TANESCO yatangaza mgawo wa umeme


Duh, poleni sana masaa 13 bila umeme! unajua mkuu wangu kusema kweli Bongo tuna ustaarabu wa kitumwa yaani ile ewallah bwana huku ukicharazwa bakora!..Nashindwa hata kufikiria tu hali hiyo ingetokea nchi hizi kwanza maduka yote yangevunjwa vunjwa, ujambazi ungeongezeka mara 10, billions na mabillioni ya hasara zingetokea acha mbali hasara za viwanda na biashara za watu...Nina hakika rais au waziri mkuu angetakiwa kujiuzuru mara moja!... Sii nchi ya Wadanganyika ambayo kila kitu ni Mungu hakutujalia!

Hata hivyo tumsubiri Zitto atuletee habari kamili nini Tanesco wamejibu..inashangaza sana kuona generators za Songos na mashirika mengine zilizowekwa majuzi tu (less than 4 years) tayari imekwisha haribika beyond repair!. kisha tunaambiwa mitambo hiyo ilikuwa mipya!
 
Hili tatizo la umeme linachukua miongo mingapi kulitatua? Maana tokea niko shule ya vidudu mpaka sasa na approach miaka 40 bado lipo tu....why?

Shida ni pale mpangaji anapolalama na tatizo la umeme ... ebo kwani mie Tanesco kama vipi weka generata ukihama hama nalo.
 
Poleni sana lakini mkome kuchagua CCM kwa madai wapinzani hawako tayari,nimekaa states zaidi ya miak kumi sijawahi kuona umeme ukikatika kwa hiyo hata home inawezekana,tatizo ni CCM tuu!
 
Tutaishi maisha haya ya kubahatisha mpaka lini? Tz imekua haina kitu ambacho kitaendeshwa bila ya kuleta maendeleo, sasa wametangaza mgao, haya matatizo yatakwisha lini. yaani nilivyokasirika nashindwa hatakuendelea kuandika, wacha niishie hapa, maana hii ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa
 
Kuna kazi kubwa sana katika siasa za Tanzania maana kila mtu ni msemaji wa mambo muhimu katika Taifa letu. Inasikitisha sana
 
Kaka i would do the same with TPDC and STAMICO. These Parastatals have to be guided like nothing. They are potential champions of our economy - TANESCO; TPDC and STAMICO!
Kama mashirika haya yanahitaji guidance ya kiwango hicho ujue tatizo hasa ni Menejimenti unayoisifia hapa kwamba wanakaribia kutengeneza faida! Usidanganywe na uandikaji wa vitabu vya mahesabu ya mashirika haya au ukaguzi unaofanywa na CAG. Vyote ni vya kubumba na usanii mtupu. Kiini cha matatizo ya mashirika ya UMMA ni ulafi wa ninyi wanasiasa wetu ambao umezipa mianya menejimenti za mashirika haya kuyatafuna kwelikweli.
Hebu fikiria waziri anapojengewa nyumba ya milioni 500 na shirika lililo chini ya wizara yake au anapopewa kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya kampeni mwakani. Rushwa hi imekomaa sana kwenye wizara nyingi na mashirika yake na ushahidi wake ni mgumu mno. Waziri wa kazi anaishi hivo na NSSF yake; waziri wa maji anaishi hivo na DAWASA na mamlaka nyingine za maji mijini; Waziri wa miundombinu anaishi hivo na mameneja wa TANROADS wa mikoa;.......Kamati zenu za Bunge nazo mkipita huko mnalambishwa bahasha nzitonzito; mambo ni magumu mno hadi pale wanasiasa wala rushwa watakapodhibitiwa kwa sheria kama zile za CHINA.
 
Bado mimi napata shida katika kujua kwa kiasi gani watu kama hawa mawazo yao yanavyoweza kuwa sio ya maana na kuona ni kitu cha kawaida sana. hivyo hata kama iwe vipi bado watu watasema tu maana mpaka lile tatizo la msingi liishe kabisa
 
ukosefu wa viongozi walio na mwanga wa mawazo ndio uliotufikisha katika tatizo hili lisilo la lazima la upungufu wa umeme.

akina mwakyembe, shelukindo na wenzao wanajijenga kisiasa kupitia hoja rahisi kama hii ya DOWANS..

