Mpita Njia
JF-Expert Member
- Mar 3, 2008
- 6,997
- 1,172
Utakuwa ni saa nane kila siku zinatazogawanywa katika vipindi viwili vya saa nne nne kila kimoja. Yaani, kama ni zamu yenu ya kukosa umeme, mtakosa asubuhi kwa saa nne, na jioni kwa saa nne.
Mgawo unaanza mara moja.
tanesco wanasema mgawo unatokana na kuharibika ghafla kwa mitambo miwili ya Songas.
I hope it is not part of concerted efforts to 'force' the buying of Dowans turbines
hakuna evidence ya kuharibika kwa mitambo ya songas, huu ndo msimu wake babake wa kukatwa umeme. wasitufanye wajinga.
au hii ni tetesi?
lete source mkuu.
...Kama mmewahi kusikia kuwa nchi imetekwa nyara.. basi ndiyo hivyo..
Bora turudi ktk vibatari na chemli tujipange upya.Nyie hamtaki.. nilisema Mwezi wa nne watu wakaja juu utadhani nini! Nimesema majenereta yatanunuliwa mtake msitake kwani kuna watu wanadaiwa na lazima walipe milioni 60 si mchezo.. watu hawataki. Na mkigoma mtanyimwa umeme masaa 12 hadi mpige magoti na kukubali kuvunjwa!
Msiwe na shaka.. kesho na Ijumaa nadhani moto wa mapambano unazidi kuwashwa! Maneno ya Mzee Malecela leo yatakuwa yameangukia kwenye sikio lisilosikia! Kama mnataka ile kongwa ya mafisadi ivunjwe ni kuendelea kusimama imara kuipinga Dowans; Kama mmewahi kusikia kuwa nchi imetekwa nyara.. basi ndiyo hivyo.. je mtafanya nini kuigomboa?
Leo wanataka mnunue Dowans.. ili wawape umeme kesho watataka mfanye nini? !!
NO DOWANS, NOT BOWING DOWN!
I have ni my possession a Tanesco Statement announcing the mgawo
Huo mgawo ni nchi nzima?
Hapana, ni dar es Salaam tu. Mitambo ya Songas iliyoleta matatizo inatumika kuzalisha umeme kwa ajili ya Dar na Zanzibar, hivyo sehemu nyingine za nchi hazitaathirika. Hata hivyo, tanesco hawajasema iwapo Zanzibar nayo itaathirika. Kwa kawaida dar na Zenji zinatumia kama megawati 370 hivi, zilizokosekana kutokana na kuharibika kwa mashine hizo ni megawati 53.
Mi naomba kutoa ushauri, tuanze mapema kujizaititi na mgawo huu , tununue mishumaa na vibatari na wenye uwezo wanunue jenereta, tukae tukisubiri Dowans washindwe na walegee!
Leo wanataka mnunue Dowans.. ili wawape umeme kesho watataka mfanye nini? !!
NO DOWANS, NOT BOWING DOWN!
hakuna evidence ya kuharibika kwa mitambo ya songas, huu ndo msimu wake babake wa kukatwa umeme. wasitufanye wajinga.
au hii ni tetesi?
lete source mkuu.