TANESCO, Songas zamaliza Mkataba wa Uzalishaji Umeme. Serikali yagoma kuendelea na mkataba kulinda maslahi ya nchi

TANESCO, Songas zamaliza Mkataba wa Uzalishaji Umeme. Serikali yagoma kuendelea na mkataba kulinda maslahi ya nchi

Ulipaswa useme songas walikua wanaingiza megawatt ngapi kwenye grid ya taifa ili tuone hilo gap kama haliwezi kufidiwa na bwawa
Songas, Pan-African Energy na wadau wamewekeza fedha kibao, wanamiliki miundo mbinu ya bomba la gesi toka Songo Songo yenye urefu wa kilometa zaidi ya Mia mbili hadi Ubungo Dar es Salaam kwenye mitambo ya kufua umeme. Wawekezaji hawa wamekuwa wadau wa maendeleo endelevu kuhakikisha nishati ya umeme inapatikana kwa uendelevu kukidhi mahitaji ya umeme ...

August 2022

KESHO YA MRADI WA GESI YA SONGOSONGO

PANAFRICAN ENERGY Managing Director, Andrew Hanna MBE highlights the status of PanAfrican Energy Tanzania's Natural Gas Exploration and the foreseeable future

4 August 2022

MGUSO CHANYA WA SONGAS NA PANAFRICAN ENERGY, NDIYO MAANA TUNAWEKA UWEKEZAJI ENDELEVU TUKIANGALIA SIKU ZA USONI

Mkurugenzi wa PANAFRICAN ENERGY Bw. Andrew (Andy) Hanna azungumzia changamoto na mipango endelevu ya mradi wa gesi wa Songosongo kwa kina kabisa kwa kuangalia mwaka 2026....


View: https://m.youtube.com/watch?v=8DnAGTbMDXs
Mradi wa SONGAS unaosafirisha gesi kwa bomba hadi Dar es Salaam kutoka mitambo katika kisiwa cha Songosongo field una changamoto za uchakavu na kuonesha uhalisia wake ambao miaka 30 iliyopita haikufahamika.

Hivyo kuhitaji utafiti wa kina kujua kama kutaanza kuwepo upungufu wa uzalishaji wa gesi ya Songosongo au la kwani kunadalili kisima kupunguza mbinyo (pressure) hivyo kuna hatihati je nini hasa kifanyike kuhakikisha gesi inazalishwa kwa kiwango hitajika hadi mwezi Oktoba 2026 ...

Tumewekeza US$70 milioni kukarabati miundo-mbinu hiyo ili wateja wapate ugavi wa gesi sahihi yenye pressure ya kutosha mfano wateja wetu wa Dar es Salaam..

Pia tumewekeza US$20 milioni kuona visima vingine vya gesi kuingizwa ktk mfumo uliopo, tunategemea kutakuwepo upungufu katika miaka ijayo. Kisima ni kama chupa ya coca cola kwa maana ukiifungua pressure hupungua vivo hivyo visima vyetu pressure yake ni kama ilivyo ktk chupa hupungua na ndiyo maana tunawekeza ktk visima vingine kuhakikisha pressure haipungui katika mfumo mzima wa uzalishaji.

Inabidi twende mbio ili kuhakikisha changamoto ya ugavi wa gesi hauleti matatizo kutokana na uzalishaji. Tumewaingiza watu sahihi na makini kuhakikisha mambo ya ugavi wa gesi haupati changamoto,,watu hao ni PanAfrica Energy, Orca na tunawajibu siyo tu ktk nishati bali hata kurudisha kwa jamii ktk miradi ya afya, elimu, lugha ya kiingereza shule kwa wakaazi wa Songo Songo

Tunaonekana mradi wetu wa Songo Songo kama kitu kidogo lakini kumbuka kuwa visima vyetu katika kisiwa cha SongoSongo, vina upekee maana miundo-mbinu mabomba yetu tunayomiliki yameunganishwa na wateja wetu moja kwa moja waliopo Dar es Salaam.

Lakini tunaangalia soko jingine la Bagamoyo, Morogoro, Kibaha Pwani na hata nchi jirani pia hivyo tunaamini katika hilo ndiyo maana tunaendelea kuingiza mitaji zaidi katika sekta hii muhimu ya nishati kwa nchi ...

