TANESCO yang’ara tuzo za umahiri wa mawasiliano kwa umma

TANESCO yang’ara tuzo za umahiri wa mawasiliano kwa umma

TANESCO

Official Account
Joined
Jul 12, 2014
Posts
5,210
Reaction score
2,779
WhatsApp Image 2026-10-09 at 14.37.30.jpeg

📌 Yanyakua tuzo nne katika vipengele mbalimbali

📌 Yatambuliwa kwa ubora katika mawasiliano ya kimkakati, elimu kwa umma na usimamizi wa mawasiliano wakati wa migogoro

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limefanikiwa kutwaa tuzo nne za umahiri katika mawasiliano kwa umma, ikiwa ni kutambua mchango wake katika kuboresha eneo la utoaji wa taarifa, kuimarisha mawasiliano ya kimkakati na kutumia ubunifu katika kuwafikishia wananchi taarifa kwa ufanisi.

Akizungumza Kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Bw Lazaro Twange mara baada ya kupokea tuzo hizo leo Oktoba 8, 2026, katika Mkutano wa Mwaka wa Chama cha Maafisa Uhusiano na Mawasiliano Tanzania (PRST), Mkurugenzi wa Mawasiliano na Huduma kwa Wateja wa TANESCO, Bi. Irene Gowelle, amesema mafanikio hayo ni heshima kubwa kwa Shirika na chachu ya kuendelea kubuni njia bora za mawasiliano pamoja na kuimarisha matumizi ya mifumo ya kidijitali katika utoaji wa huduma kwa wananchi.

Amesema TANESCO itaendelea kutumia teknolojia na majukwaa ya kidijitali kuhakikisha wananchi wanapata taarifa sahihi, kwa wakati na kwa njia rahisi, za kisasa na zenye ufanisi.

“Kwanza naishukuru sana PRST kwa kutambua mchango wa TANESCO katika mawasiliano kwa umma. Mafanikio haya yametokana na ushirikiano mkubwa tunaoupata kutoka Wizara ya Nishati, Bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti ya TANESCO. Tunamshukuru pia Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwekeza katika sekta ya umeme kwa kuimarisha miundombinu ya upatikanaji wa umeme na matumizi ya teknolojia zinazotusogeza karibu zaidi kwenye kuwahudumia wananchi,” amesema Bi. Gowelle.

WhatsApp Image 2026-10-09 at 14.37.29 (2).jpeg


Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi. Savera Kazaura, aliyemwakilisha Waziri wa Wizara hiyo, ameipongeza TANESCO kwa mafanikio hayo na kwa hatua kubwa iliyopiga katika kuboresha utoaji wa taarifa kwa wananchi, hususan wakati wa changamoto za huduma ya umeme.

Amesema taasisi za umma zinapaswa kuendelea kuwekeza katika mawasiliano ili kuongeza uelewa kwa wananchi na kuimarisha uhusiano kati ya serikali na jamii.

“Nawapongeza sana TANESCO kwa mafanikio haya. Shirika limeonyesha mabadiliko makubwa katika utoaji wa taarifa kwa wananchi kuhusu changamoto za umeme zinapojitokeza. Jitihada hizi zinapaswa kuendelezwa ili kuongeza imani ya wananchi na kuboresha zaidi utoaji wa huduma,” amesema Bi. Kazaura.

WhatsApp Image 2026-10-09 at 14.37.29 (1).jpeg


Katika tuzo hizo zilizoandaliwa na PRST, TANESCO ilitunukiwa Tuzo ya Ubora katika Usimamizi wa Mawasiliano wakati wa Migogoro (Crisis Communication Management), Tuzo ya Ubora katika Kampeni ya Elimu kwa Umma (Public Awareness Campaign) kupitia kampeni ya Nishati Safi ya pika kwa Umeme, pamoja na Tuzo ya Idara Bora ya Uhusiano na Mawasiliano kwa Umma (Best Public Relations Department).

Aidha, Bi. Irene Gowelle alitangazwa mshindi wa Tuzo ya Mtaalamu Bora wa Uhusiano na Mawasiliano kwa Umma Tanzania kwa mwaka 2026 (Best PR Practitioner 2026).

