Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Dar es Salaam, 19 Februari 2025 - Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limetangaza mpango wa maboresho katika Kituo cha Kupokea, Kupooza, na Kusambaza Umeme cha Msongo wa Kilovoti 220 kilichopo Ubungo, Dar es Salaam. Maboresho haya yanatarajiwa kuanza Jumamosi, tarehe 22 hadi 28 Februari 2025.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TANESCO, hatua hii inalenga kuboresha huduma kwa wateja kutokana na kuongezeka kwa mahitaji ya umeme katika maeneo ya Zanzibar, Dar es Salaam, na Pwani.
Kituo hicho kimeelemewa na mahitaji yaliyopo, hivyo kitafungwa kwa muda ili kuweka Mashineumeme (Transformer) mpya yenye uwezo wa MVA 300 ili kukidhi mahitaji ya umeme katika maeneo husika.