Hivyo ni suala complex sana kuweza kupata mtu kama sisi wakuweza kuhakikisha ugavi (supply) wa uhakika ikimaanisha kuendesha mitambo, visima na mabomba ya kufikia wateja wetu watiifu waliopo Dar es Salaam, nasema hvyo kwa kuwa ni eneo nyeti ndiyo maana tumeanza kujitayarisha sasa

Kumbuka suala la kupata gesi kwa kuchimba kisima ni risk sana hivyo tumejitayarisha sasa kutafuta a Rig kuchimba, kuingia mikataba, rasilimali watu wajuzi, kuingiza mitambo nchini n.k ili tusiwaangushe wateja wetu katika eneo la ugavi wa gesi Tanzania ...tumeendelea kuwekeza na kuwekeza ... Pan-African Energy,,SONGAS tupo inagawa hatuonekani katika bidhaa zinazo zalishwa Tanzania katika bidhaa kama ceramic, sigara, pepsi kwa kutaja kwa uchache mguso wetu mkubwa..

Source : The Guardian Digital
 
Biashara siyo mchezo wa hasira, tukae chini tukubaliane kununua kila kitu cha SONGAS ikiwemo mategemeo ya mapato waliyotarajia SONGAS kwa zaidi ya miaka mingine 20 kuanzia 2026 yaani 2050

Sasa kama ilivyotolewa angalizo umeme lazima uwe na vyanzo vingi JNHPP, KIHANSI, KIDATU, MTERA, HALE, SONGAS, MAKAA YA MAWE, UPEPO, JOTO ARDHI (Thermal) n.k

09 March 2025
Same, Kilimanjaro
Tanzania


TANZANIA SASA KUNUNUA UMEME ETHIOPIA


View: https://m.youtube.com/watch?v=9-Th7aD8KCw
Mheshimiwa rais Dr. Samia Hassan akiwa wilaya ya Same mkoa wa Kilimanjaro kuzunduwa mradi mkubwa wa maji, pia ametumia nafasi hiyo kuelezea changamoto ya sekta ya umeme kanda ya kaskazani na kubainisha kuwa serikali ya Tanzania Inapanga kununua umeme kutoka Ethiopia kupitia mpango wa Eastern Africa Power Pool (EAPP) ili kumaliza changamoto ya usambazaji umeme ...

Pia soma makala hii:
TOKA MAKTABA


Africa Energy Insights
https://africaenergyinsights.com
TANZANIA : $1.9 Billion Used On Electricity Network Upgrade

The project will “upgrade power sub-stations and transmission lines across the country to stabilize power supply,” Energy Ministry January Makamba...
 
"Sinunui umeme wako, na makubaliano yamekwisha duration time ni 20yrs, imekamilika, in peace,
That mean kuna phase 2, majadiliano itabidi yafanyike, #SONGAS aombe serekali inunue miundombinu, aidha songas itumie miundombinu hiyo kwa matumizi mengine, aidha apewe kazi ya kuuza gesi daresalam na mengineyo!
Ep-Nahitaji maji hapa, maji yapo rufiji, (do as you can nataka maji hapa utaniuzia, na nayaitaji kwa miaka 30 tu, seller atafanya costing zake kuona akiyatoa rufiji akuletee hapo, akikuchaji kiasi fulani kitamlipa? Kwa miaka 30,after costing ndipo at Ajibu naweza au siwezi, alisema it's OK, maana ametambua ana miaka 30ya kupiga kazi yake!..

UFAFANUZI MSEMAJI MKUU WA SERIKALI KUHUSU UMEME WA ETHIOPIA

March 10 2025
Dodoma, Tanzania

GERSON MSIGWA - TANZANIA KUNUNUA UMEME KUTOKA KAPU LA UMEME (POOL) LA AFRIKA YA MASHARIKI LENYE CHANZO KIKUU KUTOKA ETHIOPIA
1741604898221.jpeg

Sasa taifa la Tanzania lageukia umeme wa Ethiopia kufuatia changamoto ya usambazaji anukuliwa msemaji mkuu wa serikali Gerson Msigwa
 

Serikali Makini, yagoma kuendelea na mkataba kulinda maslahi ya nchi.​

 
Karibuni tena SONGAS.

Shamba la bibi sasa mavuno tele.
 

Attachments

  • Screenshot_20250310_134331_YouTube.jpg
    Screenshot_20250310_134331_YouTube.jpg
    133.6 KB · Views: 1
UFAFANUZI MSEMAJI MKUU WA SERIKALI KUHUSU UMEME WA ETHIOPIA

March 10 2025
Dodoma, Tanzania

GERSON MSIGWA - TANZANIA KUNUNUA UMEME KUTOKA KAPU LA UMEME (POOL) LA AFRIKA YA MASHARIKI LENYE CHANZO KIKUU KUTOKA ETHIOPIA
View attachment 3265603
Sasa taifa la Tanzania lageukia umeme wa Ethiopia kufuatia changamoto ya usambazaji anukuliwa msemaji mkuu wa serikali Gerson Msigwa


Katibu mkuu wizara ya Nishati F . Mramba naye aingilia kati kufafanua zaidi ununuzi wa umeme toka kapu kuu (pool) la umeme wenye chanzo kutoka Ethiopia


View: https://m.youtube.com/watch?v=BwtUSfPZiak
 
Maamuzi ya Serikali kutokuendelea na mkataba huu ni kwa ajili ya kulinda maslahi mapana ya nchi. Hivyo, Serikali kupitia Wizara ya Nishati na TANESCO itaendelea kusimamia sekta ndogo ya umeme ili kuhakikisha kunakuwa na huduma bora, endelevu na ya uhakika ya umeme.

