TANESCO wanakulipisha hadi taka za nishati ya nguvu ya umeme.....chukua hatua!

TANESCO wanakulipisha hadi taka za nishati ya nguvu ya umeme.....chukua hatua!

Transistor

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2013
Posts
1,061
Reaction score
1,637
Ukiwa unatumia vifaa vya umeme, haijalishi kama umeme unaotumia unaenda katika uzalishaji halisi au upotevu—vyote utavilipia.

Hii ina maana kwamba Tanesco (kihalali) wanakulipisha:

1. Nguvu iliyotumika kukamilisha upatikanaji wa huduma yako, iwe mwanga, joto, kuwasha TV, n.k.


2. Nguvu iliyopotea kukamilisha mchakato wa kutumika kwa bidhaa ya umeme.

Mfano:

Ukiwa na TV, ili iwake na kukuhudumia, hulazimika ichakate nishati kukupa kile unachotaka.
Wakati inachakata nishati, husababisha upotevu wa baadhi ya nishati katika hali ya joto... (Here is where the technology of power processing of the device matters).

Hivyo, ule upotevu unaogeuzwa kuwa joto na sio picha ya TV, utaulipia. Sababu ni kwamba ni nishati iliyopotea. Kifupi, wewe umeupoteza kupitia vifaa vyako kulingana na teknolojia zake, hivyo utalipia.

Na ile huduma halisi ya TV ya kuona mapicha-picha (Real power), utailipia pia.

Kwa kisayansi, ina maana hivi:
In your electrical bill, you pay for both wasted energy and real energy.


My Take:

1. Usipende kuacha vitu katika hali ya "standby," kwani katika hali hiyo, vinaendelea kutumia umeme na kula fedha zako bila kufanya kazi halisi. You end up paying for energy with no positive or real output.


2. Pia, zingatia kutumia teknolojia ambazo hazina kiwango kikubwa cha wasted energy. They call it efficiency in power management.

TRANSISTOR!
 
Sio unafunga mivitu mwisho wake unagombana na Tanesco...ita wataalamu wakushauri....hahahah
 
Back
Top Bottom