Katika hali ya kushangaza, pamoja na nguvu kubwa anayotumia mheshimiwa rais inaonekana ni dhahiri kashindwa kudhibiti wafanya kazi hewa katika mashirika ya umma baada ya kubainika kuwa shirika la umeme nchini, TANESCO kukaidi amri ya rais na kuendelea kuwalipa watumishi hewa.
Chanzo cha habari cha kuaminika ndani ya shirika hilo kimethibitisha pasi na shaka kuwa meneja mwandamizi rasilimali watu anayefahamika kwa jina la Watson Mwakyusa ameendelea kuwalipa wafanyakazi hewa kuanzia January 2015 mpaka June 2016.
Mpaka tetesi hii ambayo inahitaji kufuatiliwa kwa karibu inatufikia, tayari kashalipotezea shirika zaidi ya milioni 40 mbali ya malipo ya NSSF na kodi, ambazo kwa makusudi kabisa kazilipa kwa wafanyakazi hewa. Iwapo atawalipa tena mwezi huu wa Julai, kiwango cha upotevu wa pesa kitazidi kuwa kikubwa zaidi.
Mpaka sasa haijajulikana kama yuko peke yake au yuko na viongozi wengine wa juu katika hili. Lakini unyamavu wao unaashiria kuwa wanawaweza kuwa pamoja naye katiki ubadhirifu huu au basi hawajajua hali ambayo inatafsiriwa kuwa ni uzembe wa hali yao na dharau kwa mheshimiwa rais.
Katika ufuatiliaji wa habari hii, imedhihirika wafanyakazi hewa wanaofaidika na ubadhirifu unaosemekana kutendwa na Bw. Mwakyusa wanatoka katika kanda ya pwani na Dar es Salaam.
Itakumbukwa kuwa ni meneja huyu huyu ambaye anayetuhumiwa kulitia hasara nyingine shirika hilo hilo la Tanesco ya zaidi ya shilingi bilioni 1 kwa kufukuza hovyo bila kufuata utaratibu wa kisheria wafanyakazi ambao wameweza kushinda kesi mahakamani na kulipwa kiasi hicho cha pesa.
Kwa kuwa TANESCO ni shirika la umma na linawaumiza sana wananchi kwa kutotoa huduma stahiki kwa wateja kwa visingizio vya ukosefu wa pesa za kutosha, tunaomba mheshiwa rais kupitia kwa waziri wake asiyekuwa na mzaha Profesa Muhongo afuatilie kwa haraka na umakini tetesi hizi ili kunusuru pesa zaidi zinazoendelea kupotea ikiwamo na kuwachukulia hatua kali watakaobainika wanashirikiana na huyu meneja katika kuliumiza taifa. Ni katika uchunguz huo ukweli utajulikana.