TOKA MAKTABA :

Contributions by Hon. Prof. Sospeter Mwijarubi Muhongo (34 total)​

Hotuba ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa Kufungua Bunge la Kumi na Moja

View: https://m.youtube.com/watch?v=g4Tiwt6Qz-k
WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kabisa nimshukuru Mheshimiwa Rais kuwa na imani na mimi. Vilevile ndugu zangu wa Jimbo la Musoma Vijijini ambao waliamua niwe mwakilishi wao mzuri, tumeanza kujenga uchumi kwa kasi kubwa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hotuba ya Mheshimiwa Rais ni agizo na Wizara ya Nishati na Madini imeanza kutekeleza kwa vitendo. Niwashukuru Waheshimiwa Wabunge wote kwa michango mizuri na wengi ambao wamechangia watakubaliana nami kwamba wengine nimeanza kutatua kero zao. Kwa hiyo, wengi wanaomba umeme. Nawathibitishia Watanzania kwamba unakuja umeme mwingi, wa uhakika na wa bei nafuu. (Makofi)


Mheshimiwa Naibu Spika, wachimbaji wadogo wanatafuta maeneo, na watapewa na vilevile ruzuku itaendelea kupatikana. Tulianza na dola 50,000, tumefika dola 100,000 na tunataka tupate wachimbaji wadogo wanaoweza hata kufika kwenye ruzuku ya dola 1,000,000 au 5,000,000 hivi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, agizo la Mheshimiwa Rais, ni suala la kuondoa umaskini ambao unaendana na kujenga uchumi imara. Ni lazima uchumi wetu ukue kwa zaidi ya asilimia 10 na kufanya hivyo ni kila Mtanzania atumie umeme mwingi, aliyepo shambani na aliyeko kwenye viwanda.


Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sasa hivi wastani wa matumizi ya umeme wetu, kila mtu hapa, hata tuliokaa humu ni unit 9 kwa mwezi. Kazi niliyopewa ni kuwatoa kwenye unit 9 kwa mwezi, kwenda kwenye unit 250 kwa mwezi. Hiyo ndiyo inayoitwa nchi ya kipato cha kati. Tukifanya hivyo, uchumi utakua kwa zaidi ya asilimia10 kutoka asilimia 7 za sasa hivi. Tukiendelea na asilimia 7 na asilimia 8 umasikini hautatoka.


Kwa hiyo, Wizara ya Nishati na Madini inataka ilete umeme mwingi. Tuna vijiji 15,809; asilimia 33 tu ya vijiji hivi ndiyo vyenye umeme. Kwa miaka miwili inayokuja, ni lazima tufike angalau asilimia angalau 67, theluthi mbili ya vijiji hivyo vipate umeme. Sasa hivi ni asilimia 40 ya Watanzania wote wanaopata umeme. Tukitaka kuingia nchi ya kipato cha kati, ikifika mwaka 2025 angalau asilimia 75 ya Watanzania na ikifika mwaka 2030 kwa sababu Tanzania ndiyo iliwakilisha Afrika kwenye mambo ya nishati duniani, ni lazima tuwe zaidi ya asilimia 90 ya Watanzania wanaotumia umeme. (Makofi)


Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, tutafanyaje sasa? Ni kutumia ni vyanzo vyote vya umeme ambavyo tunavyo. Kwa sasa hivi gesi ni karibu asilimia 50, maji asilimia 35 na umeme wa mafuta karibu asilimia 15.


Ni lazima tuachane na umeme wa mafuta, uwe umekaa pale kama tahadhari yetu tu. (Makofi)


Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, tutazalisha umeme mwingi kutokana na gesi asilia, makaa ya mawe na maji. Halafu ndiyo tunakuja nishati jadidifu yaani jua, upepo na mengineyo.


