Baba Ubaya
Senior Member
- Jun 24, 2008
- 127
- 21
Mkuu Zitto,Safi sana. Ninawajulisha TANESCO ili tuone jinsi ya kutatua tatizo la Mwanza kwanza. PM address details zako na za huyo President wenu. Nakutana na TANESCO next week kwenye kamati kupitia hesabu zao na kupata maelezo ya madhara ya ule mgawo wa mwanzo. Naomba hizo details haraka tafadhali tuokoe nchi yetu.
Katika hali ya kawaida inachukua mwaka, katika hii ambayo watu wamecancel order inachukua muda gani kufunga na kuwasha?
Tunacho hoji siyo yanayotokea leo..... ni uzembe wa muda mrefu. Wewe kama unafikiri unaelewa zaidi mambo ya uendeshaji wa mashirika kama ilivyo tanesco...nadhani unakosea na wala hujui taaluma za kila member wa JF. Unasema mitambo inafanya kazi 24hrs bila kupumzishwa.......mitambo za ziada (standby..),....who should do that? Kazi ya tanesco ni nini?
Unasema wabongo wanapenda kupindisha mambo.....kk mjadala huu ni nini kimepindishwa?? Jaribu kutumia akili kabla huja bandika ujinga wako humu.
Mkuu Zitto,
Ur not serious!.. are You?
Mkuu tulikwambia toka siku zile kwamba mitambo ipo na sii GE peke yake mipya na kukukuu maadam wapeni kazi vijana wataifanya..Mimi binafsi nilikwambia pia kabla na baada ya mgogoro wa Dowans...nimeandika humu humu JF iweje leo somo tunarudia kule tulikotoka?..
Acha mbali kwamba Lowassa alipotembelea hapa (hatukuonana naye alikwenda Mexico badala ya kukutana na Watanzania)niliwajulisha baadhi ya viongozi walioandamana na msafara wake, lakini Richmond ilikuwa ndio somo na hakuna upinzani.
Sasa nenda kawaone hao Tanesco wambie vijana wapo tayari kisha rudisha kazi hiyo hapa JF utaona uwezo wa vijana mnapowapa kazi ya taifa...
Binafsi siwezi kwenda ovyo kutafuta mitambo kisha majibu yenu yawe yale yale tunaonekana wajinga na matapeli.. ongea na Tanesco watupe go ahead, contact zao hata iwe kupitia kwako tutaifanya kazi tena haraka kuliko mtakavyo fikiria.
Kisha gharama ya ujenzi haiwezi kuwa kubwa kwa sababu ile mitambo ya Richmond/Dowans tayari ilikwisha jengewa na kufanya kazi hivyo chochote mtakachonunua kitawekwa pale ilipokuwa mitambo ya Dowans au sio!.
Mkuu Zitto, nimekuelewa lakini umesema mengi sana hapa swali linabaki pale pale kuwa kwanini matatizo haya hayaishi Tanesco na mipango yote hiyo toka serikalini??Brother,
Nadhani unajua taratibu za serikali hazitaki ivo. Zabuni inatangazwa na kisha inafanyiwa tathmini na ndio mshindi anatangazwa. Mpaka sijui kama GE waliomba TANESCO walipotangaza zabuni hii. Ninyi mlipaswa kuwajulisha wazalishaji mara baada ya kuona tangazo la zabuni. Mkandara ulipaswa kuwa proactive na sio kusubiri kuja hapa kulalama. Hivi ulifanya nini baada ya zabuni kutangazwa? Hivi sasa kuna mgawo, sheria sasa inatoa lee way ya udharura na hapo ndipo tu TANESCO wanaweza kushop na kupata 3 quotations na kisha kununua.
Ujenzi wa mtambo kaka ujue kuna 100MW unaotakiwa Dar kwa haraka na 60MW unaotakiwa Mwanza haraka. Huo wa Dar unaweza kuwekwa pale ilipokuwapo ya Dowans na kufanya marekebisho fulani fulani. Lakini pia ni lazima TANESCO ipate eneo lingi la mbali kujenga na kuweka mitambo hii kwani pollution imekuwa too much Ubungo.