Tunakosaa visionary leaders wenye kuweka masilahi ya taifa mbele zaidi kuliko masilahi yao ya kupita ya kisiasa.

pia poor decision making process ya serikali,bunge vimetufikishaa hapa tulipoooo.
waziri wa nishati anapata kazi rahisi kutokuwajibika kutokana na kuzungukwaa na viongozii wababaishaji kama bunge.

leo tuna mgawoo wa umeme kwa tahadhariii amabayoo ilitolewaa mapemaaaaa..
je hiyoo mitambooo mipyaa mbonaa haijanunuliwaa mpaka sasa?

tusonge mbele kwa kuwa na upeo wa mbelee zaidiii kulikooo siasaaa za kichovuuu
 
tanzania tunachokosa ni kitu kimoja kikubwa,kuchanganya SIASA na TAALUMA( Politics with Technical issues), yapo mambo ambayo siasa inatakiwa iyaongelee baada ya Technical part kuapprove 100%, tena bila kuingiliwa! kwa mtindo huu wa kutojali taaluma za watu ndo inatufikisha huku tulipo,tupo almost 80yrs back,still tunajisifia tunao viongozi bila vission,mission na objectives, tutafika wapi,kama karne hii nchi inashondwa kuzalisha umeme wa just few Mw's? mito,maziwa,natural gas, vyote hivi ni natural, tumepewa na Mungu mwenyezi bureee, ni kutumia tuu. Mimi kama ningekuwa president na mawaziri, makatibu wakuu wote kwanza hata suti singevaa,safari za nje kwa wenzetu ningeona aibu kwenda sababu ninaonekana kama chizi, daily safari zoote huwezi hata kucopy and paste? wananchi tupo duni and ni rahisi sana kuwaongoza but still tumelala! inatia hasira na karaha! namini tumelaaniwa na shetani kwani hata yeye hawezi kuishi tz!!
 
Zitto alikuwa sahihi kwenye hili na kama kawaida yetu tuliacha kufuata ushauri wa kitaalam tukavamia ushabiki wa maneno ya "wapiganaji" leo taifa linaingia kwenye kiza anaeumia ni mwananchi wa kawaida.

Akina Mwakyembe na genge lake nyuso zimewashuka wanaona hata haya kusema kitu.
 
Jamani hivi hiyo mitambo ya Dowans ingenunuliwa ndio tusingekuwa na mgao sasa hivi??

Oh my God!!
 
Mimi si mshabiki wa Chadema kama chama lakini kuna viongozi na wa admire ambao ni slaa na Zitto. lakini wengine wote ni pasua kichwa yaani wale wale!!! wakipewa nafasi tutarudi miaka mingi nyuma... nawashauri watafute chama kingine huko waliko wamepotea tena sanaaaaaa! hatuhitaji conservative na mabepari Tanzania tutakwisha kuibiwa.
 

Nakubaliana na wewe asilimia 100. Upo sahihi kabisa na ndivyo hali ilivyo. Ndiyo hali ninayopigana nayo. Soma ripoti yangu ya mwaka niliyotoa Aprili 2009 Bungeni.
Nimekuwa nikipigana wabunge wasiwe wajumbe wa Bodi za Mashirika haya ili kupunguza 'kugawana' misosi.
Nimepigania sana kuanzishwa kwa Office of State Entreprises ili kudhibiti mashirika na bodi zao. Au kuimarisha ofisi ya Treasury registrar.
Nimepigania Bodi kupewa mikataba ili kuwadhibiti.
Hawa wnasiasa wote wa CCM hawa mnaowasikia wanapiga kelele wamo kwenye mabodi au marafiki zao wamo kwa mabodi na wananipiga vita kwa kuwapinga. Lakini sitaacha maana ninaamini ni njia sahihi.

