TANESCO yasaini mkataba wa kuzalisha Umeme Jua MW 150 Kwa Bilioni 275. Waziri Makamba apiga marufuku mauziano ya Umeme kwa Dola

TANESCO yasaini mkataba wa kuzalisha Umeme Jua MW 150 Kwa Bilioni 275. Waziri Makamba apiga marufuku mauziano ya Umeme kwa Dola

Serikali Kupitia Tanesco imeandika Historia ya kusaini mkataba wa Kuzalisha Umeme wa Juna na kampuni ya China wenye thamani ya Shilingi Bilioni 275 ambao utazalisha megawatt 150 Kishapu ,Shinyanga na Kwa awamu ya kwanza Wataanza na megawatt 50.

Waziri wa Nishati January Makamba akishuhudia mkataba huo amepiga marufuku Tanesco kununua Umeme kutoka Kwa wazalishaji Kwa malipo ya dola badala yake Shilingi ndio ittumika..


Aidha amewataka Tanesco kuwawezesha wazawa Ili waweze kuzalisha umeme akisema hakuna maajabu Hadi wao washindwe..


My Take
Hongera sana Makamba,majungu achilia failures wewe endelea kuchapa kazi.

=======


Wizara ya Nishati kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) imesaini mkataba wa kwanza wa uzalishaji wa umeme Jua wa kiasi cha megawati 50 utakaotekelezwa wilayani Kishapu mkoani Shinyanga.

Mkataba huo umesainiwa tarehe 29 Mei, 2023 jijini Dodoma na kushuhudiwa na Waziri wa Nishati, Mhe.January Makamba ambaye alikuwa mgeni rasmi.

Kwa ujumla mradi huo wa umeme wa Jua ni wa megawati 150 ambapo awamu kwanza itajengwa mitambo itakayozalisha megawati 50 na awamu ya pili itajengwa mitambo ya megawati 100 kwa jumla ya shilingi bilioni 275. Utekelezaji wa mradi wa Awamu ya kwanza hautazidi miezi 12.

Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri wa Nishati amesema kuwa “kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi tunaingiza umeme wa Jua katika gridi ya Taifa, nimpomgeze Rais wetu kwa kwa muongozo na uongozi ambao umepelekea nchi kuaminiwa na washirika wa maendeleo ikiwemo Shirika la Maendeleo la Ufaransa ambalo limetoa mkopo ambao utatekeleza mradi huu.”

Ameeleza kuwa, utekelezaji wa mradi huo wa Jua ni jitihada za Serikali za kuhakikisha inatengeneza mchanganyiko wa umeme wenye afya katika gridi ya Taifa ambao utatokana na vyanzo mbalimbali kama vile maji, gesi, upepo na Jua ili hata pale chanzo moja kinapotetereka, vyanzo vingine vitaendelea kuzalisha umeme.

Waziri Makamba amesema kuwa, ili kuongeza zaidi uzalishaji wa umeme kwa kutumia nishati jadidifu, Serikali inakuja na Sera mpya ya Nishati Jadidifu (iko kwenye maandalizi) ambayo itasaidia nchi kuongeza uwekezaji kwenye eneo hilo kwani fedha nyingi duniani, masoko ya mitaji na teknolojia mpya zinajielekeza kwenye nishati jadidifu.

Ameongeza kuwa, kwa sasa kazi inayofanyika pia ni kuainisha maeneo yaliyo na rasilimali ya nishati jadidifu na kipaumbele kitakuwa kwa wazawa kuwekeza kwenye miradi kama ya Upepo na Jua na Serikali itawaunga mkono na kwamba Serikali itakuja na muongozo wa utekelezaji wa suala hilo.

Ameongeza kuwa, kwa maeneo yaliyo nje ya gridi kama vile visiwa, bado Serikali itaendelea kuwezesha jitihada za kupelewa umeme kwa kutumia miradi ya nishati jadidifu kama vile Jua na Upepo.

Poa
 
Waziri Makamba katika hili amefanya jambo kubwa lenye kustahili pongezi. Kuwa na sera katika eneo la uzalishaji wa umeme kwa kutumia nishati jadidifu ni kitu cha msingi sana kwa wakati huu, hasa ikizingatia nchi yetu ipo katika ukanda wa kijografia wa kitropiki, basi hata uvunaji wa nishati hii utakuwa na ufanisi mkubwa sana."Waziri Makamba amesema kuwa, ili kuongeza zaidi uzalishaji wa umeme kwa kutumia nishati jadidifu, Serikali inakuja na Sera mpya ya Nishati Jadidifu (iko kwenye maandalizi) ambayo itasaidia nchi kuongeza uwekezaji kwenye eneo hilo kwani fedha nyingi duniani, masoko ya mitaji na teknolojia mpya zinajielekeza kwenye nishati jadidifu"
Ujerumani wanatumia huu umeme wa upepo, nchi nzima imejaa hayo makata upepo. Na sisi tunao mwingi maeneo ya Singida kuelekea Arusha.

