Watanganyika! Hebu tusemeni sasa kwa sauti moja kwamba imetosha! naomba kuuliza, hivi ni kitu gani Tanzania kwa sasa kipo shwari? nini kinaendeshwa na kuzaa matunda au kuhudumia wananchi ipasavyo? naomba nikumbushwe labda namwonea bwana mkubwa JK. Kama hakuna, basi naomba niseme kwa sauti kuu, kunajambo la kufanya la sivyo tunakoelekea ni kubaya zaidi, hebu niwakubushe kuwa ni miezi michache iliyopita tulihakikishiwa serikali inanunua mitambo kwa ajili ya kuepusha mgao wa umeme, pia ikasemekana mvua zilinyesha vizuri nmaji yalijaa, sawa najua pia yanapungua, lakini leo kunamgao, madai yao mashine zimeharibika tena zote, ya kihansi na SONGAS zote mara moja! hili linaleta wasiwasi,ukiacha hilo TANESCO wenyewe wanasema mgao ni mdogo lakini umeme unakatwa hata sehemu nyeti za uzalishaji mali, hospitali na balozini, tena kwa saa zaidi ya kumi mchana wakati umeme unahitajika zaidi kuzalisha. Kwangu mimi hii ni hujuma tena ya hali ya juu ilikudhibitisha maneno yaliyokwishasemwa au/na kutoa malipizi kwa mapambano ya ufisasdi yanayoendelea kwani tufahamu kwamba baadhi ya walengwa wapo TANESCO, mimi naamini kwa asilimia kubwa kwamba Huu NI UMAFIA wa baadhi ya watu wachache ambao kwa muda mrefu sasa wamekua wakiuhujumu uchumi wa watanganyika bila huruma ya maisha ya watoto, wajawazito na wazee wanakufa kwa njaa, magonjwa na huduma mbovu wakati nchi yetu ni TAJIRI, nasema haya kwa hasira kwasababu sasa hujuma inafanywa waziwazi bila kujali macho ya watanganyika milioni 40 yanayoshudia. Nasema hukumu ya hawa ni KUTENGANISHWA KICHWA NA KIWILIWILI HADHARANI.