Mheshimiwa Naibu Spika, hii ni kwasababu hesabu hizi lazima ziendane na muda. Leo hii Watanzania tuko milioni 53.5; tutakavyokuwa tunapiga kura mwaka 2020 tutakuwa karibu milioni 65; na tutakapofika mwaka 2025, tukiwa nchi isiyokuwa na maskini na mtu anaamua anachotaka kula, kama mimi napenda muhogo basi tutakuwa karibu watu milioni 80 na uchumi hapa ndugu yangu inabidi Pato la Taifa liwe zaidi ya shilingi bilioni 240 mwaka 2025. Kwa hiyo, niwahakikishie Watanzania umeme wa uhakikia ni lazima. Ahsante. (Makofi
 
Hoja za Hon. Prof. Sospeter Mwijarubi Muhongo

View: https://m.youtube.com/watch?v=xxXYRNArHcY

Mapendekezo ya Mpango wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali katika Mwaka wa Fedha 2016/2017
WAZIRI WA NISHATI NA MADINI:



Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana. Huu ni Mpango mzuri. Waheshimiwa Wabunge mawazo yenu tumeyapata na tutayafanyia kazi na mengine tunayafanyia kazi tayari. Cha maana cha kujua ni kwamba maana ya uchumi ambao unafanyiwa mapinduzi makubwa huwa mara nyingi haukubaliki kiurahisi, ndio historia ya mapinduzi ya kiuchumi duniani. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, upande wa mafuta na gesi, nataka niwaeleze Watanzania ukweli, wengine wamesema hakuna wataalam siyo kweli na wala hatuhitaji kumleta kama alivyosema mwingine mzungu mmoja aje kutufundisha, haiwezekani hiyo. Kwa sababu huku kuna watalaam kweli kweli.


TPDC penyewe kuna Ph.D nne, kuna Masters 62, kuna shahada za kwanza zaidi ya 200. Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kina degree programmes zaidi ya tano, UDOM wapo tano, lengo ni kwamba kwa miaka michache inayokuja Tanzania ndiyo itakuwa na wataalam wengi wa madini na mafuta nchini hapa. (Makofi)


Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile tunasomesha watu, mwaka huu Norway tumemaliza scholarship ya watu 40 na wengine 40 tutaziomba tena. Kwa hiyo, maana ya mageuzi haya tunayoyaongelea ndugu zangu Wabunge yataendana na uchumi wa gesi, ndiyo roho ya mapinduzi ya uchumi wetu na niwahakikishie tuko kwenye njia nzuri. Wanaosema hawaoni faida, umeme utatoka huko, viwanda vya mbolea tutajenga, majumbani tutatumia na gesi tutaisindika.


Mheshimwa Mwenyekiti, niongelee kingine ambacho ni injini ya mageuzi yote haya, ni mambo ya umeme. Ndugu zangu Waheshimiwa Wabunge na Watanzania wote ni kwamba, umeme wa uhakika na umeme wa bei ndogo lazima utapatikana kwenye Taifa hili. (Makofi)


Mheshimiwa Mwenyekiti, tunakwenda kwa mahesabu, sio kwa hisia, sio kwa matusi, sio kwa kumkejeli mtu. Ni lazima tutoke kwenye power per capita, yaani mtu mmoja mmoja, mwenye umeme wa units 108 kwenda units 3000. Ndio kazi ambayo Wizara ya Nishati inaifanya. Hiyo inaendana na ukuaji wa uchumi, utoke sasa hivi asilimia saba mpaka asilimia 10 kwa mwaka ili ifikapo mwaka 2025, tukiwa nchi ambayo ni ya kipato cha kati, yenye Pato la Taifa GDP ya bilioni 240, tunahitaji umeme wa uhakika na Wizara ya Nishati na Madini na Serikali kwa ujumla ndiyo kazi inayoifanya hiyo.


Sasa Waheshimiwa Wabunge kingine ambacho ni cha kufahamu, tumeongelea sana fedha za wafadhili, Watanzania wote naomba tuelewane, fedha za wafadhili ni tofauti na fedha za uwekezaji. Mimi huku Wizara ya Nishati na Madini, hata wakinipatia fedha zote za wafadhili, ni fedha kidogo.


Fedha za wafadhili, wasiojua siyo zaidi ya dola milioni 500 kwa mwaka, dola za Marekani hazivuki milioni 500. Halafu upatikanaji wake, kwa ndani ya miaka 10 hesabu zimepigwa ni wachache wamevuka asilimia 50 ya ahadi walizozitoa.


Mheshimiwa Mwenyekiti, Kinyerezi I, megawati 150, uwekezaji ni dola milioni 183. Kinyerezi II ambayo tutaweka jiwe la msingi mwezi huu, inahitaji dola za Marekani, milioni 344.