Afrika kwa ujumla ni tajiri sana, na mzungu anatuzidi kwa hujuma nyingi anazopenyeza katika hizi nchi.
 
Weka hapo ug wanazalisha megawat ngapi? Na kwa hizo us d

Manake solar 215 tsh bilion

Miradi yore pia ya mama na mwanae
Twende lazi
Toa upuuzi wako,huo ni mradi wa pamoja na megawatt ndio hizo 14 Kwa Zaidi ya bil.250

Hivyo hivyo ukienda Rusumo Falls Kuna mradi gharama ni kubwa kama zote
 
Unadhani mgt 2100 ni nyingi Kwa viwanda vikubwa? Kuna viwanda vya kuzalisha vyuma vinahitaji mgt 3500 kwa nchi kama ya kwetu ili tuwe na viwanda vikubwa tuwe na mgt 10000 mpaka 35000 ndiyo tutaweza hata kuuza umeme mkubwa
Nani amekwambia ni nyingi na issue sio viwanda tu hata sasa hivi raia hawapati umeme wa gharama nafuu wakati tuna vyanzo lukuki..., sasa kukimbilia na kuanza kuwaza mg 5000 wakati 2500 bado na unaongelea viwanda wakati hata raia hawana umeme wa nafuu vilevile unaongelea private sector wakuzalishie ili wakuuzie ili wewe ndio uuze naashiria kusema kwamba you have not looked at the whole equation....

 
Huo sio mradi wa nchi, ni mradi binafsi
Mradi Binafsi ambapo hao watu watawauzia Tanesco kwa bei gani kwa unit ?

Na je hio bei inaweza ikawa ndogo kama / kuliko gharama za uzalishaji wa unit kwenye Hydropower; Mwisho wa siku umeme ni huduma kwa nchi hakuna jambo la muhimu kama Nishati issue sio kuzalisha tu bali ni gharama pia...

By the way huo wakizalisha mchana wanawapa Tanesco (inawekwa kwenye grid directly) au wanatunza alafu wanawapa katika peak times (kukiwa na uhitaji ) yaani sio kuwauzia off-peak time kwa bei ya peak times....

Hayo yote inabidi tuyaweke kwenye consideration (electric generation kwa Tanzania na vyanzo vyetu haijawahi kuwa Tatizo); Kama hao ni ma-genius waende wakawekeze huko vijijini kwenye miundombinu migumu na wawauzia wateja directly (walifanya kina Mobisol et al); Kwa Tanesco kama chanzo ni kizuri wawekeze, kama ni mwekezaji basi auze cheaper kuliko kama Tanesco wangefanya wenyewe...

Huu utapeli wa kubinafsisha Nishati unaitafuta Europe mpaka kesho (watu wanapangiana bei wanavyotaka kwa mtaji wa mlipa kodi)
 
Ujerumani wanatumia huu umeme wa upepo, nchi nzima imejaa hayo makata upepo. Na sisi tunao mwingi maeneo ya Singida kuelekea Arusha.

Afrika kwa ujumla ni tajiri sana, na mzungu anatuzidi kwa hujuma nyingi anazopenyeza katika hizi nchi.
Germany nchi nzima imejaa makata upepo? Hii sio kweli, Germany wanatumia vyanzo vingi kuzalisha umeme. Huo wa upepo hauzalishi hata robo ya umeme wote

Tatizo kubwa lililopo kuamua kutumia vyanzo gani ni gharama za uzalishaji. Gharama za uzalishaji umeme kwa chanzo fulani zikiwa kubwa na gharama ya umeme itakua kubwa. Gharama ikiwa kubwa COP itakua kubwa
 
Kudebate na Shetani Nako ni shida 😁😁
Screenshot_20230530-140723.jpg
Screenshot_20230530-140534.jpg


Nioneshe Bilioni 300 hapo Juu 👆👆
 
Siyo mbaya...make hapo ni kama panels 125,000 ambayo ni sawa na Bilioni 62. Ukiongeza na storage batteries bank...cabling system pamoja na kujenga msongo wa kuinganisha kwenye line ya kuisafirisha. Naona gharama inakuja hapo.

Shida ni je tumejiandaa kwa ajili ya kuitunza na kubadilisha panels kwa muda muafaka? Make kwa uchafuzi huu wa TANESCO sijui....??
Swali kama miradi wa Nyerere wa Mega Watt 2015 umefikia asilimia zaidi ya 79, kulikuwa na haja gani na huu miradi?
 
Hapo umeambiwa sehemu tatu. Utalii, umwagiliaji na Umeme. Umeme gharama yake ni Tsh bilioni 300
Leta mgawanyo wa Kila sehemu usitafute pa kujifichia 🤣🤣

Hata gharama za mradi wa bwawa la Nyerere inasemwa hivyo hivyo Kilimo, kudhibiti mafuriko na Utalii sawa wewe kima.
 
Back
Top Bottom