Stuxnet
JF-Expert Member
- Feb 12, 2011
- 13,417
- 23,310
Absolutely Januari angewapa. Yule ni corrupt vibaya sanaAngekuwepo january wizarani lazima angewapa mkataba
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Absolutely Januari angewapa. Yule ni corrupt vibaya sanaAngekuwepo january wizarani lazima angewapa mkataba
Hadi wanatia aibu aiseeHawa ndio makamanda wa Chadema bhana...
Hapa wako bize kutetea beberu.
Ni akili ndogo na ile hali ya kutaka kujifanya wako kinyume na serikali kwa kila kitu.Hadi wanatia aibu aisee
Sikubaliani na wewe kuhusu elimu ya sheria za kimikataba ya kimataifa. Nadhani kinachomiss ni uzalendo ila elimu ipo ya kutosha. Wakipewa rushwa wanaachia vifungu visivyo na masilahi kwa taifa viingie kwenye mikataba. Kusoma na kuelewa ni kitu kimoja na kulinda masilahi ya taifa ni kitu kingineTanzania bado sana katika eneo la mikataba na makampuni ya kimataifa.
Taifa liwekeze katika elimu iliyo sahihi kupambana ktk dunia hii ya utandawazi, na pia lugha ya kimataifa ya kiingereza tangu darasa la kwanza.
Ndipo tutafanikiwa kuwa na wanasheria wabobezi katika mikataba ya kimataifa, tukiendekeza kiswahili chetu pekee lazima tutaendelea kuwa wanyonge kimataifa.
na investment waliyofanya ni hasara kwa nani ? mbona wame invest pakubwa na muda ni mdogo miaka 20 tu? hapa naona kabia tunapelekwa mahakamani tenaKUMALIZIKA KWA MKATABA WA UNUNUZI WA UMEME KATI YA TANESCO NA KAMPUNI YA UZALISHAJI UMEME KWA NJIA YA GESI ASILIA YA SONGAS
ljumaa 01 Novemba, 2024
Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) linapenda kuufahamisha umma kuhusu kumalizika kwa mkataba wa ununuzi wa umeme kutoka Kampuni ya uzalishaji umeme kwa njia ya Gesi asilia ya Songas. Mkataba huu umedumu kwa muda wa miaka ishirini (20) na umefikia ukomo wake jana tarehe 31 Oktoba 2024.
Pia soma: Serikali: Mkataba wa Songas kumalizika Julai 2024
Pamoja na kufika ukomo wa mkataba huu Shirika linapenda kuwahakikisha wateja wake kuwa hali ya upatikanaji wa umeme nchini ni nzuri kwa kuzingatia vyanzo mbalimbali vya uzalishaji wa umeme ambapo kwa sasa uwezo wa uzalishaji umeme kwa kutumia mitambo ya Gesi asilia na mitambo inayotumia maji ni mkubwa kuliko mahitaji ya umeme hapa nchini.
Hali hii imechangiwa na maendeleo mazuri ya Mradi wa Bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere ambalo mpaka sasa jumla ya megawati 940 zimeungwa kwenye Gridi ya Taifa.
Pia soma: Ujue kwa ufupi: Mkataba wa Songas na TANESCO unaotarajiwa kufika tamati Julai 2024
Maamuzi ya Serikali kutokuendelea na mkataba huu ni kwa ajili ya kulinda maslahi mapana ya nchi. Hivyo, Serikali kupitia Wizara ya Nishati na TANESCO itaendelea kusimamia sekta ndogo ya umeme ili kuhakikisha kunakuwa na huduma bora, endelevu na ya uhakika ya umeme.
Pia soma: Hii ndio hatari inayoweza kujitokeza baada ya mkataba wa Songas kumalizika
View attachment 3141013
Issue ni terms za mkataba ambao una capacity charges ambazo lazima ulipe whether umeingiza umeme kwenye grid au hujaingiza.Bado tunahitaji umeme kuliko unaozalishwa na TANESCO, si wangeendelea kununua tuu kwa bei inayoeleweka sawa na vyanzo vingine kuliko kuachia investment ya mabilioni iondoke kirahisi hivyo, kesho utasikia maji au mitambo imejaa tope umeme hakuna, I hope wafanye mkataba mpya kwa terms nzuri za upande wetu kuliko kupoteza imani ya investors na kuishia mahakamani na kushindwa
Kwani mkataba umevunjwa au umefika ukomo wake?Mhhh subirini mahakamani huko uingereza
NCHI BADO INAHITAJI UMEME MWINGI, SITISHO HILI LA GESI YA SONGAS KUTAPELEKEA UPUNGUFU WA NISHATI UMEME WA UHAKIKA
TANESCO waache mihemuko, ni vinu 3 tu vya bwawa la JNHPP namba 9, namba 8 na namba 7 kati ya vinu 9 ndivyo vinafanya kazi.