Hizo ni zaidi ya fedha za wafadhili. Kwa hiyo, tunachokitafuta sisi, ni fedha za uwekezaji, kwa hiyo, Watanzania msiwe na wasiwasi, fedha za wawekezaji zitapatikana. (Makofi)


Mheshimiwa Mwenyekiti, wengine wamesema Exim Bank ya China imekataa, siyo kweli. President Jinping alivyokuwa Afrika ya Kusini ametoa dola bilioni 60, kwa uhusiano wa China na Afrika. Tanzania ni kati ya nchi tatu ambazo zitafaidika. Nawaambia Wizara yangu yenyewe, mimi nataka…
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2015 na Mpango wa Maendeleo ya Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 – Wizara ya Fedha na Mipango
 
WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kabisa napenda kutoa pongezi kwa Waziri wa Fedha, Naibu na Wizara nzima ya Fedha kwa sababu wametengeneza bajeti ambayo ni ya mwaka mmoja lakini iko kwenye picha ya miaka mitano na iko kwenye picha ya dira yetu ya maendelea.


Mheshimiwa Naibu Spika, tunavyojadili hii bajeti usiichukue kama ni ya mwaka mmoja, lazima uone kwamba ni bajeti ambayo imeanza safari ya kwenda mwaka 2025.

Kwa hiyo ikiwa kweli tumedhamiria kuwa nchi ya kipato cha kati ifikapo mwaka 2025 inamaanisha bajeti yetu lazima inapanuka, inakuwa kubwa na fedha nyingi zinaenda kwenye maendeleo na siyo matumizi ya kawaida na ndiyo shukrani zangu nazitoa kwenye hii bajeti.


Mheshimiwa Naibu Spika, tumesema tunataka kuwa nchi ya kipato cha kati mwaka 2025 maana yake ni kwamba ukipiga hesabu, bajeti yetu sasa hivi ni vizuri nikiongea kwenye dola kwa sababu nalinganisha na nchi zingine, GDP yetu (Pato la Taifa) karibu kwenye bilioni 55, 56.


Kama tunataka kuwa nchi ya kipato cha kati, mwaka 2025 tunataka bajeti yetu ambayo itaonesha kwamba GDP per capita (pato la mtu mmoja) litakuwa la dola 3,000 inabidi tuizidishe mara nne. Kwa hiyo hii bajeti ni kubwa kwa sababu ifikapo mwaka 2025 tukiwa nchi ya kipato cha kati ni lazima tuwe na GDP ambayo ni zaidi ya bilioni 200 tuzidishe mara nne bajeti ya sasa hivi.



Mheshimiwa Naibu Spika, sasa basi engines ziko nyingi sana, engine za kupeleka vitu huko mbele huko na engine mojawapo ni umeme, na ndiyo maana bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini imekuwa kubwa ni ya shilingi trilioni 1.23 katika hiyo bajeti asilimia 94 zinaenda kwenye maendeleo na ukichukua kwenye maendeleo asilimia 98 inaenda kwenye umeme.

Hapo ndipo unajua bajeti ya Serikali iliyotayarishwa na Dkt. Mpango na wenzake imedhamiria kweli kutufikisha uko. Dalili za kusema kwamba fedha zinapatikana ni kweli zitapatikana, mwaka huu tunaomaliza mwezi huu, Wizara ya Nishati na Madini upande wa maedeleo tumeshapata asilimia 82 na REA - umeme vijijini tumeshapata asilimia 81.


Mheshimiwa Naibu Spika, bajeti yetu kwa hiyo ni kwamba umeme vijijini ndiyo itawatoa watu kwenye umaskini. Bajeti mliyoipitisha ya umeme vijijini imo ndani ya bajeti kubwa ya Serikali ambayo ni ya umeme vijijini shilingi bilioni 534.4, hii imeongezwa kwa asilimia 50 ya bajeti ya mwaka uliopita.


Lakini Waheshimiwa Wabunge na Watanzania ni kwamba kwa mara ya kwanza kwa historia ya nchii hii, na kuonesha hii Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kujenga nchi ya viwanda, ni kwamba umeme vijijini tutakuja kufikisha trilioni moja. Kwa sababu hii ni Serikali inayoaminika, hata wenzetu wanaopenda kutuchangia maendeleo na wao wanaweza wakachangia zaidi ya bilioni 500 na taarifa nitawapatia ndani ya wiki mbili kutoka sasa.



Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo hii bajeti inahakikisha umeme unapatikana, siyo umeme tu kusambaza, lakini hii bajeti ndiyo itatuhahakikishia kwamba vyanzo vyetu vyote tulivyonavyo vya umeme tunaanza kuzalisha umeme.


Tumejipanga kuzalisha umeme kutokana na gesi asilia, makaa ya mawe, maji, sola, upepo, joto ardhi, mawimbi (tides and waves) na mabaki ya mimiea (bio energies). Hayo yote yako kwenye hii bajeti ya trilioni 29.5, kwa hiyo ndugu zangu Wabunge tusipoipitisha hii, tukiwa na wasiwasi nayo basi haya yote ya umeme hayatakuwepo.


