TANESCO yatakiwa kutafuta vyanzo vipya vya nishati

TANESCO yatakiwa kutafuta vyanzo vipya vya nishati

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,566
Reaction score
4,013
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani ameiagiza Bodi na Menejimenti ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuhakikisha kuwa wanafanya tafiti kubaini vyanzo vipya vya uzalishaji umeme ili kuongeza kiasi cha nishati hiyo nchini na kuweza kufikia lengo la kuwa na megawati 10,000 ifikapo mwaka 2025.

Dkt.Kalemani alitoa agizo hilo tarehe 19 Disemba, 2019 jijini Dar es Salaam wakati wa kikao kati ya Wizara ya Nishati na Bodi/Menejimenti ya TANESCO ambapo kikao hicho kilihudhuriwa na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu na Kamishna Msaidizi wa Umeme, Mhandisi Innocent Luoga.

“Lazima tufanye tafiti kubaini vyanzo mbalimbali vya kuzalisha umeme ukiacha hivi vilivyopo, hata kama tusipotekeleza leo, vizazi vijavyo vitatekeleza miradi hiyo, mfano tafiti za mradi wa umeme wa Julius Nyerere (MW 2115) zilifanyika miaka mingi iliyopita, lakini mradi tunautekeleza sasa, hivyo nasi hatuna budi kuibua vyanzo vingine.” Alisema

Aidha, Dkt Kalemani aliiagiza Bodi na Menejimenti ya TANESCO kuhakikisha kuwa maeneo yote nchini yanaunganishwa na umeme wa Gridi ifikapo mwezi Juni 2022 ili wananchi wapate umeme wa uhakika na pia Serikali kuokoa fedha zinazotumika kununulia Mafuta ili kuendesha mitambo ya umeme kwenye baadhi ya maeneo nchini.

Kuhusu kazi ya usambazaji umeme vijijini, alisisitiza kuwa lengo la Serikali ni kufikisha umeme kwenye vijiji vyote ifikapo mwezi Juni mwaka 2021 na asilimia 85 ya wananchi wanapata umeme hivyo TANESCO ina jukumu la kuhakikisha kuwa lengo hilo linafanikiwa.

Vilevile, Dkt Kalemani aliiagiza TANESCO kuhakikisha kuwa, kila kiwanda au Taasisi ya umma inapojengwa, inafikishiwa umeme lengo likiwa ni kuongeza mapato ya Shirika na pia kuboresha upatikanaji wa huduma za kijamii nchini.

Aidha, aliiagiza Bodi na Menejimenti ya TANESCO kuongeza ukusanyaji wa mapato ya Shirika kutoka shilingi Bilioni 46 zinazokusanywa sasa kwa wiki hadi kufikia Bilioni 52 kwa Wiki.

Dkt. Kalemani aliongeza kuwa, Shirika hilo pia linapaswa kumaliza madeni yake ifikapo mwaka 2026, linaboresha nidhamu ya watumishi ili kuweza kutoa huduma bora kwa wananchi na kuhakikisha kunakuwa na mpango wa ukarabati wa miundombinu ya umeme kwenye maeneo yote nchini.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, pamoja na kuipongeza TANESCO kwa majukumu mbalimbali wanayofanya, aliiagiza Bodi kujielekeza pia kwenye ukusanyaji wa madeni ya TANESCO kutoka kwa wateja mbalimbali zikiwemo Taasisi za umma kwani fedha zitakazopatikana zitasaidia Shirika kuweza kutekeleza majukumu yake ipasavyo.

Aidha, aliiagiza TANESCO kuangalia suala la malipo ya huduma ya umeme ili kuwe na utaratibu wa malipo hayo kufanyika kwa awamu ili kuweza kuunganishia umeme wananchi wengi zaidi na hivyo miradi hiyo ya umeme kuleta tija.

Kamishna Msaidizi wa Umeme, Mhandisi Innocent Luoga, alisema kuwa, hali ya umeme nchini imeimarika hivyo TANESCO inapaswa kujikita pia kwenye kazi ya kuongeza wateja wa nishati hiyo ili kuongeza mapato.

Vilevile, alisisitiza kuhusu suala la mikoa yote nchini kuunganishwa na gridi ya Taifa ili kuimarisha hali ya umeme kwenye mikoa hiyo
 
Nyuklia ndiyo chanzo kikubwa Cha umeme na rafiki kwa mazingira hilo halihitaji utafiti, itakuwa ni kuharibu hela kwa makusudi, yapeni tenda hiyo makampuni ya ufaransa au marekani, uranium tunayo
 
Nyuklia ndiyo chanzo kikubwa Cha umeme na rafiki kwa mazingira hilo halihitaji utafiti, itakuwa ni kuharibu hela kwa makusudi, yapeni tenda hiyo makampuni ya ufaransa au marekani, uranium tunayo
Mnaweza kui manage? nishati ni jambo moja tu...kuna ishu ya usalama wenu.
 
