Highlander
JF-Expert Member
- Feb 12, 2012
- 3,093
- 1,075
Jamani nipo eneo la Maji ya Chumvi Ubungo. Ni wapi? Ni jeshini Ubungo Kibangu. Hakuna Umeme siku nzima hapa, wakati maeneo mengine yote ya Ubungo yamekuwa na umeme leo hata kama kwa kuzimika na kuwaka baada ya muda mfupi. Hizi samaki kwenye mafriji inakuwaje? Saa hizi Ubungo yooote ina umeme, jeshini tu ndo hakuna umeme. Sisi wananchi tunaopakana na hili heshi giza totolo. Tukisema CCM inaajiri watu wabovu kwenye mashirika yetu ya Umma mnasema hoooo...tunageuza kila kitu kuwa cha kisiasa. Hili la kukosesha kambi ya kubwa namna hii ya jeshi umeme na raia waishio jirani limekaje jamani, wakati kwingine koooote umeme upo?