Zitto,
Nadhani unajua taratibu za serikali hazitaki ivo. Zabuni inatangazwa na kisha inafanyiwa tathmini na ndio mshindi anatangazwa. Mpaka sijui kama GE waliomba TANESCO walipotangaza zabuni hii. Ninyi mlipaswa kuwajulisha wazalishaji mara baada ya kuona tangazo la zabuni. Mkandara ulipaswa kuwa proactive na sio kusubiri kuja hapa kulalama. Hivi ulifanya nini baada ya zabuni kutangazwa? Hivi sasa kuna mgawo, sheria sasa inatoa lee way ya udharura na hapo ndipo tu TANESCO wanaweza kushop na kupata 3 quotations na kisha kununua.
Mkuu wangu, kwanza unaelewa uwezo wangu mimi mlalahoi inapokuja swala la tender.Sina uwezo wa hali na mali hivyo kunilaumu ati nilitakiwa kuwa proactive ktk tender ambayo kwa aslimia 100 unaelewa kingetokea kitu gani...Kumlaumu mtu yeyote leo hii baada ya kuelewa kilichotokea wakati wa tender hiyo ni kuepa ukweli wa yale yanayotokea nyumbani... Hivi kweli ktk akili yako unafikiria mimi Mkandara ningeweza kupindisha tender aliyopewa Richmond yakakataliwa mashirika mengine kwa sifa gabi haswa!...
Pili, nadhani utakumbuka vizuri kwamba niliwahi kuandika hapa hapa JF kwamba hatuhitaji kuweka tender, mashirtika kama GE haliwezi kuingia ktk mashindano ya tender.. wao ni watengenezaji wa mitambo ambayo wewe mnunuzi unakwenda dukani na kutoa order yako.. mara nyingi utakuta mashirika kama haya wanauza franchize, hivyo kuwezesha kupanuka kwao kama vile unavyoona ma agent wa magari ya BMW, mahotel na kadhalika, hao ndio wanaweza kuingia ktk tender zinazotolewa... GE hana shida kabisa ya kuingia mradi wa kufua umeme wakati sisi ndiio walalahoi wenye shida tunaotafuta kujikwamua..
Naijuia vizuri nchi yangu na naelewa haikuhitaji kufanyika kwani sisi ndio tunaotembea uchi, leo tukatangaze tender hata hao FUBU waliofulia hawatakuja ila wachuuzi toka China wenye njaa kama sisi ndio watajitokeza..Haihitaji elimu ya chuo kikuu kuelewa kwamba tunajaribu kuiga vitu wakati sisi bado kabisa tunavaa mitumba ktk maendeleo, yaani hatufahamu kile tunachokihitaji.
Ebu nambie wewe iweje mnatoa tender ambayo mnatafuta mali bora kwa bei rahisi pasipo kuwa na taarifa kamili ya mali mnayoitafuta.. mathlan ukitaka kununua nguo dukani ni lazima uwe na hint fulani mathlkn Armani suit, kisha unapoita walanguzi unaitazama mali (nguo) hiyo kama ni Armani halali au feki na sii kuita wachuuzi wa nguo waje kujieleza wao wakati wewe huna idea kabisa ya utengenezaji wa nguo wala designer unayemhitaji..Huo Uimara itaujua vipi kwa kusoma maandishi yaliyochapishwa kiutaalam na mlanguzi?
Hata magari mnayoagiza hayo mashangingi siii mnajua fika ni gari gani mnaitaka? iweje ktk mitambo ya uzalishaji umeme mnaita walanguzi lama biashara ya Kariakoo..
Mkuu nashindwa kuelewa kwa nini tuliweka tender ikiwa sisi tunachotafuta ni kununua mtambo na sii shirika la kuendesha ufuaji umeme, hainingii akilini na sidhani kama viongozi wetu huwa wanaweka temder wanapotaka kununua hayo mashangingi. Majuzi wamenunua BMW za Ikulu sikuona tender kutafuta wachuuzi ila walikwenda BMW kwenyewe wakapewa agent anaye deal na nchi zetu iweje ktk swala zito kama la Umeme mnaweka tender..
Licha ya yote hayo mkuu wangu nizungumze mara ngapi?.. nasema tena niliwafuata viongozi waloandamana na Lowassa hapa, nikawambia uwezekano wa kupata mitambo kama hiyo kwa bei nafuu kabisa lakini Richmond ndio iliyopendekezwa na kusifiwa kwa kila hotuba ya viongozi wetu... Licha yangu kuna vijana kibao hapa walisema wazi kuhusiana na Richmond mara tu walipopewa tender na gharama ya mitambo yao inapatikana kwa bei gani mkawapuuza..Haya tazama swala la Dowans tulipiha kelele weee serikali imekuja kubali baafa ya kupata ushauri toka wapi?..Rex Attorneys... yaani kama sii hao wajomba tungeinunua kweli mitambo ya Dowans.
Leo hii imekuwa ni makosa yetu tena! mlitaka tuwe active kiasi gani ikiwa serikali yenyewe inawadharau vijana wake..