Inawezekana..... Kwan wao wamewezaje?
Japan imewatoa jasho baada ya ile tsunami.

ila pia hilo swali lako zuri tungejiuliza pia kwa mambo yote kwa ujumla sio kuwa na vinu vya nyuklia pekee, kwa mfano pia tujiulize kama Brazil wamechukua World cup kwa nini sisi tushindwe?
 
Nyuklia ndiyo chanzo kikubwa Cha umeme na rafiki kwa mazingira hilo halihitaji utafiti, itakuwa ni kuharibu hela kwa makusudi, yapeni tenda hiyo makampuni ya ufaransa au marekani, uranium tunayo
Hebu tuisaidie management kuibua vyanzo vipya.
1.Pale mto Simiyu tunaweza jenga hyro power ya 300MW.
2. Singida tuplan kuweka wind farm ya 400MW, mradi wa mwakyembe uchukuliwe na Tanesco
3. Dodoma tunaweza jenga solor planet 300MW
4. Kiwira coal project tujenge 600MW
5. Manyara tunaweza jenga Geo therm ya 2000MW
6. Mto kagera tugenge 300MW project isaidizane na rusumo
7. Mto malagarasi tujenge 2000MW
8. Kihansi na bwawa la mungu ziwe up graded kufikia 600MW
9. Tanesco ianze mazungumzo kuinunua mitambo ya Song Gas, IPTL, Symbion na kuiwezesha kuzalisha 2000MW
10. Lindi tujenge Gas Turbine za 2000MW
11. Umeme wa Nyuklia 3000MW,
 
Mbele ya nyuklia hiyo miradi haioni ndani, ni uoga wetu tu ndiyo unatusumbua
 
Umeme wote huu hatuna kaz nao
Hebu tuisaidie management kuibua vyanzo vipya.
1.Pale mto Simiyu tunaweza jenga hyro power ya 300MW.
2. Singida tuplan kuweka wind farm ya 400MW, mradi wa mwakyembe uchukuliwe na Tanesco
3. Dodoma tunaweza jenga solor planet 300MW
4. Kiwira coal project tujenge 600MW
5. Manyara tunaweza jenga Geo therm ya 2000MW
6. Mto kagera tugenge 300MW project isaidizane na rusumo
7. Mto malagarasi tujenge 2000MW
8. Kihansi na bwawa la mungu ziwe up graded kufikia 600MW
9. Tanesco ianze mazungumzo kuinunua mitambo ya Song Gas, IPTL, Symbion na kuiwezesha kuzalisha 2000MW
10. Lindi tujenge Gas Turbine za 2000MW
11. Umeme wa Nyuklia 3000MW,
 
Kwamba umeme wa stieglers hautatosha???
Mkuu jumla ya umeme wote tulionao pamoja na ule wa Rufuji haviwezi kitufanya tuwe nchi ya viwanda. Ni umeme kidogo sana kwa watu mil 60 tulionao.

Nchi ya viwanda itafikiwa tutakapokuwa na umeme kuanzia MW 40,000 na watu wasiozidi mil 80.
 
Nyuklia ndiyo chanzo kikubwa Cha umeme na rafiki kwa mazingira hilo halihitaji utafiti, itakuwa ni kuharibu hela kwa makusudi, yapeni tenda hiyo makampuni ya ufaransa au marekani, uranium tunayo
Hapana mkuu nuclear ata sio future ya dunia kwa upande wa Nishati kwa sasa tunauhitaji zaidi wa vyazo Vya nishati asilia yani renewable energy kama Water falls, sun, Geothermal n.k vyazo vya namna hii kwanza haviharibu mazingira pia running costs zake ni ndogo sana compare na hizo nuclear afu kwa africa ni nchi moja tu South africa ndio ina nuclear plant ambayo nayo ina add up kama 5% tu ya umeme kwenye national grid yao..Nuclear ni hatari sana mkuu na inahitaji umakini wa hali ya juu vinginevyo imaweza kuleta maafa makubwa mimi naishauri tanesco izidi kujikita katika renewable sources kwa vìle ni unlimited pia Waache kampuni binafsi zitumie renewable sources kama solar panel kuzalisha umeme na kuwauzia kwenye Grid lakini yote kwa yote kuna changes kubwa zimetokea na Mgawo wa umeme ni kama hakuna kabisa japo kuna maeneo machache yana face outages ila ni within a short time na power ina kuwa restored very quickly
 
Roadmap acha uoga mkuu, dunia iliyoendelea inatumia nyuklia gharama ndogo, hakuna uharibifu wa mazingira, TANESCO njooni huku muamulie ugomvi kabla hatujatoana ngeu
 
Japan imewatoa jasho baada ya ile tsunami.

ila pia hilo swali lako zuri tungejiuliza pia kwa mambo yote kwa ujumla sio kuwa na vinu vya nyuklia pekee, kwa mfano pia tujiulize kama Brazil wamechukua World cup kwa nini sisi tushindwe?
Tanzania kutumia nuclear power tuko nyuma hatua kumi..... Tanzania kuchukua world cup tuko nyuma hatua 9.99×10^100000000
 
Back
Top Bottom