Tuzo hizo hufanyika kila mwaka zikilenga kuonesha mchango wa mawasiliano kwenye kuimarisha sekta mbalimbali na namna zinaongeza tija kwa wataalamu wa mawasiliano nchini.​

WhatsApp Image 2026-10-09 at 14.37.31.jpeg
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2026-10-09 at 14.37.28 (1).jpeg
    WhatsApp Image 2026-10-09 at 14.37.28 (1).jpeg
    333 KB · Views: 10
  • WhatsApp Image 2026-10-09 at 14.37.28 (2).jpeg
    WhatsApp Image 2026-10-09 at 14.37.28 (2).jpeg
    310.7 KB · Views: 9
  • WhatsApp Image 2026-10-09 at 14.37.29.jpeg
    WhatsApp Image 2026-10-09 at 14.37.29.jpeg
    409.5 KB · Views: 11
  • WhatsApp Image 2026-10-09 at 14.37.30 (1).jpeg
    WhatsApp Image 2026-10-09 at 14.37.30 (1).jpeg
    86.9 KB · Views: 10
Namuona RCRO wangu ni mviiiiiivu
 
Mteja anaweza kutengeneza nguzo zake kwa specification za TANESCO? Ili kupunguza gharama za Nguzo?

Jisajiri kwenye Forum yetu mtu... inayofanana na JF - Pata miradi na wezesha miradi yako sasa

 
Pamoja na matuzo yenu hayo, Umeme Wilaya ya Chunya ni shida.
 
kusambaza umeme mmeshindwa mnachukua tuzo za kutoa taarifa za kukata umeme magroup ya whatsapp,,,
huu umeme uko na shida gani kwani?
ndani ya wiki kuupata siku 2 mfululizo ni mtihani....,
 
Pamoja na matuzo yenu hayo, Umeme Wilaya ya Chunya ni shida.
Habari Blue Bahari, asante kwa kuwasiliana nasi na pole kwa changamoto hiyo.

Tafadhali tupatie namba yako ya simu pamoja na taarifa kamili za eneo unalopatikana ikiwemo Kata na Mtaa/Kijiji ili tuweze kukupatia msaada zaidi.

Asante.^FL
 
kusambaza umeme mmeshindwa mnachukua tuzo za kutoa taarifa za kukata umeme magroup ya whatsapp,,,
huu umeme uko na shida gani kwani?
ndani ya wiki kuupata siku 2 mfululizo ni mtihani....,
Habari SankaraBoukaka, asante kwa kuwasiliana nasi na pole kwa changamoto hiyo.

Tafadhali tupatie namba yako ya simu pamoja na taarifa kamili za eneo unalopatikana, ikiwemo Mkoa, Wilaya, Kata, na Mtaa/Kijiji ili tuweze kukupatia msaada zaidi. ^FL
 
Habari SankaraBoukaka, asante kwa kuwasiliana nasi na pole kwa changamoto hiyo.

Tafadhali tupatie namba yako ya simu pamoja na taarifa kamili za eneo unalopatikana, ikiwemo Mkoa, Wilaya, Kata, na Mtaa/Kijiji ili tuweze kukupatia msaada zaidi. ^FL
Mteja anaweza kutengeneza nguzo zake kwa specification za TANESCO? Ili kupunguza gharama za Nguzo?

Jisajiri kwenye Forum yetu mtu... inayofanana na JF - Pata miradi na wezesha miradi yako sasa

https://www.city-data.com/forum/
 
Habari Blue Bahari, asante kwa kuwasiliana nasi na pole kwa changamoto hiyo.

Tafadhali tupatie namba yako ya simu pamoja na taarifa kamili za eneo unalopatikana ikiwemo Kata na Mtaa/Kijiji ili tuweze kukupatia msaada zaidi.

