TANESCO yasaini mkataba wa kuzalisha Umeme Jua MW 150 Kwa Bilioni 275. Waziri Makamba apiga marufuku mauziano ya Umeme kwa Dola

Diversification mfano gesi tunaitegemea kwa umeme 70% hivi umewahi jiuliza siku ikitokea hitilafu kwenye Bomba la gesi au pale Kinyerezi 1 and 2 si nchi nzima tutakaa gizani miezi kibao. Ila ukiwa na energy mix inasaidia ku complement Bwawa la Nyerere na Gesi
 
Gharama za kuzalisha umeme wa jua ni kubwa ukilinganisha na gharama za kuzalisha umeme wa maji. Huu u.eme wa jua / upepo ni miradi ya kifisadi
Kakono.hydro 14 mgwt gharama Dola mil.100
Kishapu solar 150 megawatt gharama bil.275

 
Umemjibu kwa akili kubwa sana. Hizo Panel za Kichina zikimaliza mwaka nendeni mkatambike yani. Baada ya miezi 12 zoote zitahitaji repair ya 270Bil
Hiyo ni hasara ya mkandarasi sio Tanesco
 
Inaweza mbona, kamamna water fall yenye uwezo wa kuzungusha turbine yenye kufua kiwango hko cha umeme
Taja hiyo sehemu,kwanza mnajua gharama za bwawa la Nyerere Dola bil.3.5 ni Nje ya gharama zingine za miundombinu,njia za kusafirisha umeme nk?
 
 
Ni mpango mzuri hasa kwa hilo lengo la chanzo mbadala badala ya kutegemea maji ambayo wakati fulani kuna ukame.

Tunahitaji ubunifu Ili umeme uwe unapatikana kwa urahisi,uhakika na unafuu. Hii ni hatua nzuri. Makamba ni kiongozi mbunifu. Kipindi alipokuwa Wizara ya Mawasiliano tulipata vifurushi na bando kwa bei nafuu baada ya kuwakomalia wamiiki wa makampuni ya Simu.
 
Huo sio mradi wa nchi, ni mradi binafsi
 
Waziri Makamba katika hili amefanya jambo kubwa lenye kustahili pongezi. Kuwa na sera katika eneo la uzalishaji wa umeme kwa kutumia nishati jadidifu ni kitu cha msingi sana kwa wakati huu, hasa ikizingatia nchi yetu ipo katika ukanda wa kijografia wa kitropiki, basi hata uvunaji wa nishati hii utakuwa na ufanisi mkubwa sana. "Waziri Makamba amesema kuwa, ili kuongeza zaidi uzalishaji wa umeme kwa kutumia nishati jadidifu, Serikali inakuja na Sera mpya ya Nishati Jadidifu (iko kwenye maandalizi) ambayo itasaidia nchi kuongeza uwekezaji kwenye eneo hilo kwani fedha nyingi duniani, masoko ya mitaji na teknolojia mpya zinajielekeza kwenye nishati jadidifu"
 
Kiukweli umeme wa maji ni janga kwenye hili la umeme wa Jua kama siyo siasa Waziri apewe maua yake.
275 billion ni hela ndogo
Kuna vitu viwili sijui kama umeviwaza
1) Tanesco itanunua umeme kutoka kwa mwekezaji, Kama ilivyokua inanunua kwa iptl
2) gharama ya mradi, bil 270 ni hela ndogo je ni kwa megawatt ngapi? Usidhani ni kwa megawatt 1000
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…