TANESCO wametimiza wajibu wao kwa upande wao licha ya mapungufu yao. Lakini na sisi tutimize wajibu wetu kaka na sio kusubiri mambo yaharibike tuje kuleta lawama hapa.
Mpaka hapa tunapozungumza TANESCO hawajapata pesa za kununua hiyo mitambo kutoka serikalini na wametoa tahadhari zote na kuweka wazi mipango yote ya muda mfupi, wa kati na mrefu.
Ikumbukwe tena, narudia, mikataba yote ya kifisadi ambayo imeingiwa katika sekta ya Nishati iliingiwa kwa shinikizo la Serikali na sio TANESCO. Uongozi wa sasa wa TANESCO haujaingia mkataba wowote wa nishati isipokuwa umevunja mkataba mmoja, ule wa Dowans, baada ya kupata legal opinion kutoka Rex Attorneys.
Uongozi wa sasa umesafisha vitabu vya TANESCO na kupunguza sana hasara na sasa Shirika linaelekea kupata faida kwa mara ya kwanza. Mgawo huu utaathiri sana mapato ya shirika na hata kutia wasiwasi uwezo wa shirika kulipa deni lake kwa taasisi za fedha - kitu ambacho kitatuma bad message to the financial sector!
Kweli kwa mtu mwenye akili ukijiuliza unashindwa kuelewa. Ni nini kinatendeka pale tanesco, miaka yote wapo wahandisi, wanansheria, mameneja, mafundi wazuri tu lakini ni aibu tupu.
Lakini chanzo cha yote ni serikali kuingilia maamuza ya menejimenti za tanesco kwa muda mrefu. Kesi ya IPTL ni serikali, richmond ni serikali, songas japo wanajikongoja lakini ni serikali kwa hiyo ni lazima tufike mahali siasa ikae pembeni.
Mimi kila mara namuuliza ngeleja, ni kwa nini asitangaze wafanyabiashara/makampuni makubwa yaje yawekeze mitambo yao ya kuzalisha na kusambaza umeme wenyewe na walipe kodi kama ktk biashara nyingine!!! Lakini ni kimya tu, oh... mara tunamikakati...oh mara tuna mgao utakuwa historia......na upuuzi mwingine mwingi.
Hata kama hii ni justification ya kununua mitambo ya Dowans, still siyo suluhisho la matatizo ya umeme tanzania. Niliwahi kutoa mfano kwamba mtu/kampuni inaweza ikapewa wilaya au hata mkoa mzima izalishe na isambaze umeme na kukusanya mapato kutoka kwa watumiaji, then ilipe kodi serikalini. Sijui viongozi wa serikali wana nini kichwani, alafu mtu anakurupuka anasema Ngeleja ni waziri kijana?? kijana gani hana vision??[/QUOTE]
Waziri kijana team ya RA, kawekwa ili asaidie kunyonya na kurahisisha maslahi ya mafisadi. Kuna siku anahojiwa na Star TV anasema mji wa Kahama umendela kwa sababu ya wawekezaji wa madini alininifua sana, Kahama haijaendelea kwa chochote kutokana na wawekezaji, kwani kilichoogezeka Kahama ni mrundikano wa watu wasio na kazi walifika kwa matumani ya kupata kazi baadaye wanageuka kuwa majambazo baada ya kukosa kazi na ongezeka la malaya wauza miili. Barabara Kahama zimechoka, hospital ya toka mkoloni haijapanuliwa na kuongezaw ward hata moja
Zitto,Brother,
Nadhani unajua taratibu za serikali hazitaki ivo. Zabuni inatangazwa na kisha inafanyiwa tathmini na ndio mshindi anatangazwa. Mpaka sijui kama GE waliomba TANESCO walipotangaza zabuni hii. Ninyi mlipaswa kuwajulisha wazalishaji mara baada ya kuona tangazo la zabuni. Mkandara ulipaswa kuwa proactive na sio kusubiri kuja hapa kulalama. Hivi ulifanya nini baada ya zabuni kutangazwa? Hivi sasa kuna mgawo, sheria sasa inatoa lee way ya udharura na hapo ndipo tu TANESCO wanaweza kushop na kupata 3 quotations na kisha kununua.
