reliable ,cost effective ,mobile (rahisi kuhamisha ) ,safe (salama kuliko old ones ) na consumption take ya maji ni ndogo mno so ni effective kuoperate hata kwenye ukame
Na unaweza kufunga katika several small units na kutengeneza power plant kubwa na ,unaweza kuhamisha pia ,kitu ambacho ni advantage kubwa katika aspects nyingi kulinganisha na njia za kufua umeme kama hydro electric power .
 
Hakuna umeme wa kutosha Tanzania, jaribu kufungua kiwanda au mgodi wa maana ndio utajua, utaishia kutumia generator hata kama gridi ya Taifa inapitia mtaa wa pili
Ndio maana huwa nawashangaa hawa wapumbavu wanapojadili hii crisis ya umeme nchi as if umeme nchi hii matumizi yake ni kuwasha taa tu ,akili dumavu ni tatizo sana .
Hapo hapo yanawaza Tanzania ipate wawekezaji katika miradi mikubwa kama viwanda ,migodi na heavy investments nyingine bila kujua wawekezaji si wapumbavu na wanafanya research kabla ya kuwekeza katika miradi hiyo kwa kuzingatia upatikanaji wa uhakika wa nishati na katika rate au bei nafuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…