BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Maharage Chande amesema wanafuatilia malalamiko ya wateja wake ya kutofuatwa kwa ratiba ya mgawo wa umeme, wakiwemo wa Mkoa wa Kilimanjaro.
Kwa nyakati tofauti, wananchi wa maeneo mbalimbali nchini wamekuwa wakiulalamikia mwenendo wa ratiba ya mgawo wa umeme wakidai haifuatwi kama ilivyotolewa na shirika hilo, wakisema hatua hiyo inawaathiri kutopata huduma ya nishati hiyo.
Mgawo wa umeme nchini ulianza wiki iliyopita, huku Chande akisema hali hiyo imesababishwa na ukame, lakini mafundi wapo kazini kufanya ukarabati ili ikifika Januari kuwe kumetulia.
Chande ameeleza hayo leo Jumapili Novemba 27, 2022 wakati akizungumza masuala ya upatikanaji wa umeme na changamoto zake ikiwemo suala la mgawo katika mjadala wa ‘Twitter Space’ wenye mada ya ‘kumekucha na mkurugenzi mkuu wa Tanesco’.
Kabla ya kueleza hayo, baadhi ya wadau waliozungumza na kuandika ujumbe mfupi wakimtaka Chande aeleza kwa nini ratiba ya mgawo wa umeme haufuatwi kama ilivyotolewa na Tanesco.
Akisoma ujumbe wa wachangiaji mada mmoja wa waendesha mjadala huo, Mrusha Jones amesema, “Tanesco imekuwa ikitoa ratiba ya mgawo lakini kwa mkoa wa Kilimanjaro haijawahi kufuatwa kwa saa 24, jambo linalowafanya wasiamini taarifa kwa umma inayotolewa na Tanesco.”
Akijibu swali hilo, Chande amesema suala la Kilimanjaro limekuwa likijitokeza mara kwa mara katika kila mijadala anayoshiriki, huku akikiri kupokea ujumbe mfupi kuhusu changamoto hiyo.
Hata hivyo, amesema ameshaweka timu ya kufuatilia suala hilo tangu wiki iliyopita.
“Alhamisi ya wiki iliyopita tumebadilisha ratiba ili niweze kupata taarifa za Kilimanjaro, wanivumilie tuangalie kama ratiba inafuatwa, lakini malalamiko yamenifikia, tunafuatilia malalamiko ya watu hasa wanaosema ratiba haifuatwa,” amesema Chande.
MWANANCHI