Tanesco yatangaza mgawo; kuanza mara moja!

Tanesco yatangaza mgawo; kuanza mara moja!

"This Idris Rashid person should go. How do they measure his perfomance, anyway? He is a total FAILURE."

*************************************

MiratKad:

1. Kabla hajaondoka Rashid arudishe zile dola 600,000 za mgao wa radar -- zilitoka kwa wananchi na hana haki nazo yeye.

2. Lakini hakuna jambo hapa? Kuharibika kwa mitambo ya Songas kumekuja masaa 24 baada ya kampuni hiyo kutangaza kwamba haina mpango kununua mitambo ya Dowans kwa maelezo kwamba haifai kuendeshwa kibiashara.

3 Mafisadi wako tayari kufanya chochote, hata kuingiza nchi kwenye machafuko ili watimize tamaa zao. Hii imeshatokea katika nchi kadha. Wanajua fika kuwa valangata likizuka wao haoooo.. nchi za nje kwenda kuponda mapesa waliyotuibia. nawasikitia wapambe wao -- Balile, Manyerere na wengine, maana wataachwa tu nyumbani tufe nao.
 
As long as fisadi Idris Rashid hafukuzwi kazi Tanesco this country will be in SHIT!!!
 
This Idris Rashid person should go. How do they measure his perfomance, anyway? He is a total FAILURE.

Naona sio sahihi unavyosema maana wengi wetu tumekataa katakata Tanesco wasinunuwe ile mitambo ya nanihiii sijuwi richmond ama dowans. Serikali pia ilipigwa stop na sauti ya bunge letu wakati Spika alipotahadharisha juu ya ununuzi wa hio mitambo.

Tatizo sisi waTz tunajifanya wahuaji sana. Hatutaki ushauri wa wataalamu na kila mmoja tunamuona kama fisadi. Sijui nani fisadi? Mgao tayari ndio huo na kama ni wa kulaumiwa basi nadhani sio serikali bali wataalamu wa bunge letu tukufu tuliowapa kula zetu wao wanaishi kwa raha na majenereta. Nani hasa fisadi?

Ni jambo linalosikitisha sana lakini ikibidi hali ndio itakuwa hivyo. Idris Rashid munamuandama sijui kwa lipi. Yeye kama mtendaji ameshauri sana na kawekwa katika kundi la fisadi.

Poleni sana mulio Dar.
 
Hatutaki ushauri wa wataalamu na kila mmoja tunamuona kama fisadi. Sijui nani fisadi? Mgao tayari ndio huo na kama ni wa kulaumiwa basi nadhani sio serikali bali wataalamu wa bunge letu tukufu tuliowapa kula zetu wao wanaishi kwa raha na majenereta. Nani hasa fisadi?

Ni jambo linalosikitisha sana lakini ikibidi hali ndio itakuwa hivyo. Idris Rashid munamuandama sijui kwa lipi. Yeye kama mtendaji ameshauri sana na kawekwa katika kundi la fisadi.

Poleni sana mulio Dar.

Kwani wataalamu wamekatazwa kutangaza tenda ya mejenereta mapya toka mwaka jana mwezi wa Nane 2008 walipofuta mkataba wa Dowans hawakujua mahitaji ya umeme? Kama hawakujua basi sio wataalamu wa kuaminiwa. Kama walikuwa wanajua walikua wapi kuueleza umma kuwa wanahitaji mitambo mingine mipya kufidia pengo linalotokana na kutokuwepo kwa Dowans? Rashid atalaumiwa tu asitufanye watoto wadogo kuwa hatujui mchezo wanaoucheza. Na ashukuru analindwa na aliyemteua la sivyo angshatimliwa zamani. Anatushauri kununua mabomu badala ya magenereta mapya huo ndiyo ushauri?

Tuwape heko wabunge walioliona hilo na kushauri mitambo ya dowans isinunuliwe bahati mbaya selikari imeweka pamba maskioni na kututesa kwa mgao ili tutii amri na kukubali mitambo ya dowans.
 
Hii sio habari mpya kwangu!!! ni jambo ambalo nilisema humu kwamba linaweza tokea wakati wowote... na jambo lenyewe ni rahisi sana, shirika lolote ya ku-kugenerate umeme linatakiwa liwe na 15% additional capatity au umeme sawa na generator moja kubwa kwenye pool ya majenerata yake... ndio hili TANESCO walituambia tukapiga siasa zetu...sasa wakati umefika!

Hili ni jambo la kawaida mitambo hiyo lazima iharibike kama ndege, gari na engine ya train inavyoharibika au hata ukifanya preventive maintenance mara nyingi lazima uzime hiyo mitambo si ndio... tuache siasa kila mahali watanzania ndio maana hatuendelei.