Mheshimiwa Naibu Spika, na hii bajeti uzuri wake ndiyo inakuja kutuhakikishia kwa mara ya kwanza kwa historia ya nchi hii haya mambo ya umeme ambao unakatikakatika hii bajeti ndiyo nakuja kutoa suluhisho la kudumu.


Tunajenga njia za kusafirisha umeme kutoka kilovoti 220 tunakwenda kilovoti 400.


Kwa hiyo, Waheshimiwa Wabunge, mimi ningependa kuzidi kuwashawishi kwamba hii bajeti siyo ya mwaka mmoja bali inaanza safari ya kutufikisha mwaka 2025 na kwenye hii bajeti ndiyo tumeweka miradi mingi ya usambazaji wa umeme na ni muhimu sana.


Waheshimiwa Wabunge wengi mmelalamika kwamba kuna vijiji vimerukwa. Hii bajeti ndiyo ina mradi wa kushusha transfoma na kusambaza nyaya kwenye vijiji ambavyo vimerukwa. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, Waheshimiwa Wabunge, mmesema hii sekta ya nishati haijashikwa vizuri sana na Watanzania. Hii bajeti ndiyoina fedha za kuwawezesha wazalishaji wadogo wa umeme na wao waweze kuchangia kwenye umeme wa Gridi ya Taifa.


Vilevile kwa upande wa kuboresha upatikanaji wa umeme, hii bajeti itatuwezesha kuibadilisha TANESCO kabisa itoke TANESCO ya zamani kuja TANESCO ya karne ya 21. TANESCO itakuwa na ushindani, lakini bajeti ya kubadilisha muundo, mfumo na utendaji unaolalamikiwa wa TANESCO uko kwenye hii bajeti.


Mheshimiwa Naibu Spika, tunaoenda huko kuanzia tarehe 1 Julai tunaweka taratibu za kisheria za kunyang‟anya TANESCO mamlaka ya yenyewe ndiyo inazalisha peke yake, ndiyo inauza umeme peke yake, ndiyo inasafirisha umeme peke yake.


Kwa hiyo, Waheshimiwa Wabunge, mimi nigependa bado kusisitiza kwamba ni muhimu sana hii bajeti tukaiunga mkono na isitoshe tumekuwa na sehemu tunaulizia ni kwamba kwa mfano wengine wamesema fedha za CAG, fedha za nani, ukweli ni kwamba bajeti hii acha ianze kufanya kazi na mahali ambapo tutakwama tutarudi tena hapa Bungeni kurekebisha.

Meshimiwa Naibu Spika na Waheshimiwa Wabunge, kwa hiyo hii bajeti ni muhimu na diyo itatufikisha mwaka 2025 ambapo GDP per capita yetu ambayo itatoka sasa hivi dola 945 GDP per capita mpaka
 