Huo umeme wa kutosha kutoka bwawa la JNHPP unatoka wapi ?
Mradi wa JNHPP Rufiji unajengwa na kampuni ya kidola ya Egypt na hadi sasa ni vinu 3 katika ya tisa ndiyo vinazalisha umeme. Vinu turbines hivyo ni namba 9, namba 8 na namba 7.
Kila kinu kinauwezo wa kuzalisha 235MW. Uzalishaji ukifanywa kwa vinu vyote 9 kwa pamoja nchi itapata jumla ya 2115 MW za ziada kuingiza katika gridi ya taifa.
Za ndani mradi wa JNHPP
Arab Contractors kampuni ya Egypt ikionesha ulipofikia mradi wa JNHPP Rufiji nchini Tanzania hadi mwezi August 2024 vinu vitatu namba 9, namba 8 na namba 7 vikizalisha umeme. Kila kinu turbine kina uwezo wa kutoa 235MW. Kazi inaendelea ili vinu vingine 6 viweze kukamilika. Mbali na hilo la vinu / turbine kazi za kujenga miundi mbinu muhimu kama saddle dam yaani kuimarisha kingo za ziwa la kuhifadi maji n.k zinaendelea .
View: https://m.youtube.com/watch?v=pRU6w6gJmfw
Mkataba umefika kikomo lakini sio kikomo, mnapoambiwa mnasaini mikataba ya milele alafu mnabisha ndio muone sasaKwani mkataba umevunjwa au umefika ukomo wake?
Si kweli. Songas walikua wanazalisha megawst 190 tu. Kwa sasa umeme unaozalishwa ni megawatt zaidi ya 3000, huku mahitaji yakiwa chini ya megawatt 2000. Hivyo bado tuna ziada ya umeme. Na hapo bado bwawa halijazalisha kwa 100%. Kuhusu uoungufu wa umeme hilo liondoeWhy not, hatuna umeme wa kutosha bado, sehemu kubwa ya nchi hakuna umeme wa kutosha, sehemu kubwa Tanzania huwezi kufungua kiwanda cha maana sababu hakuna umeme wa kutosha, labda kama unaongelea umeme wa kuwashia vibatali
JPM aliyafanya haya akitimiza ilani ya CCM, mahaba yetu yanampa heshima kubwa huku tukisahau yeye alitimiza ilani ya Chama chake baada ya kukabidhiwa na kuagizwa aitimize.Asante shujaa wetu kwa kuanzisha ujenzi wa bwawa la Nyerere. Bila wewe kuanzisha huo mradi tungeendelea kupigwa mpaka tukomae. Sasa tunao ujasiri wa kusitisha mikataba isiyo na maslahi mapana kwa taifa. Rip JPM!
Kupelekwa mara ngapi? Tayari huko wanadai fidia ya zaidi ya trillion 3. Mliwaahidi mkataba ukiisha mtawaongezeana investment waliyofanya ni hasara kwa nani ? mbona wame invest pakubwa na muda ni mdogo miaka 20 tu? hapa naona kabia tunapelekwa mahakamani tena
Ulichoandika ndio sahihi, lakini likija suala la mama samia mnajitoa ufahamu inakua sio ilani wala chama chake Bali ni yeye tu anaupiga mwingiJPM aliyafanya haya akitimiza ilani ya CCM, mahaba yetu yanampa heshima kubwa huku tukisahau yeye alitimiza ilani ya Chama chake baada ya kukabidhiwa na kuagizwa aitimize.
Mama Samia anafanya mengi sana na ya msingi, tatizo letu tunamtazama kwanza akiwa ndani ya akili zetu ni mwanamke wa kizenji.Ulichoandika ndio sahihi, lakini likija suala la mama samia mnajitoa ufahamu inakua sio ilani wala chama chake Bali ni yeye tu anaupiga mwingi
Ndio maana huwa nawashangaa hawa wapumbavu wanapojadili hii crisis ya umeme nchi as if umeme nchi hii matumizi yake ni kuwasha taa tu ,akili dumavu ni tatizo sana .Hakuna umeme wa kutosha Tanzania, jaribu kufungua kiwanda au mgodi wa maana ndio utajua, utaishia kutumia generator hata kama gridi ya Taifa inapitia mtaa wa pili