Watu wanaohusisha na ununuzi wa mitambo ya DOWANS ni wanasiasa wakubwa... kwa kuwa Songas inapokuwa haitoi umeme inakosa mapato... hao shareholders wake sio wanasiasa kama sisi, hawewezi kukubali ujinga kama sisi tunaopenda.
 
Hii sio habari kwangu!!! ni jambo rahisi, shirika lolote ya ku-kugenerate umeme linatakiwa liwe na 15% additional capatity au umeme sawa na generator moja kubwa kwenye pool ya majenerata yake... ndio hili TANESCO walituambia tukapiga siasa zetu...sasa wakati umefika.

Hili ni jambo la kawaida mitambo hiyo lazima iharibike kama ndege, gari na engine ya train inavyoharibika.

Watu wanaohusisha na ununuzi wa mitambo ya DOWANS ni wanasiasa wakubwa... kwa kuwa Songas inapokuwa haitoi umeme inakosa mapato... hao shareholders wake sio wanasiasa kama sisi, hawewezi kukubali ujinga kama sisi tunaopenda.

we endelea kuwatetea tu! Nunueni basi hiyo mitambo ya Dowans yaishe! Taifa zima, kampuni nzima, serikali nzima haina njia nyingine isipokuwa kununua mitambo ya kampuni ya kilaghai! So why don't they just buy them.? Hela si wanazo? Kura si wanazo Bungeni?

Tatizo ni kuwa wanajua hawawezi kununua cha mwizi huku wakijua ni mwizi bila ya kumkamata kwa kuwaibia!
 
Nunueni basi hiyo mitambo ya Dowans yaishe! Taifa zima, kampuni nzima, serikali nzima haina njia nyingine isipokuwa kununua mitambo ya kampuni ya kilaghai! So why don't they just buy them.? Hela si wanazo? Kura si wanazo Bungeni?

Tatizo ni kuwa wanajua hawawezi kununua cha mwizi huku wakijua ni mwizi bila ya kumkamata kwa kuwaibia!

Kweliiii
 
Hapa mi sioni kama kuna stori mpya yoyote ile......wao na waukate tu wala haina haja ya kutoa press release yoyote ile.
 
Ama kweli nchi yetu inachekesha..
Ni asilimia 12 tu ya nchi inayopata umeme nchini na kati ya hizo asilimia 50 unatumika Dar!..Na leo tunaambiwa umeme wa mgao dar hivi uwezo wetu ktk umeme ni Upi haswa?
Wakuu wa mahesabu nipeni mahesabu hapa naogopa kufikiria!...
Inatisha nchi yetu..
 
Naona sio sahihi unavyosema maana wengi wetu tumekataa katakata Tanesco wasinunuwe ile mitambo ya nanihiii sijuwi richmond ama dowans. Serikali pia ilipigwa stop na sauti ya bunge letu wakati Spika alipotahadharisha juu ya ununuzi wa hio mitambo.

Tatizo sisi waTz tunajifanya wahuaji sana. Hatutaki ushauri wa wataalamu na kila mmoja tunamuona kama fisadi. Sijui nani fisadi? Mgao tayari ndio huo na kama ni wa kulaumiwa basi nadhani sio serikali bali wataalamu wa bunge letu tukufu tuliowapa kula zetu wao wanaishi kwa raha na majenereta. Nani hasa fisadi?

Ni jambo linalosikitisha sana lakini ikibidi hali ndio itakuwa hivyo. Idris Rashid munamuandama sijui kwa lipi. Yeye kama mtendaji ameshauri sana na kawekwa katika kundi la fisadi.

Poleni sana mulio Dar.

Mkuu samahani sana,

Nimekuwa nafuatilia kauli zako kuhusu Dowans, na zaidi kuhusu Idrisa unamtetea sana na hoja yako kubwa ''Hamkusikiliza ushauri wa wataalamu''-

Hi unajua hapa JF kuna wataalam wa kila fani tena waliobobea????? Je unafahamu hata wataalamu wa Tanesco wako hapa hapa na wanapinga???

Hebu tupe wewe huo ushauri wa kitaalam uliotolewa unadhani ni bora kuliko yanayosemwa hapa.

Nikuulize tu, unafahamu Tanesco installed capacity yake ni kiasi gani????? Je unafikiri wakizalisha walau 80% ya installed capacity wanahitaji jenerator hata moja???????

