TANESCO yaingia mkataba wa kukodi software kutoka India kwa USD 30M

TANESCO yaingia mkataba wa kukodi software kutoka India kwa USD 30M

Mwanafalsafa

Platinum Member
Joined
Jun 24, 2007
Posts
673
Reaction score
865
Watanzania naona tulisahau kabisa ajenda ya ufisadi wakati wa Magufuli, mpaka sasa kuna ufisadi umefanyika fasta fasta bila ya watu hata kushtuka.

Mkataba uliosainiwa baina ya Serikali ya Tanzania (kupitia TANESCO) na kampuni ya Tech Mahindra ya India wenye thamani ya dola milioni 30 ni wa kukodisha software ya Enterprise Resources Planning (ERP) - ambayo wahindi hawa wenyewe wanaiita Corporate Management System (CMS), kama inavyosomeka kwenye bango pichani chini.

Software ya aina hii huwa inaunganisha vitengo vyote vya taasisi katika software moja kwa ajili ya urahisi wa kuendesha taasisi. Hivyo basi kwa lugha nyingine ni kwamba Wahindi hawa watafunguliwa milango ya kuingia kila mahali ndani ya TANESCO, na hivyo kuwa na siri zote za mfumo wetu wa umeme.

Jambo kama hili ni hatari sana kwa usalama wa taifa. Hakuna njia rahisi ya kuiangusha nchi bila ya kufyatua hata kombora moja kama kuangusha mfumo wa nchi wa umeme.

Software kama hizi serikali inatakiwa iwawezeshe wataalam wa ndani kupitia Mamlaka ya Serikali Mtandao kutengeneza, kama vile mfumo wa malipo serikalini ulivyotengenezwa na wataalam wetu wa ndani kwa kuwezeshwa na serikali.

Zabuni ya kukodisha software hii ilianzaga kwenye dakika za lala salama za utawala wa Kikwete. Hivyo basi kitendo cha zabuni hii kukaa benchi kwa miaka mitano ya Magufuli kinaonesha kuwa hakuwa amekubaliana nayo. Baada ya Magufuli kufa naona wadau wa zabuni hii wameiendeleza na kuimwagia wino fasta, kama wanavyotaka kufanya kuhusu bandari ya Bagamoyo.

img-618a884f193e3.jpg
 
Nakumbuka naingia tu boarding form one kuna jamaa akanipa 500 nikamnunulie Bunsen burner kwenye duka la shule na chenji yake nimpelekee, aisee...!

Haya majina ya kitaalamu haya huwa yanawaingiza watu wengi sana Chaka.

Hatari sana...!
 
Waziri wa Energy kasomea Journalism, unategemea nini ? Ni kama Waziri wa Sheria awe fundi Mekanika unategemea Sheria kuboreshwa hapo ?

I mean Makamba hata ukimuuliza umeme ni nini na unasafiri vipi hajui unategemea atakuwa na vipaumbele gani ?

Si mnamuona online kila siku mara kwenye TV mara helikopta hicho ndicho alichosomea, Journalism.

I mean nchi isiyo na umeme tuna < 1500 MW unakwenda kutumia 30 million USD kwa ajili ya Software ?
 
Hili tatizo linaanzia kule juu kabisa, unapokuwa na kiongozi asietaka kushughulisha akili yake kwa chochote zaidi ya kusubiri kuletewa taarifa na wasaidizi wake huyo ndie chanzo.

Wasaidizi wake wanaweza kumpelekea mawazo ya hovyo yenye malengo ya "kutupiga", na kwasababu kiongozi mwenyewe hawezi kuhoji chochote anayakubali tu mawazo hayo kutokana na namna pumba anazolishwa zitakavyokuwa zimepangiliwa.

Matokeo yake ndio haya, unaona habari ya kukodi software ya $ 30 milion, baada ya kutoka kule kwenye mradi wa LNG ambao nao naamini alipigwa sound akaukubali bila kujua chochote, wala asijue hao anaowatuma ndio wajanja wenyewe, anachofanya Rais ni sawa na kumkabidhi fisi bucha sasa tunavuna tulichopanda.
 
Waziri wa Energy kasomea Journalism, unategemea nini ? Ni kama Waziri wa Sheria awe fundi Mekanika unategemea Sheria kuboreshwa hapo ?

I mean Makamba hata ukimuuliza umeme ni nini na unasafiri vipi hajui unategemea atakuwa na vipaumbele gani ?

Si mnamuona online kila siku mara kwenye TV mara helikopta hicho ndicho alichosomea, Journalism.

I mean nchi isiyo na umeme tuna < 1500 MW unakwenda kutumia 30 million USD kwa ajili ya Software ?
Dr Kalemani ni mwanasheria pia ujue. Kwenye suala la kupiga dili specializations huwa haziangaliwi.
 
Back
Top Bottom