Asante.^FL
Nasema umeme Wilaya yote ya Chunya ni shida tupu, Siyo eneo nililopo Tu. Mathalani:
  • Umeme ukiwepo unakuwa na low voltage. Wenye Mashine za kusaga nafaka, makarasha, na plants wanapata Sana tabu. Uchumi wao unadumaa sababu ya kadhia hii ya low voltage.
  • Umeme Kukatika kila siku
  • Umeme Ukiwepo, kila bàada ya dakika chache unakata ghafla na kurudi. Kila Muda unawaka unakata, Unawaka unakata.
  • Kila siku wakandarasi Wako saiti wanarekebisha hiki mara wanarekebisha kile.
  • Kila siku wananchi wanapewa matumaini hewa, kwamba: "Si Muda mrefu mambo yatakuwa shwari". Hii Ni kauli ya miaka nenda Rudi.
 
Mteja anaweza kutengeneza nguzo zake kwa specification za TANESCO? Ili kupunguza gharama za Nguzo?

Jisajiri kwenye Forum yetu mtu... inayofanana na JF - Pata miradi na wezesha miradi yako sasa

https://www.city-data.com/forum/
Habari, ndugu mteja.

Tafadhali fahamu kuwa nguzo ni mali ya TANESCO na haziuzwi kwa wateja. Malipo yanayofanyika ni kwa ajili ya huduma ya kuunganishiwa umeme, ambayo inaweza kujumuisha uwekaji wa nguzo kulingana na mahitaji na tathmini ya eneo husika.

Kwa masuala yanayohusu miundombinu na vifaa vya umeme, tunawashauri wateja wetu kutembelea ofisi za TANESCO zilizo karibu ili kupata taarifa na mwongozo sahihi, na kuepuka mkanganyiko wowote.

Asante. ^HN
 
Nasema umeme Wilaya yote ya Chunya ni shida tupu, Siyo eneo nililopo Tu. Mathalani:
  • Umeme ukiwepo unakuwa na low voltage. Wenye Mashine za kusaga nafaka, makarasha, na plants wanapata Sana tabu. Uchumi wao unadumaa sababu ya kadhia hii ya low voltage.
  • Umeme Kukatika kila siku
  • Umeme Ukiwepo, kila bàada ya dakika chache unakata ghafla na kurudi. Kila Muda unawaka unakata, Unawaka unakata.
  • Kila siku wakandarasi Wako saiti wanarekebisha hiki mara wanarekebisha kile.
  • Kila siku wananchi wanapewa matumaini hewa, kwamba: "Si Muda mrefu mambo yatakuwa shwari". Hii Ni kauli ya miaka nenda Rudi.
Habari, ndugu mteja. Pole sana kwa changamoto ya umeme unayokumbana nayo. Hili suala tulishaitolea ufafanuzi.

Kama tulivyofafanua awali, TANESCO inatambua changamoto ya umeme mdogo (low voltage) inayowakabili baadhi ya wateja katika Wilaya za Chunya na Mkwajuni.

Tafadhali fahamu kuwa Serikali kupitia TANESCO imechukua hatua za kukabiliana na changamoto hii. Tarehe 11 Septemba 2026, mkataba wa ujenzi wa miundombinu muhimu ya umeme ulisainiwa, ukiwa na lengo la kuimarisha upatikanaji na ubora wa huduma katika maeneo husika.

Mradi huo, wenye thamani ya TSh bilioni 109, unahusisha ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme ya msongo wa kilovolti 220 (220kV), yenye urefu wa takribani kilomita 122 kutoka Iganjo, Mbeya hadi Saza, Mkwajuni. Aidha, utajumuisha kituo cha kupozea umeme chenye uwezo wa 100MVA (takribani MW 80).

Mradi unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 18, na utasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza changamoto za umeme mdogo, kuongeza uwezo wa miundombinu na kuboresha upatikanaji wa huduma kwa wateja.

Tunaomba muendelee kuwa na uvumilivu wakati utekelezaji wa mradi huu ukiendelea.

Asante. ^HN​
 
Habari, ndugu mteja.

