TANESCO wamejieleza ila kwa chuki za baadhi yetu kwao sidhani kama tunawaelewa

Hii nchi ina viongozi wa ajabu sana, kila mwaka tunalalamika migao ya umeme inayosababishwa na ukame, wakati huo ukame unasababishwa na jua kali, ambalo jua lenyewe ni chanzo kingine cha umeme.

Ajabu tunaacha hilo tunakimbilia miradi ya umeme wa maji ambayo sio reliable, na gesi ambayo ni bei kubwa zaidi, huku kama sio kulogwa sijui ni kitu gani.
 
Wananchi wa Bumbuli wanasema hawataki maelezo maana hata wao kwenye tozo na kodi hawakusikilizwa
 
Wananchi hawana haja na maelezo, wanachotaka ni nishati ili kusudi anaeyechomelea chuma, kutengeneza icecream, kuweka juice kwenye friji, salon za kunyoa na kusuka nk, aendelee na kazi yake.
 
Exactly.
Yaani unabaki unashangaa yaani mtu analalamikia jua wakati ni chanzo cha nishati.
Kuna vitu vingine vya kijinga sana.
Tanzania ina watu wa ajabu sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…