TANESCO: Uwepo wa Kunguru ndiyo chanzo kikubwa cha umeme kukatika mara kwa mara katika wilaya ya Kinondoni

Kwani awamu hii Kutangaza MGAO ni zambi.?
 
Kunguru wametuchelewesha sana ndugu zangu....Five again.
 
Meneja Uhusiano wa TANESCO Johari Kachwamba, amesema kuwa uwepo wa Kunguru ndiyo chanzo kikubwa cha umeme kukatika mara kwa mara katika wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, kwani Kunguru hao wanachangia kuharibu miundombinu hususani nyaya za umeme.

Kauli hiyo ameitoa hii leo Januari 5, 2021, kwenye kipindi cha SupaBreakfast cha East Africa Radio, hii ni baada ya East Africa Radio kupokea malalamiko ya wananchi wengi kuhusu tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa mara katika maeneo yao hapa nchini.

"Kinondoni tuna tatizo la Kunguru kuathiri sana miundombinu yetu, tunatumia nyaya zenye magamba ya 'silver' ambazo zinaathirika sana na katika kutatua hili tumeanza kubadilisha nyaya, tunazoziweka sasa hivi hazitakuwa zinaathirika kiurahisi na Kunguru, ni tatizo linalotokea mara kwa mara na si sehemu ya tatizo kubwa ambalo tunaweza kusema watu wa Kinondoni wanashindwa kufanya kazi zao", amesema Johari

Aidha Johari ameongeza pia, "Uwepo wa Kunguru wengi wanaonyanyua nyaya kwenye madampo ya taka na kwenye viwanda vya nyaya vilivyoko maeneo mengi ya Kinondoni ikiwepo machinjio, inafanya Kunguru kutua kwenye nyaya za umeme wa msongo mkubwa (33KV na 11KV) na kusababisha milipuko kati ya waya na waya, pia wakitutua kwenye 'Transformer' husababisha milipuko na hizo nyaya wanazobeba kwa ajili ya kutengeneza viota vyao".

Akizungumzia kuhusu suala la gharama ya kuwekewa nguzo, Johari amesema kuwa, mwananchi hatakiwi kulipa gharama ya nguzo yoyote ya umeme, huku akiwasisitiza Watanzania kuacha kufanya shughuli za kibinadamu karibu na miundombinu ya umeme ili kutoiathiri.

Kunguru wa 2021 wana tofauti na wale wamika ya nyuma?
 
Mtu aliye shindwa kufanya mapenzi utamsikia akisema godoro lilikua linatereza otherwise yule demu angeipata.
 
Kwasababu hiyo naamini tutakuwa na nyaya za hovyo kuliko zote hapa duniani, zilizochakaa kupitiliza, hili shirika linajiendesha kwa nguvu za Mungu tu.
 
Jamaa linakwapua tu, kutapanya na kuchezeachea matrilion kwa mambo yasiyo kuwa na tija. Na kwa MAKSUDI kuporomosha uchumi wa nchi tena bila aibu.

Mtu wa ajabu sana
 
Nilimsikia jamaa mmoja akisema kuna agizo litatoka ikulu la kuwafanya mboga hawa viumbe ili kuwapunguza
 
Hao kunguru ni moja Kati ya kero za muungano wa Tanganyika na Zanzibar

Zanzibar waliagiza hao kunguru India kwa mradi wa kifisadi kuwa wanasaidia kusafisha mazingira zanzibar kwa kula takataka

Sasa wakazaliana kwa wingi wakahamia wengine bara bila makubaliano ya kimuungano kuwa waje huku

Zanzibar njooni muondoe kunguru wenu wanatuletea kero Tanzania bara na gharama za ku replace nyaya za umeme mlipe wenyewe

Baraza la wawakilishi itisheni kikazi cha dharura kujadili hawa kunguru wenu waliovamia barua bila kufuata prortocol za muungano tulizokubaliana
 
Meneja Uhusiano wa TANESCO Johari Kachwamba, amesema kuwa uwepo wa Kunguru ndiyo chanzo kikubwa cha umeme kukatika mara kwa mara katika wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, kwani Kunguru hao wanachangia kuharibu miundombinu hususani nyaya za umeme.

Kauli hiyo ameitoa hii leo Januari 5, 2021, kwenye kipindi cha SupaBreakfast cha East Africa Radio, hii ni baada ya East Africa Radio kupokea malalamiko ya wananchi wengi kuhusu tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa mara katika maeneo yao hapa nchini.

"Kinondoni tuna tatizo la Kunguru kuathiri sana miundombinu yetu, tunatumia nyaya zenye magamba ya 'silver' ambazo zinaathirika sana na katika kutatua hili tumeanza kubadilisha nyaya, tunazoziweka sasa hivi hazitakuwa zinaathirika kiurahisi na Kunguru, ni tatizo linalotokea mara kwa mara na si sehemu ya tatizo kubwa ambalo tunaweza kusema watu wa Kinondoni wanashindwa kufanya kazi zao", amesema Johari

Aidha Johari ameongeza pia, "Uwepo wa Kunguru wengi wanaonyanyua nyaya kwenye madampo ya taka na kwenye viwanda vya nyaya vilivyoko maeneo mengi ya Kinondoni ikiwepo machinjio, inafanya Kunguru kutua kwenye nyaya za umeme wa msongo mkubwa (33KV na 11KV) na kusababisha milipuko kati ya waya na waya, pia wakitutua kwenye 'Transformer' husababisha milipuko na hizo nyaya wanazobeba kwa ajili ya kutengeneza viota vyao".

Akizungumzia kuhusu suala la gharama ya kuwekewa nguzo, Johari amesema kuwa, mwananchi hatakiwi kulipa gharama ya nguzo yoyote ya umeme, huku akiwasisitiza Watanzania kuacha kufanya shughuli za kibinadamu karibu na miundombinu ya umeme ili kutoiathiri.

Hii inaitwa jambo limezua jambo, hawa kunguru si waliletwa kusafisha mji? Sasa wameanza kukata umeme!
 
Back
Top Bottom