Tafadhali fahamu kuwa nguzo ni mali ya TANESCO na haziuzwi kwa wateja. Malipo yanayofanyika ni kwa ajili ya huduma ya kuunganishiwa umeme, ambayo inaweza kujumuisha uwekaji wa nguzo kulingana na mahitaji na tathmini ya eneo husika.

Kwa masuala yanayohusu miundombinu na vifaa vya umeme, tunawashauri wateja wetu kutembelea ofisi za TANESCO zilizo karibu ili kupata taarifa na mwongozo sahihi, na kuepuka mkanganyiko wowote.

Asante. ^HN

Hongera TaNESCO kwa kuenga Magufuli City..​

​

Mapungufu​

Jiji la Magufuli, lililopo eneo la Ihumwa, Dodoma, ni mradi wa Serikali unaolenga kukusanya wizara na shughuli mbalimbali za serikali katika eneo moja. Mradi huu una ukubwa wa zaidi ya hekta 617 na ulikuwa bado unaendelea kujengwa kwa sehemu mwaka 2024.




Yafuatayo ni mapungufu na changamoto zinazoweza kuikabili Magufuli City, kwa kuzingatia taarifa zilizopo kuhusu mradi na mahitaji ya kuendesha mji mpya.

1.​

  • Ujenzi wa miundombinu, majengo ya serikali, barabara na huduma za jamii unahitaji fedha nyingi.
  • Fedha nyingi zinapotumika kwenye mradi mmoja, kuna haja ya kuhakikisha miradi mingine ya afya, elimu na maji nayo inapata rasilimali za kutosha.
  • Gharama za matengenezo ya majengo na miundombinu zinaweza kuwa mzigo kwa Serikali kwa muda mrefu.

2.​

  • Magufuli City iko takribani kilomita 17 kutoka katikati ya jiji la Dodoma.
  • Umbali huo unaweza kuongeza gharama za usafiri kwa wafanyakazi, wananchi wanaofuatilia huduma za serikali na wageni.
  • Usafiri wa umma usipokuwa wa kutosha, wananchi wanaweza kutumia muda mwingi kufika kwenye ofisi za serikali.

3.​

  • Mji unahitaji maji ya uhakika kwa matumizi ya ofisi, makazi na huduma nyingine.
  • Mfumo wa majitaka lazima ujengwe na kuendeshwa kwa ufanisi ili kuzuia uchafuzi wa mazingira.
  • Juni 2026, DUWASA ilitangaza mradi wa kuondoa na kutibu majitaka ya Magufuli City, jambo linaloonyesha umuhimu wa kuendeleza miundombinu hiyo.

    DUWASA

4.​

  • Baadhi ya majengo na maeneo ya mradi yalikuwa bado katika hatua za ujenzi mwaka 2024.
  • Ujenzi usipokamilika kwa wakati unaweza kuchelewesha matumizi kamili ya miundombinu na huduma zilizopangwa.

    The Citizen

5.​

  • Ujenzi wa eneo kubwa unaweza kuondoa uoto wa asili na kuathiri makazi ya viumbe.
  • Ongezeko la magari na shughuli za ujenzi linaweza kuongeza uchafuzi wa hewa na kelele.
  • Mji unahitaji mifumo bora ya kuhifadhi maji, kutibu majitaka na kusimamia taka ngumu.

6.​

  • Mji mpya unahitaji hospitali, shule, masoko, maeneo ya biashara na huduma za dharura.
  • Huduma hizo zisipoendelezwa sambamba na majengo ya ofisi, wafanyakazi na wakazi wanaweza kulazimika kwenda maeneo mengine kwa mahitaji ya kila siku.

7.​

  • Uwekezaji mkubwa hauhakikishi moja kwa moja kuwa wananchi wote wa maeneo jirani watanufaika kiuchumi.
  • Kuna haja ya kuweka mazingira yatakayowezesha vijana na wafanyabiashara wadogo kupata ajira, zabuni na fursa za biashara.

8. Matumizi ya miundombinu kwa ufanisi​

  • Majengo yasiyotumika kikamilifu yanaweza kuongeza gharama za ulinzi, usafi na matengenezo.
  • Ni muhimu kuhakikisha kuwa taasisi za serikali zinahamia na kutumia majengo yaliyokamilika kulingana na mpango.

