TANESCO yaingia mkataba wa kukodi software kutoka India kwa USD 30M

Wataalamu waandike basi hiyo ERP itumike kwenye mashirika ya umma na pia tuuze nje ya nchi tuingize madola. Au wewe andika yako utajirike.
 
Kwahiyo shida kubwa ya Serikali yetu haipo kwenye kutokuwa na pesa ya kutosha, hapana, shida ipo kwenye matumizi ya hovyo bila kujali wala kushirikisha wananchi

Mungu atusaidie
 
Mikataba ya namna hii, hapana kwa kweli, dah , wangewekeza kwenye miundombinu kwanza
 
Halafu wanaposema ni ya kukodi kwanza hatuelewi wanamaanisha nini hasa

Kwenye software hakuna msamiati wa kukodi bali kuna kitu kinaitwa trial au free version

Kwamba kabla hujanunua unapewa bure (trial) uijaribu kwa kipindi fulani ikiwa na limitations kadhaa ambazo huondolewa unapoamua kununua premium package

Kwahiyo hawa Tanesco kama hawapewi software kamili wapo kwenye muda wa trial (kukodi) hawapaswi kulipa hela yoyote, wanatakiwa wapewe na waijaribu bure

Hakuna software unayopaswa kulipia chochote kwenye muda wa trial (kukodi)

Labda nieleweshwe vinginevyo
 
Naamini kwa sasa nchi iko uchi, safari nyingi hizi zinawapa watu nafasi ya kufanya watakavyo sbb hakuna mwenye uwezo wa kujua hayo!

Nilikoswa imani siku aliposema mie sina uwezo wa kukagua mabati, mbao,cement ama Matofari, wakauu wa mikoa nyie ndio muwe jicho langu!

Nyie ni watu wazima hakuna haja ya kufuatiliana, tayari nikajua gari limepata pancha hakuna safari hapo.
 
Mama yangu!!
Usisahau kupitia na hapa😁👇

 
Watalaamu wetu wana uwezo mkubwa wa kutengeneza software hizi kwa gharama ndogo sana. Mahakama na taasisi nyingi tu wametengenezewa software kama hizo za uendeshaji wa ki tekohama na watalaamu wetu. Lakini tanesco chini ya January wamekodi software hiyo kwa TSh 70 bilioni kwa mwezi bila kupitia utaratibu wa bunge kupitisha bajeti hiyo.
 
jiwe ule ujuaji wake wakati mwingine ulisaidia sana Taifa maana wasaidizi walijua lolote watakalompelekea atawa challenge tu
Mama hata mimi naweza kumdanganya,yeye kila kitu hukubali tu
 
hii issue inaniuma sana, kwanini tusiwaamini wataalamu wetu wa ndani? mbona mfumo wa GePG umetengenezwa hapa bongo na unafanya kazi vyema tu, hizo hela tungewapa wataalamu wetu wa ndani zingewasaidia sana katika kujiimarisha kimifumo na ujuzi mwengine ambao ungezidi kuliheshimisha taifa letu kwa kuwaongezea CV na hatimae wangepata hata kazi zingine kimataifa. Hata kama nao wangesource baadhi ya vipengele kwa wataalamu wa nje ni sawa tu, hata kwenye sekta nyingine vingi vishafanyika kama hivyo na mambo yameenda vyema tu

kuna mtu anasema eti System haitokuwa stable wataalamu wa ndani hakuna wanachojua, kwanza, system kuzingua ni kitu cha kawaida na ndio maana hata wenye investment kubwa kama mitandao kijamii huwa kuna muda system inacheza lakini wana-troubleshoot na mambo yanakuwa sawa.
 
Halafu wabunge wenye uchungu na nchi yao kama Mh Mpina wakiibua bungeni kasoro hizi wanaandamwa sana na akina Msukuma, halafu mambo yanazimwa kirahisi na spika. Ndugai hangalikubali yazimwe.
 
Katika hili Makamba amefeli, huwezi chukua mfumo kutoka india ukauleta TZ as if TZ hakuna wataalam
 
Unaenda kukodi application ya software ya bilioni 70 kutoka India kwa pesa za umma wakati nchi hii ni maskini?Mfano mdogo tu hiyo bilioni 70 angeinvest kuboresha Tanesco umeme usikatike katike hovyo au kununua nguzo za kutosha nchi nzima?Leo hii ukienda Tanesco kujaza na kulipia kuunganishiwa umeme kama ni mahali pa nguzo wanakuambia kabisa kwamba hakuna nguzo kuna uhaba!!!
 
IFM wanafundisha engineering?
 
IQ ya Mama ni ndogo sana, form four failure, kaingia CCM, kafanya yake kujiendeleza vicertificate, na kupanda ngazi uko kupitia mafisi wa kiume wa uko CCM, kajikuta yuko hapo. Ni majanga kwa taifa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…