TANESCO yasaini mkataba wa kuzalisha Umeme Jua MW 150 Kwa Bilioni 275. Waziri Makamba apiga marufuku mauziano ya Umeme kwa Dola

Nani amekwambia ni nyingi na issue sio viwanda tu hata sasa hivi raia hawapati umeme wa gharama nafuu wakati tuna vyanzo lukuki..., sasa kukimbilia na kuanza kuwaza mg 5000 wakati 2500 bado na unaongelea viwanda wakati hata raia hawana umeme wa nafuu vilevile unaongelea private sector wakuzalishie ili wakuuzie ili wewe ndio uuze naashiria kusema kwamba you have not looked at the whole equation....

Muulize kwanza hivi ukiwa 3 itaanza kukimbiia 8 kabla ya 5 au maanacm hata nusu tu hiyo 5000 hatijafikia au ni wale wanaopenda porojo za vijiweni sio
 
Tanesco inasaini mikataba mingi kwa Sasa HV tofauti kbsa na wizaraaa yoyote
 
Leta mgawanyo wa Kila sehemu usitafute pa kujifichia 🤣🤣

Hata gharama za mradi wa bwawa la Nyerere inasemwa hivyo hivyo Kilimo, kudhibiti mafuriko na Utalii sawa wewe kima.
Huwezi kufananisha mradi unaozalisha umeme wa sola tu na unaofanya umwagiliaji na miundombinu ya utalii. Mchanganuo ndiyo huo nimekupa, Kuzalisha umeme bilioni 300. zingine umwagiliaji na kujenga njia ya umeme kutoka huko, barabara, fidia kuhamisha watu, fidia mashamba, nk nk.
 
Umeme wa jua na upepo siku zote kwa africa ni utapeli

Serikali inabidi iweke uwazi je watauza kwa bei gani $5 cents per kwh au $10 cents per kwh maana hapa ndipo maswali yapo. isije kuwa umeme wa gharama za juu. Mfano ule umeme wa Uganda wa juzi ni $8 cents lakini Museveni anataka wanunue kwa $5 cents
 
Hii nchi yetu sijui kwenye issue ya umeme tumemkosea Mungu nini maana kila siku ni ngonjera tu tumetumbukiza fedha nyingi sana kwenye Bwawa la Nyerere
 
Germany nchi nzima imejaa makata upepo? Hii sio kweli, Germany wanatumia vyanzo vingi kuzalisha umeme. Huo wa upepo hauzalishi hata robo ya umeme wote

Tatizo kubwa lililopo kuamua kutumia vyanzo gani ni gharama za uzalishaji. Gharama za uzalishaji umeme kwa chanzo fulani zikiwa kubwa na gharama ya umeme itakua kubwa. Gharama ikiwa kubwa COP itakua kubwa
Windmills zimejaa Ujerumani kuanzia kaskazini kule Hamburg mpaka hukuchini Ulm. Ni kweli wana vyanzo vingi vya nishati.
 
China wamemaliza kujenga largest hydropower source duniani ,Tanzania uwe umeme wa kizamani kwa sasa ?
Wapi nimesema ni teknolojia ya kizamani?
Alafu huwezi kulinganisha ufanisi wa Hydropower China na Tanzania. Climatic change impacts on biophysical features are spatial temporal.
Sisi umeme wa Hydropower mbona tunao kitambo... Na changamoto zake za kujirudia ni zile zile ukame...mafuriko...matope kujaa kwenye mabwawa...

NB: is a very conventional and risk technology.
Solution ya umeme wetu ni kuwa na energy mix kutoka vyanzo vingi vingi... Na si kupriotitize Hydropower pekee
China wamemaliza kujenga largest hydropower source duniani ,Tanzania uwe umeme wa kizamani kwa sasa ?
 
Serikali Kupitia Tanesco imeandika Historia ya kusaini mkataba wa Kuzalisha Umeme wa Juna na kampuni ya China wenye thamani ya Shilingi Bilioni 275 ambao utazalisha megawatt 150 Kishapu ,Shinyanga na Kwa awamu ya kwanza Wataanza na megawatt 50.

Waziri wa Nishati January Makamba akishuhudia mkataba huo amepiga marufuku Tanesco kununua Umeme kutoka Kwa wazalishaji Kwa malipo ya dola badala yake Shilingi ndio ittumika..

Aidha amewataka Tanesco kuwawezesha wazawa Ili waweze kuzalisha umeme akisema hakuna maajabu Hadi wao washindwe..

My Take
Hongera sana Makamba,majungu achilia failures wewe endelea kuchapa kazi.

=======

Wizara ya Nishati kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) imesaini mkataba wa kwanza wa uzalishaji wa umeme Jua wa kiasi cha megawati 50 utakaotekelezwa wilayani Kishapu mkoani Shinyanga.

Mkataba huo umesainiwa tarehe 29 Mei, 2023 jijini Dodoma na kushuhudiwa na Waziri wa Nishati, Mhe.January Makamba ambaye alikuwa mgeni rasmi.

Kwa ujumla mradi huo wa umeme wa Jua ni wa megawati 150 ambapo awamu kwanza itajengwa mitambo itakayozalisha megawati 50 na awamu ya pili itajengwa mitambo ya megawati 100 kwa jumla ya shilingi bilioni 275. Utekelezaji wa mradi wa Awamu ya kwanza hautazidi miezi 12.

Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri wa Nishati amesema kuwa “kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi tunaingiza umeme wa Jua katika gridi ya Taifa, nimpomgeze Rais wetu kwa kwa muongozo na uongozi ambao umepelekea nchi kuaminiwa na washirika wa maendeleo ikiwemo Shirika la Maendeleo la Ufaransa ambalo limetoa mkopo ambao utatekeleza mradi huu.”

Ameeleza kuwa, utekelezaji wa mradi huo wa Jua ni jitihada za Serikali za kuhakikisha inatengeneza mchanganyiko wa umeme wenye afya katika gridi ya Taifa ambao utatokana na vyanzo mbalimbali kama vile maji, gesi, upepo na Jua ili hata pale chanzo moja kinapotetereka, vyanzo vingine vitaendelea kuzalisha umeme.

Waziri Makamba amesema kuwa, ili kuongeza zaidi uzalishaji wa umeme kwa kutumia nishati jadidifu, Serikali inakuja na Sera mpya ya Nishati Jadidifu (iko kwenye maandalizi) ambayo itasaidia nchi kuongeza uwekezaji kwenye eneo hilo kwani fedha nyingi duniani, masoko ya mitaji na teknolojia mpya zinajielekeza kwenye nishati jadidifu.

Ameongeza kuwa, kwa sasa kazi inayofanyika pia ni kuainisha maeneo yaliyo na rasilimali ya nishati jadidifu na kipaumbele kitakuwa kwa wazawa kuwekeza kwenye miradi kama ya Upepo na Jua na Serikali itawaunga mkono na kwamba Serikali itakuja na muongozo wa utekelezaji wa suala hilo.

Ameongeza kuwa, kwa maeneo yaliyo nje ya gridi kama vile visiwa, bado Serikali itaendelea kuwezesha jitihada za kupelewa umeme kwa kutumia miradi ya nishati jadidifu kama vile Jua na Upepo.

Wanini wakati tunategemea karibuni umeme wa bwawa la Nyerere?hii mikataba Inakuwa na capacity charge ambayo inahumiza Tanesco na Taifa.hii ni njia ya kuzipiga faida za Tanesco itakayotokana na na umeme wa bwawa la Nyerere.
 
Nani kasema?
 
Back
Top Bottom