Hitimisho​

Kwa ujumla, changamoto kuu zinazoweza kujitokeza katika Magufuli City ni gharama kubwa za ujenzi, umbali kutoka katikati ya Dodoma, mahitaji ya maji na majitaka, athari za mazingira, huduma za jamii na matumizi bora ya miundombinu.

Ni taasisi pekee inayoangaza maisha ya watanzania
 

Aksante Tanesco kwa ujenzi wa mradi huu kawe​

​

Ushahidi maalumu kuhusu changamoto za Samia Housing Scheme – Kawe​

Kwa taarifa rasmi za NHC, awamu ya kwanza ya Samia Housing Scheme – Kawe ina nyumba 560 na imeorodheshwa kuwa imekamilika. NHC pia imetangaza bei ya kuanzia TSh milioni 38, lakini bei hutegemea aina ya nyumba na taarifa ya sasa ya mauzo inapaswa kuthibitishwa.

NHC Projects


Changamoto muhimu ya kuichunguza ni ikiwa nyumba hizo zinamudu kweli watumishi wa kipato cha chini na cha kati. Makala ya The Citizen ya mwaka 2026 imeibua mjadala kuhusu gharama za baadhi ya miradi ya makazi ya NHC na kama inawanufaisha walengwa wenye uhitaji mkubwa wa nyumba nafuu. Huu ni mjadala wa sera na uwezo wa kumudu nyumba, si uthibitisho kwamba kila nyumba ya Kawe ina kasoro.

The Citizen


5. Changamoto ya usimamizi wa nyumba baada ya mauzo​

Taarifa ya Mei 2026 kuhusu Samia Housing Scheme – Kawe ilieleza kuwa NHC ilitoa elimu kwa wamiliki kuhusu mfumo wa hati pacha na kuhimiza kuundwa kwa umoja wa wamiliki. Pia ilisisitiza umuhimu wa kulipa service charge kwa ajili ya lifti, ulinzi, usafi na matengenezo ya maeneo ya pamoja. Hili linaonyesha kuwa usimamizi wa pamoja na gharama za uendeshaji ni masuala muhimu yanayopaswa kuchunguzwa, ingawa taarifa hiyo haithibitishi kuwa huduma hizo zilikuwa na hitilafu.

GREEN WAVES MEDIA


Hitimisho​

Mapungufu yanayoweza kuchunguzwa katika Samia Housing Scheme – Kawe ni:

  • Uwezo wa watumishi wa kipato cha chini na cha kati kumudu bei za nyumba.
  • Gharama za huduma za pamoja na matengenezo.
  • Upatikanaji na ufanisi wa miundombinu na huduma za makazi.
  • Uelewa wa wanunuzi kuhusu hati pacha na wajibu wa wamiliki.
  • Uendelevu wa usimamizi wa majengo baada ya mauzo.
 
Habari, ndugu mteja.

Tafadhali fahamu kuwa nguzo ni mali ya TANESCO na haziuzwi kwa wateja. Malipo yanayofanyika ni kwa ajili ya huduma ya kuunganishiwa umeme, ambayo inaweza kujumuisha uwekaji wa nguzo kulingana na mahitaji na tathmini ya eneo husika.

Kwa masuala yanayohusu miundombinu na vifaa vya umeme, tunawashauri wateja wetu kutembelea ofisi za TANESCO zilizo karibu ili kupata taarifa na mwongozo sahihi, na kuepuka mkanganyiko wowote.

Asante. ^HN
Tule tumatusi wakati wa kubebeba NGUZO bado tupo? Tunajenga sana Taifa letu... Big up Mali ya Tanesco
 
Tule tumatusi wakati wa kubebeba NGUZO bado tupo? Tunajenga sana Taifa letu... Big up Mali ya Tanesco
Habari, ndugu mteja. Hatujakuelewa. Unamaanisha nini kwa msaada zaidi?
 
Back
Top Bottom