View: https://m.youtube.com/watch?v=vmklIZUtTPo

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mjadala wetu ni lazima kwanza tujue malengo yetu. Mipango tunayoifanya iko ndani ya mipango ya miaka mitano ambayo inaisha 2025, ambayo malengo yake ni ukuaji wa uchumi, upatikanaji wa ajira mpya na huduma bora kwa wananchi. Ndiyo maana kwa vyote hivi hatuwezi kukwepa pendekezo ambalo tumerudia mara kwa mara kulitoa, kwamba lazima tuwe na Planning Commission ambayo iko ndani ya Ofisi ya Rais.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa malengo yetu ambayo yako kwenye hiyo document inasema kwamba, ikifika mwaka 2025 tunataka GDP per capita yetu iwe dola 3000. Hiyo inamaanisha kwamba ikiwa sasahivi tuko watu takribani milioni 62, kufika 2025 huenda tutakuwa milioni 68 lakini tunaweza tukafika milioni 70. Maana yake ni kwamba ukichukua GDP per capita ya dola 3000 kwa kila mtu kwa mwaka, tukifika 2025, tunapaswa kuwa na GDP isiyopungua bilioni 200.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hivi GDP yetu ni dola bilioni 62. Kwa hiyo huu mpango na bajeti yake ni lazima ituweke kwenye barabara ya kutoka bilioni 62 sasa kwenda kwenye bilioni 200; ni kazi kubwa kweli kweli. Na hapa lazima mipango yetu tuelezane ukweli, tuone kama hilo lengo la GDP per capita ya dola 3000 lilikuwa sahihi au tuliandika tu kwa haraka haraka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sasa hivi sisi tukiwa na bilioni 62, GDP per capita yetu inakadiriwa mwishoni mwa mwaka kuwa dola 990. Kwa maneno mengine tumerudi chini, na hivyo tutaenda kwenye group la nchi masikini kufuatana na viwango vilivyowekwa na Benki ya Dunia tarehe moja Julai mwaka jana. Kwa hiyo tumeshuka, tusiongelee uchumi wa kati, hatuko huko tena, tumeshuka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati huohuo sisi tukiwa hivyo, wenzetu wa Kenya ikifika mwisho wa mwaka huu sisi tukiwa na GDP ya dola bilioni 62, wao watakuwa na GDP ya dola bilioni 107. GDP per capita ya Kenya, mwisho wa mwaka huu itakuwa ni dola 1,550, sisi tutakuwa ni dola 990. Kwa hiyo ukichukua yale ma-group yaliyotengenezwa na World Bank, Jirani yetu Kenya ambaye tunataka kumpatia na gesi yetu, yeye yuko kwenye Lower Middle-Income Country ambayo inaanzia dola 1046 mpaka dola 4095. Sisi tuko chini tuko dola 990, Kenya wapo dola 1,550. Kwa hiyo haya tunayoanza kuyajadili leo, mapendekezo yangu ni haya: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, malengo yetu ni lazima tupunguze mfumuko wa bei (low inflation), mipango na bajeti yetu. Inflation August mwaka huu ilikuwa 4.6%, Septemba imepanda imekuwa 4.8%. Hii lazima tuipunguze, ndiyo tuyajadili, tushawishi Wizara ipunguze. Lengo la pili muhimu kwenye mambo tunayoyapanga na bajeti yake na inafanyika duniani kote, wanapunguza low inflation halafu wanapunguza na interest rates. Ikiwa inflation itapanda inamaanisha benki nazo zitapandisha riba zao za mikopo. Kwa hiyo huu mpango na bajeti yake lazima tulenge huko kwamba interest rates zisipande, zikipanda hata waliokopa nyumba, baiskeli na magari lazima zipande.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine ambacho tunapaswa kukiongelea kwenye hii bajeti ni kuzuia Government Bonds (hatifungani) kutumika pasipokuwa na malengo sahihi. Maana yake ukiitumia, inflation ikiongezeka, utalazimika kutumia hii hatifungani. Ukishaitumia ujue sasa umeleta matatizo kwa uchumi wa nchi. Kwa hiyo hili nalo, hii bajeti ije itueleze namna ya kuzuia kukimbia kutumia Government Bonds, kututoa kwenye matatizo ambayo tungeweza kuyatatua kwa njia nyingine kabisa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile mipango tunayoijadili na uchumi wake, lazima ituelekeze ambapo wachumi wanatueleza. Unajua kuna wachumi wa aina mbili na inabidi uchague unapenda kumsikiliza nani. Kuna wale waliochukua econometrics kama akina marehemu Prof. Rweyemamu na kitabu chake cha miaka ya 1970; halafu kuna wale ambao ni political economist, hao maneno ni mengi na hesabu zao za kujumlisha na kutoa tu. Sasa inabidi sijui unataka kumsikiliza yupi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo ukichukua wataalamu wa uchumi kabisa wanasema duniani ukitaka kupunguza uchumi ni lazima uchumi wako ukue kwa zaidi ya 8%. Kwa hiyo hii mipango lazima itueleze, kwa sababu mwaka 2020 uchumi ulikua kwa 2%, mwaka jana kwa 4.5% na mwaka huu tunategemea kwenda kati ya 4% na 5%; na mimi takwimu zangu nazitoa kwenye vyanzo ambavyo dunia inaviamini. Unaweza kuwa na chanzo chako kama huko duniani hawakijui, sipendi kukitumia hicho.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa China, ukisikia China kufanikiwa kiuchumi, kwa zaidi ya miaka 20 uchumi wao ulikuwa kwa kadiri ya asilimia 15 mpaka asilimia 20; kwa miaka 20 ndipo China ikafika hapo ilipo. Sasa sisi tunataka tu tufike 8% growth. Kwa hiyo mapendekezo yangu ni kama haya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukuaji ili uende kasi, ndugu zangu lazima tuwe na bidhaa nyingi na mpya kwenye soko, siyo kuongeza tozo. Tozo na kodi hazikuzi uchumi. Kinachokuza uchumi ni bidhaa kwenda kwenye soko la ndani na soko la nje. Kwa hiyo hii bajeti, mipango yetu na bajeti, tueleze hivyo, halafu lazima itueleze ajira mpya. Hili neno mpya, siyo zilezile. Ajira mpya ni zipi na kiasi gani?