Pili unafahamu umeme unaopotea kwa sababu ya uzembe wa kutokufikiri ( na watu kulelea vitambi bila kufanya kazi ) ni kiasi???? Hao wataalamu wako wanafanya kazi gani???? tujuze kabla sijakupa maswali mengine magumu zaidi

WAZEE WA KUCHOMA NDIZI
 
Hii sio habari mpya kwangu!!! ni jambo ambalo nilisema humu kwamba linaweza tokea wakati wowote... na jambo lenyewe ni rahisi sana, shirika lolote ya ku-kugenerate umeme linatakiwa liwe na 15% additional capatity au umeme sawa na generator moja kubwa kwenye pool ya majenerata yake... ndio hili TANESCO walituambia tukapiga siasa zetu...sasa wakati umefika!

Hili ni jambo la kawaida mitambo hiyo lazima iharibike kama ndege, gari na engine ya train inavyoharibika au hata ukifanya preventive maintenance mara nyingi lazima uzime hiyo mitambo si ndio... tuache siasa kila mahali watanzania ndio maana hatuendelei.

Watu wanaohusisha na ununuzi wa mitambo ya DOWANS ni wanasiasa wakubwa... kwa kuwa Songas inapokuwa haitoi umeme inakosa mapato... hao shareholders wake sio wanasiasa kama sisi, hawewezi kukubali ujinga kama sisi tunaopenda.

Unajua kazi ya Bwala la KIHANSI kubwa ni backup hiyo 15% na ndio maana kila wakati umeme unaozalishwa hapo ni kwa capacity ya chini sana ili iwe ka reserve. kwa maelezo zaidi soma: Report ya Tanesco aliyopeleka kwa kamati ya Zitto et al.

WAZEE WA KUCHOMA NDIZI
 
Mie nauliza, je, tunaweza kufanya mgomo baridi wa kuinyima TANESCO mapato, kwa kupunguza - kwa lazima - matumizi ya umeme, kwa sisi wateja wa LUKU? Kwa mfano, wanapoturejeshea umeme, tunaongeza 2 hours za mgomo, juu ya hizo 4 hours zao wanazosema, kwa hiyo jumla tunaongeza 4 hours, 2 hours asubuhi na 2 hours mchana, for a total of 12 hours kwa siku! Je, inawezekana? Tuone nini kitafanyika?

Mimi najua kwamba hii power crisis ni artificial, na hapa kuna njama za kutaka kununua hiyo mitambo ya umeme ili hao mafisadi wapate 20 percent zao! Sasa nini kifanyike tuwaoneshe kwamba tumechukizwa na ufisadi huo? Can we BOYCOTT TANESCO?
 
Cha kushangaza ni kwamba Ngeleja alishatoa kauli kwamba hakutakuwa na mgao, Sasa kulikoni? Ngeleja anajikanyagakanyaga kila siku na kauli ambazo hazina ukweli wowote pamoja na hayo Mkuu wake wa kazi anamwacha aendelee kupeta tu!! Kazi kweli kweli. Dar maji shida sasa na umeme hakuna 🙁
Kazi kweli kweli!!! na haya matatizo yasiyokwisha miaka nenda miaka rudi.

tatizo sio ngejela, dowans,rostam au nani
tatizo ni mkulu mwenyewe
hao wengine ni vibaraka tu yeye aonekane mzuri wengine wabaya
 
Chakufanya nikumbana huyu Rostam wenu mapaka hiyo 60million akamkamue mama yake mzazi. Enough is enough..
 
Unajua kinachoumiza sana ni pale Wataalamu wetu walioko huko nje wanafanya mambo yanasikilizwa..............na nchi husika haziingii ktk matatizo kama tunayoyaona hapa nyumbani........you knowa why....beacuse they have leaders who are committed and determined kuwahudumia wananchi wao....and they become proud of their achievements...........kwetu sisi viongozi huwa proud ku-achieve 10% na kuzikimbiza Uswisi and Caribbean....matokeo yake ndiy hayaaa......Songas ina mushkeli....jamani!!
 
Hili tangazo la mgao linashangaza kidogo, siku zote ukipita k'koo mchana hakuna umeme. Kwetu kila j'mosi na j'pili wanachukua mapema tu, huu ni mwezi wa pili sasa na wiki iliyopita wamekuwa wakichukua hata ktk ya wiki. Kubwa yake j'pili iliyopita wamechukua umeme wao asubuhi wamerudisha j'tatu saa 4:30 usiku. Unapotangazwa mgao leo hii inamaana ule uliokuwapo siku zote ulikuwa ni nini?, au wanataka kusema ndio hakutakuwa na umeme kabisa?. Kama wakati generators hazijaaribika hali ilikuwa hivyo sasa zimeharibika si itakuwa tusahau kabisa habari ya umeme!.
 
tangazo limetolewa labda kwa sababu mgawo utagusa Masaki,Mikocheni, osterbay na mbezi beach.
 
Back
Top Bottom