Ujenzi wa mtambo kaka ujue kuna 100MW unaotakiwa Dar kwa haraka na 60MW unaotakiwa Mwanza haraka. Huo wa Dar unaweza kuwekwa pale ilipokuwapo ya Dowans na kufanya marekebisho fulani fulani. Lakini pia ni lazima TANESCO ipate eneo lingi la mbali kujenga na kuweka mitambo hii kwani pollution imekuwa too much Ubungo.
TANESCO wametimiza wajibu wao kwa upande wao licha ya mapungufu yao. Lakini na sisi tutimize wajibu wetu kaka na sio kusubiri mambo yaharibike tuje kuleta lawama hapa.
Mpaka hapa tunapozungumza TANESCO hawajapata pesa za kununua hiyo mitambo kutoka serikalini na wametoa tahadhari zote na kuweka wazi mipango yote ya muda mfupi, wa kati na mrefu.
Ikumbukwe tena, narudia, mikataba yote ya kifisadi ambayo imeingiwa katika sekta ya Nishati iliingiwa kwa shinikizo la Serikali na sio TANESCO. Uongozi wa sasa wa TANESCO haujaingia mkataba wowote wa nishati isipokuwa umevunja mkataba mmoja, ule wa Dowans, baada ya kupata legal opinion kutoka Rex Attorneys.
Uongozi wa sasa umesafisha vitabu vya TANESCO na kupunguza sana hasara na sasa Shirika linaelekea kupata faida kwa mara ya kwanza. Mgawo huu utaathiri sana mapato ya shirika na hata kutia wasiwasi uwezo wa shirika kulipa deni lake kwa taasisi za fedha - kitu ambacho kitatuma bad message to the financial sector!
Mkuu wangu, kwanza unaelewa uwezo wangu mimi mlalahoi inapokuja swala la tender.Sina uwezo wa hali na mali hivyo kunilaumu ati nilitakiwa kuwa proactive ktk tender ambayo kwa aslimia 100 unaelewa kingetokea kitu gani...Kumlaumu mtu yeyote leo hii baada ya kuelewa kilichotokea wakati wa tender hiyo ni kuepa ukweli wa yale yanayotokea nyumbani... Hivi kweli ktk akili yako unafikiria mimi Mkandara ningeweza kupindisha tender aliyopewa Richmond yakakataliwa mashirika mengine kwa sifa gabi haswa!...Nadhani unajua taratibu za serikali hazitaki ivo. Zabuni inatangazwa na kisha inafanyiwa tathmini na ndio mshindi anatangazwa. Mpaka sijui kama GE waliomba TANESCO walipotangaza zabuni hii. Ninyi mlipaswa kuwajulisha wazalishaji mara baada ya kuona tangazo la zabuni. Mkandara ulipaswa kuwa proactive na sio kusubiri kuja hapa kulalama. Hivi ulifanya nini baada ya zabuni kutangazwa? Hivi sasa kuna mgawo, sheria sasa inatoa lee way ya udharura na hapo ndipo tu TANESCO wanaweza kushop na kupata 3 quotations na kisha kununua.
Zitto,
Umejiingiza sana kwenye masuala ya TANESCO kuliko shirika jingine lolote la UMMA. Hii ni hatari kwako kwani wewe unaongea na MENEJIMENTI tu, undani hasa wa shirika lile hauujui. Iachie Bodi ya TANESCO ifanye kazi yake. Ufisadi uliomo ndani ya TANESCO hakuna siku litakaa litengeneze faida!
Ndio hapoo basi Tazara wenyewe wamefanya maamuzi ya mkataba na GE kwa sababu wanajua wanachokitaka hakuna siasa wala haziwezi kuingia huko Tazara..Laa sivyo ungesikia kampuni ya Kihindi Rites wamepewa tender ku overhaul injini zote zimetumwa India..kwa jinsi zitto alivyoelezea hapo juu kama sio kutaja jina waweza fikiri ni Dr. Idriss alikuwa akifanya press comference,well done Zitto...... nafahamu hawa GE waliingia pia mkataba na TAZARA kusupply baadhi ya equipments labda mdau Zitto na wengine mnijulishe hapa ilikuwaje tender ilitangazwa?au GE walikuwa contracted direct?