Nakubali mawaziri wanatumia vibaya mashirika yao, mawaziri wote kabisa na ninagombana nao sana. The other day i invoked act no. 3 to detain Mary Nagu and she ran from Dodoma and by the time parliamentary officer found her in Dar she had rectified what she did for NDC. I was to do the same to Ngeleja for not appointing TPDC Board for two years!

Nakubaliana na wewe kabisa na ndio maana nasema sisi wanasiasa tufanye oversight (our constitutional role). Wataalamu wafanye kazi zao. Lakini sisi tunawapowaingilia katika kazi zao ndio tunaharibu. Thats my stand kaka!
 
Mimi naamini Zitto Kabwe ni mwanasiasa wa mfano kwa vijana wengi huko tuendako. Na ninaamini alikuwa na bado yuko sahihi katika hili la umeme kwasababu zifuatazo;
1. Zitto ameonesha kwamba yupo tayari kufanya maamuzi kitaalamu zaidi kuliko kisiasa hata kama maamuzi hayo ni unpupolar...kitu ambacho JK ana CCM wanakikosa mno.
2. Zitto anaweza kusimamia maamuzi unpopular bila kuyumba mpaka anapoamini vinginevyo. Nakumbuka Mzee Ndesambulo alikaririwa na TanzaniaDaima la Jumapili wakati huo akionya hatari ya nchi kuingia giza kama taifa litaendekeza cheap politics...badae akachimba baada ya kuona ngoma ya siasa za bei nafuu inakuwa nzito kufunika taalama yake ya biashara.
3.Engineer Stella Manyanya, mwanamke wa kilokole, ambae ni mmoja wa wajumbe wa ilikuwa kamati ya kuchunguza Richmond, alikaririwa na gazeti la majira akionesha kutokuwa na wasiwasi kwa hoja kuwa kinachotakiwa sio mkataba, ni mitambo ya kunusuru taifa dhidi ya mgawo.
4.Profesa Lipumba, akizungumza kama mtaalamu wa masuala ya uchumi mbele ya wahariri wa Tanzania alionesha hilo, na kushauri ununuzi wa mitambo kwa misingi ya ubora wake na unafuu wa gharama bila kujali inauzwa na nani, cha msingi taratibu za manunuzi zifuatwe.
5.Dr Lwaitama pia alisisitiza msimamo wa kununua mitambo kwa hoja za kitaalamu zaidi kuliko siasa, hasa katika mazingira ya kwetu ambapo siasa zinaendeshwa kienyeji mno, hakuna professionalism...ndo sababu akamsifu zitto katika hili.
6.Mmoja wa washauri waandamizi katika masuala ya nishati pale benki ya dunia, Engineer Ralph Karhammar alisema suala la ununuzi wa mitambo ya Dowans limebebwa na siasa kiasi cha kuvuka mijadala ya kitaalamu..
7. Mimi narudia kusisitiza, kwamba uahaba wa umeme kwa sasa kutokana na mapungufu yaliyojitokeza bado hayafikii 100MG...kama tungefanya mamuzi sahihi kitaalamu tusingetaabika na mgawo unao tukabilli sasa...tatizo la umeme tanzania kwa sehemu kubwa msingi wake sio uongozi wa tanesco, ni uongozi wa nchi....mimi nimepata kuona mipango mikubwa sana ya tanesco ya namna ya kukabiliana na tatizo la umeme kwa miaka mingi ijayo. lakini serikali haitekelezi, inabaki inaendesha sekta ya umeme ki misheni town, matokeo yake inaonekana tanesco kila kukicha wakija na mipango ya dharula, sio tanesco unayotaka haya, ni serikali ya JK.......mimi naamini tunahitaji kubadili mwelekeo wa siasa zetu, tukiacha taifa liendeshwe kwa misingi ya nani ana influence ya media, nani hana, tumekwisha!.....
 
sphist unapaswa kujua kuwa tanesco ni shirika kubwa sana, na mafanikio yake kwa sehemu kubwa yanategemea ufanisi wa serikali...tanesco imekwishawasilisha mikakati ya umeme tanzania kwa miongo kadhaa ijayo, serikali haitekelezi, tanesco wafanyaje?
 