Mheshimiwa Mwenyekiti, itueleze mzunguko mkubwa na mpana wa fedha kwa wananchi wetu. Kwa hiyo, tufanye yafuatayo: mimi nina mapendekezo yangu kwa wataalamu kwamba twende kwenye kilimo, kwani kina asilimia 30 ya GDP yetu. Hebu tupigane tufikishe asilimia 40. Sasa sitaki kurudia, haya nilishayaongea. Mazao ambayo ni lazima tuyawekee mkazo ni yale ambayo tunatumia ndani ya nchi na nje ya nchi yana soko, ambayo ni mahindi, mchele, ngano, mihogo, matunda na mbogamboga. Haya yote matumizi yake duniani kila siku ni kati ya asilimia 40 na 60 ya watu waishio duniani, twende huko. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, uvuvi na ufugaji. Samaki watoke ziwani, watoke baharini, tuongeze nyama na maziwa. Hapa uvuvi na ufugaji tukazane tuchangie angalau 5% ya GDP yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tatu, madini. Tuendelee na Tanzanite, Gold na Diamond. Pia kama nilivyowahi kuwaeleza hapa, kuna madini ambayo ni muhimu na yana thamani kubwa kuliko haya. Haya ni lazima mipango na bajeti hii itueleze inavyoiwezesha geological survey. Haya madini yatapatikana kwa kutumia geological survey, siyo Tume ya Madini. Tume ya Madini inasimamia, sasa utasimamiaje huna kitu kipya? Tuwapatie geological survey waendelee kufanya utafiti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia tuna madini ya electronics industry, yanayotumika kwenye electronics kama Palladium, Lithium, Copper, Tin, Nickel, Gold na Aluminum. Computer zozote tulizonazo zina Lithium, Cerium, Europium, Samarium, Neodymium na madini mengine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna ugomvi mkubwa sasa hivi unaendelea wa microchips kati ya Marekani na China kama mnafuatilia. Kwa sababu hizi hata simu zenu zote zina microchips. Computers zote na electronics zote madini yanayotakiwa humo ni Sillicon na rare earth element 17, niliwahi kuyataja humu, sina haja ya kutaja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa haya madini, atakayetusaidia kuyapata ni geological Survey, wawekeze wafanye utafiti, watafute madini mapya yanayohitajika duniani, yanaitwa technology metals. Sasa hapa madini tujipige mpaka tufikishe asilimia 15 ya GDP; wanakaribia 10, lakini uchumi wetu uwasukume twende kwenye 15% of our GDP.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine ambacho ni muhimu na ukiona katika mapendekezo yangu nimeanza ajira ya watu wengi naenda napungua kilimo, uvuvi, ufugaji, mining na sasa uchumi wa gesi. Yote hayo yalitushinda tukadhani uchumi wa gesi, ndiyo utatutoa, lakini tukaamua kuweka kapuni. Sijui kama tutasalimika tusipotoa huko kapuni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kwamba uchumi wa gesi una vitu vitatu muhimu; tutazalisha umeme mwingi wa bei nafuu na ujenzi wa mitambo yake ni wa haraka. Halafu umeme wa gesi hauna jua, hauna ukame, tuta-export LNG tunayotaka kuijenga pale Lindi, ni biashara kubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tatu muhimu kabisa, ni petrochemical industrials. Hapa kabla hatujamuuzia mtu yeyote jirani yetu tunayeshindana naye gesi, lazima tujiulize: Je, tukimpa gesi yetu, atakuja na viwanda haraka atuuzie bidhaa zinazotokana na gesi yetu? Hilo ni suala la muhimu sana. Petrochemical industries mfano wake ni mbolea, plastics zote, viti vyote mnavyokalia, vyote ni gesi; sabuni, detergents nyingine, drugs, madawa ya wadudu, rangi na insulating materials. Viwanda ni vingi sana vya gesi. Kwa hiyo, napendekeza hapa hii gas economy ituchangie kati ya 15 na 20% ya GDP. Huu mpango…

MWENYEKITI: Profesa, hiyo ni kengele yako ya mwisho, nakuongeza dakika tatu.

MHE. PROF. SOSPETER M. MUHONGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Wewe Mwenyekiti ni mwema bwana. Nyingine ya tano ni tourism. Kufika Aprili mwaka huu 2022, tourism imeingiza dola bilioni 1.5. Sasa jamani, tujitahidi tourism tujitahidi ituletee 12% ya GDP yetu, hapo uchumi utakuwa mzuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sita, nimeandika, sports, games, music na culture vitupatie GDP mbili. Mwisho ni climate change. Tunataka kuiona hii bajeti inaongelea hili, maana yake matatizo yamekuwa mengi. Sasa hivi Carbon dioxide emission za Tanzania per Capita; tunavyochafua mazingira kwa kila mtu kwa mwaka. Kwa mwaka 2020 ilikuwa 0.18 metrics tons a person per annum. Mwaka 2019 ilikuwa 0.21 metric tons per person per annum.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tutengeneze mpango na tuje na bajeti. Ndiyo maana kwa kumalizia ni kwamba haya yote niliyoyataja hatuwezi kuruhusu Wizara moja inayapanga yote, mengine hayapo kwao ndiyo maana
 
Back
Top Bottom