Hapa umenena. Kwa kuongezea tuu. Wakuu wa haya mashirika wasiteuliwe na Rais. Kazi hiyo iachiwe bodi. Kwa kuteuliwa na Rais kunawapa kinga dhidi ya bodi na kuifanya ishindwe kufanya kazi yake ambayo ni kudhibiti menejimenti!

Amandla......
 

Hivi wewe mwenzangu umesoma hicho kilichoandikwa na Mbala-mwezi na kukielewa au umejibu tu bila kusoma? Maana naona ulichojibu hakiendani kabisa na hoja za msingi za makala husika.
 
Si vibaya tukajikumbusha wizi uliofanywa na Richmond/Dowans hasa kwa wale wanaolaumu Watanzania walio wengi kupinga kununuliwa kwa mtambo wao kama tulivyoshinikizwa na MD wa TANESCO, Idrissa Rashid

Siri ya wizi mkubwa Richmond

Mwandishi Wetu Januari 28, 2009
Raia Mwema~Muungwana ni Vitendo

Watimka na mabilioni ya walipa kodi

Walichotewa kabla hata ya kazi

WAKATI Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akisubiriwa na wabunge kuwasilisha taarifa ya Serikali kuhusu utekelezaji wa mapendekezo ya Bunge kuhusu kampuni ya Richmond Development, kampuni hiyo iliyorithiwa na kampuni ya Dowans, ilitokomea na zaidi ya Sh. bilioni 23, Raia Mwema imebaini.

Kinyume cha maelezo yaliyowahi kutolewa na baadhi ya viongozi wakuu serikalini katika Bunge, kwamba Richmond haikuwahi kupewa fedha za Serikali, ukweli ni kwamba kampuni hiyo ilichotewa zaidi ya Sh. bilioni 30 (Dola 30,696,598 za Marekani).

Kiasi hicho ni sawa na asilimia 35 ya gharama ya kodi ambayo msingi wake ulikuwa kufanikisha mchakato wa ufunguaji wa hati ya muamana (letter of credit) kati ya kampuni hiyo na Benki ya Biashara.

Malipo hayo ya asilimia 35 ni utekelezaji wa makubalino yaliyofikiwa awali, kati ya Serikali na wawakilishi wa kampuni ya Richmond Development.

Uchunguzi wa Raia Mwema umebaini kuwa baada ya kupewa kitita hicho cha zaidi ya Sh bilioni 30, Richmond ilipewa masharti ya kurejesha fedha hizo serikalini katika malipo ambayo yangefanyika kwa awamu tatu.

Hesabu zilizofanywa ni kwamba Richmond ilitakiwa kurejesha serikalini dola 1,279,044 za Marekani (zaidi ya Sh bilioni 1.3), kila mwezi, lakini katika mikupuo (awamu) mitatu.

Hesabu hizo zinabainisha kuwa kama makubaliano hayo yangefanyika bila ukorofi au kasoro yoyote, Richmond ingefanikiwa kurejesha serikalini fedha ilizopewa katika miaka miwili. Kwa tafsiri nyingine ni kwamba, Richmond ingelipa deni hilo serikalini ndani ya muda wa uhai wa mkataba wake na Serikali, ambao ni miaka miwili.

Lakini uchunguzi zaidi wa Raia Mwema umebaini kuwa malipo ya awali yalipaswa kuanza kufanyika Novemba, mwaka 2007. Hata hivyo, kutokana na utata wa kampuni ya Richmond hasa kwa upande wa uwezo wake kiteknolojia na utendaji, kampuni hiyo iliuza shughuli zake kwa kampuni nyingine binafsi ya Dowans.

Imebainika kuwa wakati mchakato wa uuzaji wa shughuli za kampuni hiyo kwa Dowans unafanyika, Richmond ilikuwa haijarejesha fedha ilizopewa na Serikali na kwa kuwa Dowans ndiyo iliyobeba mikoba, ilipaswa kuendeleza urejeshaji huo wa fedha.

Kutokana na hali hiyo ya fedha za Serikali kubaki kwa 'wawekezaji' hao waliopasiana mpira wa uwajibikaji, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), kupitia timu ya watalaamu wa sheria, ilichunguza mkataba kati yake na Richmond ambao ulirithiwa na Dowans.

Taarifa ya timu ya wanasheria wa TANESCO ilibaini kuwa mkataba huo hauna nguvu za kisheria na kuamuru uvunjwe. Mkataba ukavunjwa rasmi Agosti mosi, mwaka 2008.

Hata hivyo, wakati mkataba huo unavunjwa uchunguzi wa Raia Mwema umebaini kuwa fedha zilizopaswa kurejeshwa Serikali hazikuwa zimerejeshwa zote.

Imebainika kuwa fedha zilizorejeshwa hadi mkataba unavunjwa ni jumla ya dola 7,674,186 za Marekani (zaidi ya Sh bilioni 7.7), huku dola za Marekani 23,022,412 (zaidi ya Sh. bilioni 23) zikibakia kwa Richmond na mrithi wake Dowans.

Taarifa zaidi za kiuchunguzi zinaeleza kuwa kutokana na hali hiyo Bodi ya TANESCO pamoja na uongozi wa shirika hilo umekwisha kuchukua hatua.

Hizo ni pamoja na maagizo ya Bodi ya TANESCO kwa uongozi wa shirika hilo kuchukua hatua zinazostahili kuhusu deni hilo na kutokana na maagizo hayo, uongozi wa TANESCO ulilazimika kutoa taarifa rasmi serikalini ili hatimaye ijulikane namna fedha hizo zitakavyorejeshwa.

Uchunguzi zaidi umebaini kuwa ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), imechunguza mchakato huo na kubaini kuwa Serikali ilitoa fedha hizo kwa Richmond.

Ofisi hiyo ya CAG, katika taarifa yake ya ukaguzi wa Hesabu za Serikali kwa mwaka ulioishia Desemba 31, mwaka 2007, imeweka bayana kuwa fedha hizo bado hazijarejeshwa serikalini.

"Tunafahamu kutokana na taarifa za uongozi kwamba mkataba kati ya TANESCO na Dowans ulivunjwa Agosti mosi, 2008. Matokeo yake ni kwamba kiasi cha fedha kilichotolewa na kutakiwa kurejeshwa kinaweza kuwa hasara kwa TANESCO au Serikali," inaeleza sehemu ya waraka rasmi wa ofisi ya CAG kwa serikali ambao Raia Mwema imeuona.

Kampuni ya Richmond Development ilipewa zabuni tata na Serikali kuagiza mitambo ili kuzalisha umeme wa dharura nchini.


Kutokana na utata wa zabuni hiyo, Bunge lililazimika kuunda Kamati Teule kuchunguza na kubaini upungufu ambao hatimaye ulimgharimu aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa na mawaziri Nazir Karamagi na Dk. Ibharim Msabaha waliojiuzulu Februari 2008.

Mbali na viongozi hao kujiuzulu, Kamati ya Bunge iliwasilisha mapendekezo 23 yanayohitaji kufanyiwa kazi na Serikali. Mapendekezo hayo ni pamoja na kuwawajibisha baadhi ya watendaji wa Serikali na baadhi ya vyombo nyeti, akiwamo Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Dk. Edward Hosea pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika.

Katika mkutano wa Bunge ulioanza wiki hii, Serikali inatarajiwa kuwasilisha taarifa yake kuhusu utekelezaji wa mapendekezo hayo. Taarifa hiyo inatarajiwa kuwasilishwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
 


Kweli kabisa. Hongera sana kwa uchambuzi wako wa kina na nuunga mkono 100%
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…